Zitto: Kwanini Serikali inaogopa Wachunguzi wa Kimataifa? Ushauri wa Lema swadakta

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Kwanini Serikali inaogopa Wachunguzi wa Kimataifa? Ushauri wa Lema swadakta

Zitto Kabwe, Mb
Jana Jumanne, siku ya 6 tangu Mohammed Dewji, Mfanyabiashara na Mlezi wa Klabu ya Simba atekwe nyara, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani Bwana Godbless Lema alitoa pendekezo kuwa Serikali ya Tanzania iombe msaada wa nje kuongeza juhudi za kumtafuta na kumwokoa Mohammed. Jana hiyo hiyo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Masauni alijibu kuwa Serikali haitafanya hivyo kwa sababu jeshi la polisi nchini lina uwezo na utaalamu wa kutosha kuendelea na uchunguzi. Naibu Waziri hayupo sahihi kukataa pendekezo la Waziri Kivuli.

Nashauri kuwa pendekezo la Waziri Kivuli lichukuliwe kwa uzito unaostahili. Uchunguzi wa kutekwa kwa Mo unapaswa kuwa nguvu kubwa ili kuondoa taswira iliyoanza kujengeka nchini kuwa watu wanaweza kutekwa na hakuna kinachofanyika. Uchunguzi huru wa kimataifa utasaidia sana kurejesha imani ya raia na kuwaondolea hofu kuwa wakati wowote wanaweza kutekwa au hata kushambuliwa.

Matukio ya kupotea kwa Afisa Utafiti na Sera wa CHADEMA Ben Saanane, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo Simon Kanguye, Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda na kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yanadhihirisha kwa kiasi kikubwa sana vikwazo kadha wa kadha ambavyo polisi wetu wanakumbana navyo Katika Uchunguzi wa masuala kama haya ya jinai. Vikwazo hivi ambavyo vingine ni vya kitaasisi, vinaonekana pia kwenye suala la utekwaji nyara wa MO.

Nilifuatilia kwa kina sana suala la Ben Saanane na Simon Kanguye. Pia nilipata Taarifa za awali za kupotea kwa Azory Gwanda kabla ya Taarifa hizo kujulikana kwa Umma. Niligundua kuwa Jeshi letu la Polisi lina watu wenye Nia ya dhati ya kukomesha matukio haya lakini wanafika mahala wanakwama. Jeshi la Polisi lilifuatilia suala la Ben Saanane kwa kina Lakini walikwama mahala ambapo waligundua kuwa taasisi nyingine ya Serikali ina mkono. Polisi waliishia hapo na hawakuendelea tena na suala la Ben Saanane. Vile vile suala la Simon Kanguye, Polisi kuanzia Kibondo mkoani Kigoma mpaka makao makuu ilifika mahala walifungwa mikono na kutoendelea na suala hilo. Nilifuatilia pia suala la Tundu kwa kina kwa kutumia mahusiano yangu na Vijana wapelelezi wazuri ndani ya jeshi la Polisi na kugundua kuwa Polisi walikatazwa hata kufungua file la Uchunguzi.

Mazingira haya yanaonyesha kuwa wakati mwengine huwa tunashambulia sana Jeshi la Polisi na wao hawawezi kujitetea Lakini wanakuwa wameshikwa mikono. Hata hivyo kwa kuwa wao Ndio wenye mamlaka ya usalama wetu hawana namna lazima wapokee lawama zote. Njia pekee ya wao kuondokana na lawama hizi ni Serikali kuruhusu Uchunguzi wa Kimataifa kwenye suala la kutekwa kwa MO. Nimeshangazwa sana kuwa Waziri wa Polisi amekuwa mbele kukataa pendekezo hili.

