Zitto: Mbowe ni Kiongozi wangu, Tusameheane

Zitto: Mbowe ni Kiongozi wangu, Tusameheane

Kijana kaitambua nafasi ya baba yake safi
 
hicho ulicho kiandika hakipo kwenye account ya zitto kilichopo ni hiki
uploadfromtaptalk1454506051837.jpg
 
Tunaposema Zitto Zuberi Kabwa ni Mwanamapinduzi na Mpinzani pekeee msipayukage mujitahidi kumuelewa kijana yule ana dhamira dhabiti na Taifa hili.. Sio kuanza kuleta mibezo yenu na mapovu kuwajaaa mdomoni kwa kumwita kibaraka La hasha!!!
 
Dogo mjanja sana.

Hapa anaitafuta 2020 kwa ukaribu sana. Kwasisi wenye macho mpaka kisogoni tumeshaling'amua hili.

Kila lakheri kwake

BACK TANGANYIKA
 
Kuna watu wakisikia hizi kauli za kupatana hawa magwiji wa siasa za nchi hii.Roho zinawauma sana kama vipi wanywe marimao.
 
Je wale waliomuunga mkono Mbowe na kumwita Zitto msaliti nao wamemsamehe Zitto. ?

Vipi wale waliofukuzwa na Zitto Chadema nao wamemsamehe Mbowe. ?

Watanzania tutakuja kuendelea tu pale tutakapogundua ulaghai wa wanasiasa.
 
Hizo ndo siasa...Ugomvi wa Zitto na CDM ulisababisha baadhi ya watu hawapatani hadi leo..watu hao sijui wanajisikiaje kwa sasa
 
Akileta zake tunamzingua tena kama kawa, sisi ndio CDM, tunaijua siasa vizuri sana. Hakuna mwanasiasa aliyefanya siasa kwa mafanikio makubwa katika nchi hii kama Mbowe. Jamaa ni genius. Zitto anajifanya mjanja lakini kwa Freeman amechemka. Kupatana kwao sio bure, lazima kuna kitu Mbowe anakitafuta, maana hafanyi siasa kihasara. Tuendelee kusubiri!!
 
Zitto ndumilakuwili asidhani anapata cheo cha kuteuliwa na mbowe katika mawazir vivuli
 
Zitto namkubali sana ila hivi sasa nimeona ipo haja ya kumewekea censor maalum za ku detect dhamira yake.
 
Mbowe huwa Ana busara sana. Inshaallah mungu amuweke. Hashindwi kumeza matapishi yake hasa pale anapoona Pana maslahi ya wengi ambao ni watanzania ambao anawapigania kila siku. Nadhani sasa ni muda wa kuganga yajayo. Taifa linawahitaji sana wapinzani wa kweli hasa kipindi hiki tunachopitia cha ukoloni mamboleo
 
Nisaidieni kumuita Aibibu Nchange asome hapa
 
Soon na Dr Slaa naye atapatana na Mbowe, waliokuwa wakimwita kila aina ya majina mabaya sijui nao watapatana naye,yaelekea kuna watu huwa wanachukia watu wengine kwa kufuata mkumbo tu,lakini hata wao wenyewe hawajui kwanini wanamchukia mtu huyo,ni kwasababu wamemsikia mtu flani wanayemuabudu akimchukia mtu huyo.In the same way watarudisha upendo tena kiurahisi mno kwa huyo mtu bila hata wao wenyewe kujijua.They're simply acting like programmed robots.
 
Back
Top Bottom