Kuna maswali Hayana majibu Katika Uchunguzi wa suala la Mohammed Dewji. Baadhi ya vyombo vya Habari wameanza kuyachambua Mambo ambayo baadhi yetu waliyahoji mapema sana. Kwa Mfano, rafiki yangu mmoja aliamua kuhesabu CCTV camera kuanzia mataa ya Kanisa la Mtakatifu Petro mpaka panapoitwa kilimanyege na kukuta camera 30 zikiwemo camera zenye nguvu sana kutoka makao makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa yaliyopo mtaa huo wa Haile Selasie. Haiwezekani kuwa mpaka leo ‘footages’ za camera hizi hazijachunguzwa na kupata Namba za gari zilizotumika kufanya utekaji huu na kisha kutambua umiliki wa gari hizi na kupata njia ya kumfikia MO alipo. Jeshi la Polisi linasema camera za hoteli ya collosium zilichezewa, watekaji hawawezi kuchezea camera za mtaa Mzima. Polisi wakipata msaada wa wenzao kutoka nje wanaweza kupata jawabu ya hili.

Jambo lingine ni kuwa kuna kauli tata Kuhusu utekwaji wa Mohammed. Mwanzoni kabisa Polisi walisema kuwa MO alitii kukamatwa hakufanya harakati zozote. Hata hivyo ukweli umeanza kutoka kuwa MO alipambana. Katika kupambana alipiga kelele walinzi wasifungue geti la kutokea collosium Ndio maana watekaji wakapiga risasi Juu na kufungua geti wenyewe. Vile vile kiatu kimoja cha MO kilivuka na pia kofia ilivuka. MO Katika kuona anazidiwa alidondosha funguo ya Gari yake na simu ( naamini kuwa alidondosha funguo ya gari makusudi ili watu wachukue Gari kukimbiza watekaji). Bahati mbaya hapakuwa na mtu aliyethubutu kuwakimbiza watekaji wale. Kwanini hizi taarifa hazikutolewa kwenye press ya Mkuu wa Mkoa wa ZPC? Kwanini Umma uliambiwa kuwa MO alikubali tu kubebwa?

Jambo la mwisho kwa leo, ni la kawaida kwenye mambo ya Uchunguzi, ni ganda la risasi ambayo ilitumika. Limeokotwa na Polisi? Kinachoitwa ‘ballistic report’ kimetolewa na kusambazwa duniani kwenye kanzidata za watengeneza silaha? Hii ingesaidia sana kuweza kujua umiliki wa silaha iliyotumika na kuwa na njia ya kuwapata watekaji na pia kumpata MO. Jeshi la Polisi likipata msaada kutoka nje ya nchi laweza pia kufanikisha hili.

Mwisho, kumekuwa na kauli za kusema kuwa ‘wanasiasa wasitake umaarufu’ kwenye tukio hili. Hii ni kauli ya hovyo na inapaswa kupuuzwa. Mamlaka za Serikali zimejengwa kusimamiana. Waziri Kivuli Godbless Lema ana wajibu wa kumhoji Waziri wa Mambo ya Ndani bila kuonekana anaingiza Siasa. Hakuna kipindi Serikali imepewa fursa ya kupumua kwenye tukio kama tukio hili la kutekwa kwa Mohammed Dewji. Wanasiasa wa upinzani tulikaa kimya kupisha vyombo kufanya kazi zake. Serikali kuanza kuweweseka pale wabunge wanapotimiza wajibu wao kuhoji kunatia mashaka Kwamba kuna kitu Serikali inaogopa. Serikali inaogopa nini? Wanachokiogopa Ndio kinaogopesha kukaribisha Wachunguzi wa Kimataifa?

Zitto Kabwe, Mb

Buzebazeba, Kigoma Ujiji

17/10/2018
 
Word!

Lakini Mkuu, kila Serikali huwa na itikadi, msimamo na sera zake. Hii ya sasa inatazama wachunguzi wa nje/wa kimataifa kama watakaoionyesha Serikali kushindwa katika kuchunguza na kushughulikia masuala ya kiusalama.

Kwa msimamo wao, wako sahihi ingawa demokrasia inaruhusu kutofautiana nao.

Piga kazi Mkuu Zitto. Mambo yote yapo 2020!
 
Profession zikiingiliwa na wanasiasa au zikichanganywa na siasa hazijawahi kufanya kazi zikafanikiwa!

Tanzania unakuta suala linalohusu utatuzi kwa njia ya kitaalam wanaokuwa mstari wa mbele ni wanasiasa badala ya wataalam.

Mtu hajui hata masuala ya kiuchunguzi na athari zake kijamii na kitaifa ndio yuko kwenye media akitoa ushauri na maelekezo mbali mbali!

Inashangaza kuona hata media nchini zinahoji wanasiasa wenye fani za dini au uchumi kwenye suala la kichunguzi kuhusu utekaji badala ya kutafuta watalaam wa masuala ya crime investigation and kidnapping!

Eti Mkuu wa Mkoa, Waziri wa Mambo ya ndani, Waziri kivuli wa Mambo ya ndani na wanasiasa wengine kama Zitto ndio wamekuwa waeleza mbinu za kichunguzi kuhusu Utekaji!

Wengine eti wanataka waambiwe namba za gari! Hivi mtu anayeamua kufanya tendo la kuteka kwa kutumia gari anaweza kuweka namba halali za gari yake? What if, namba bandia zilizowekwa niza gari la mwanasiasa fulani wa CCM au Upinzani ili kupoteza malengo ya kiuchunguzi?

Tanzania kuna vituko!

Dhana ya kusema lazima tupate wachunguzi wa kutoka nje ni nzuri sana kisiasa/wanasiasa lakini swali muhimu kitaalam linabaki, je, nini athari zake kiulinzi kitaifa baada ya uchunguzi kwa sababu wachunguzi wa nje watakapokuja watataka kujua uimara na udhaifu wa vyombo vya ulinzi nchini. Ni sawa na kuikabidhi nchi kwa vyombo vya ulinzi vya nchi nyingine. Hili kitaalam haliwezi kukubalika hasa kwenye nchi zetu ambazo bado tatizo la mapinduzi ya kijeshi au njia ya ''divide na rule'' ni njia ya kuiondoa serikali madarakani.

Kikubwa zaidi, serikali za nchi za Africa zilizoruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia katika taasisi zao za ulinzi zimejikuta zikianguka au kuondolewa madarakani kwa nguvu.

Tuache kudanganyana. Hakuna urafiki kwenye masuala ya ulinzi hasa katika zama hizi za vita vya kiuchumi ambavyo msingi wake sio uimara wa uchumi bali uimara wa vyombo vya ulinzi.

Marekani na Uingereza ni marafiki wa karibu lakini urafiki wao kiulinzi sio open ended ndio maana wanachunguzana wao kwa wao mienendo yao kwa siri.

Kwa wale wanafuatilia siasa za nje watafahamu kuwa hata suala la yule mwandishi wa Saudi Arabia, Jamal Ahmad Khashoggi limegundulika baada ya vinasa sauti na kamera zilizowekwa na vyombo vya ulinzi vya Uturuki nje na ndani bila Ubalozi wa Saudi Arabia kufahamu ambazo zilimnasa akiingia na akiwa ndani. Ieleweke kuwa kuweka vyombo vya kunasa sauti ndani ya Ubalozi wa nchi nyingine ni kosa kisheria kama ilivyoainishwa kwenye Vienna Convention. Hii haijazuia nchi ya Uturuki kufanya udukuzi kwa sababu hata nchi zingine ndivyo zinavyofanya kama vyombo vya ulinzi sio imara kugundua.

Vyombo vya ulinzi wa nchi zingine kuruhusu maeneo ya ulinzi na kazi za ulinzi kujulikana haikubaliki kiulinzi.

Hoja ya wanasiasa ya kusema eti serikali ijisafishe kwa kuleta wachunguzi wa nje ya nchi kwenye masuala ya ulinzi zina mashiko kisiasa lakini ni suala la kipuuzi kiulinzi na kitaalam.

Tuache kufanya siasa kwenye kazi za kitaalam zinazohitaji wataalam wa masuala ya ulinzi na usalama nchini.

Ni kweli jukumu namba moja la serikali ni kulinda raia wake lakini serikali makini haiwezi kudhoofisha ulinzi wa Taifa lote kwa maslahi ya mwananchi mmoja au wachache.
 
Upinzani chadema, Zito Kabwe wanavalia njuga kupotea kwa mwana CCM Dewji kwamba, Serikali inayoongozwa na CCM haimtendei haki Mwanachama wake, yaani chadema na Zito Kabwe wanamtetea mwana CCM hapo sasa, kweli siku za mwisho alizoahidi Yesu zimekaribia kufika, Chadema wanamtetea mwana CCM???
 
Kwanini Serikali inaogopa Wachunguzi wa Kimataifa? Ushauri wa Lema swadakta

Zitto Kabwe, Mb
Jana Jumanne, siku ya 6 tangu Mohammed Dewji, Mfanyabiashara na Mlezi wa Klabu ya Simba atekwe nyara, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani Bwana Godbless Lema alitoa pendekezo kuwa Serikali ya Tanzania iombe msaada wa nje kuongeza juhudi za kumtafuta na kumwokoa Mohammed. Jana hiyo hiyo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Masauni alijibu kuwa Serikali haitafanya hivyo kwa sababu jeshi la polisi nchini lina uwezo na utaalamu wa kutosha kuendelea na uchunguzi. Naibu Waziri hayupo sahihi kukataa pendekezo la Waziri Kivuli.

Nashauri kuwa pendekezo la Waziri Kivuli lichukuliwe kwa uzito unaostahili. Uchunguzi wa kutekwa kwa Mo unapaswa kuwa nguvu kubwa ili kuondoa taswira iliyoanza kujengeka nchini kuwa watu wanaweza kutekwa na hakuna kinachofanyika. Uchunguzi huru wa kimataifa utasaidia sana kurejesha imani ya raia na kuwaondolea hofu kuwa wakati wowote wanaweza kutekwa au hata kushambuliwa.

Matukio ya kupotea kwa Afisa Utafiti na Sera wa CHADEMA Ben Saanane, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo Simon Kanguye, Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda na kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yanadhihirisha kwa kiasi kikubwa sana vikwazo kadha wa kadha ambavyo polisi wetu wanakumbana navyo Katika Uchunguzi wa masuala kama haya ya jinai. Vikwazo hivi ambavyo vingine ni vya kitaasisi, vinaonekana pia kwenye suala la utekwaji nyara wa MO.

Nilifuatilia kwa kina sana suala la Ben Saanane na Simon Kanguye. Pia nilipata Taarifa za awali za kupotea kwa Azory Gwanda kabla ya Taarifa hizo kujulikana kwa Umma. Niligundua kuwa Jeshi letu la Polisi lina watu wenye Nia ya dhati ya kukomesha matukio haya lakini wanafika mahala wanakwama. Jeshi la Polisi lilifuatilia suala la Ben Saanane kwa kina Lakini walikwama mahala ambapo waligundua kuwa taasisi nyingine ya Serikali ina mkono. Polisi waliishia hapo na hawakuendelea tena na suala la Ben Saanane. Vile vile suala la Simon Kanguye, Polisi kuanzia Kibondo mkoani Kigoma mpaka makao makuu ilifika mahala walifungwa mikono na kutoendelea na suala hilo. Nilifuatilia pia suala la Tundu kwa kina kwa kutumia mahusiano yangu na Vijana wapelelezi wazuri ndani ya jeshi la Polisi na kugundua kuwa Polisi walikatazwa hata kufungua file la Uchunguzi.

Mazingira haya yanaonyesha kuwa wakati mwengine huwa tunashambulia sana Jeshi la Polisi na wao hawawezi kujitetea Lakini wanakuwa wameshikwa mikono. Hata hivyo kwa kuwa wao Ndio wenye mamlaka ya usalama wetu hawana namna lazima wapokee lawama zote. Njia pekee ya wao kuondokana na lawama hizi ni Serikali kuruhusu Uchunguzi wa Kimataifa kwenye suala la kutekwa kwa MO. Nimeshangazwa sana kuwa Waziri wa Polisi amekuwa mbele kukataa pendekezo hili.

Kuna maswali Hayana majibu Katika Uchunguzi wa suala la Mohammed Dewji. Baadhi ya vyombo vya Habari wameanza kuyachambua Mambo ambayo baadhi yetu waliyahoji mapema sana. Kwa Mfano, rafiki yangu mmoja aliamua kuhesabu CCTV camera kuanzia mataa ya Kanisa la Mtakatifu Petro mpaka panapoitwa kilimanyege na kukuta camera 30 zikiwemo camera zenye nguvu sana kutoka makao makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa yaliyopo mtaa huo wa Haile Selasie. Haiwezekani kuwa mpaka leo ‘footages’ za camera hizi hazijachunguzwa na kupata Namba za gari zilizotumika kufanya utekaji huu na kisha kutambua umiliki wa gari hizi na kupata njia ya kumfikia MO alipo. Jeshi la Polisi linasema camera za hoteli ya collosium zilichezewa, watekaji hawawezi kuchezea camera za mtaa Mzima. Polisi wakipata msaada wa wenzao kutoka nje wanaweza kupata jawabu ya hili.

Jambo lingine ni kuwa kuna kauli tata Kuhusu utekwaji wa Mohammed. Mwanzoni kabisa Polisi walisema kuwa MO alitii kukamatwa hakufanya harakati zozote. Hata hivyo ukweli umeanza kutoka kuwa MO alipambana. Katika kupambana alipiga kelele walinzi wasifungue geti la kutokea collosium Ndio maana watekaji wakapiga risasi Juu na kufungua geti wenyewe. Vile vile kiatu kimoja cha MO kilivuka na pia kofia ilivuka. MO Katika kuona anazidiwa alidondosha funguo ya Gari yake na simu ( naamini kuwa alidondosha funguo ya gari makusudi ili watu wachukue Gari kukimbiza watekaji). Bahati mbaya hapakuwa na mtu aliyethubutu kuwakimbiza watekaji wale. Kwanini hizi taarifa hazikutolewa kwenye press ya Mkuu wa Mkoa wa ZPC? Kwanini Umma uliambiwa kuwa MO alikubali tu kubebwa?

Jambo la mwisho kwa leo, ni la kawaida kwenye mambo ya Uchunguzi, ni ganda la risasi ambayo ilitumika. Limeokotwa na Polisi? Kinachoitwa ‘ballistic report’ kimetolewa na kusambazwa duniani kwenye kanzidata za watengeneza silaha? Hii ingesaidia sana kuweza kujua umiliki wa silaha iliyotumika na kuwa na njia ya kuwapata watekaji na pia kumpata MO. Jeshi la Polisi likipata msaada kutoka nje ya nchi laweza pia kufanikisha hili.

Mwisho, kumekuwa na kauli za kusema kuwa ‘wanasiasa wasitake umaarufu’ kwenye tukio hili. Hii ni kauli ya hovyo na inapaswa kupuuzwa. Mamlaka za Serikali zimejengwa kusimamiana. Waziri Kivuli Godbless Lema ana wajibu wa kumhoji Waziri wa Mambo ya Ndani bila kuonekana anaingiza Siasa. Hakuna kipindi Serikali imepewa fursa ya kupumua kwenye tukio kama tukio hili la kutekwa kwa Mohammed Dewji. Wanasiasa wa upinzani tulikaa kimya kupisha vyombo kufanya kazi zake. Serikali kuanza kuweweseka pale wabunge wanapotimiza wajibu wao kuhoji kunatia mashaka Kwamba kuna kitu Serikali inaogopa. Serikali inaogopa nini? Wanachokiogopa Ndio kinaogopesha kukaribisha Wachunguzi wa Kimataifa?

Zitto Kabwe, Mb

Buzebazeba, Kigoma Ujiji

17/10/2018
Sawasawa Mheshimiwa!
 
Hakika. Umezungumza vyema.

Naomba nikuulize swali moja Mh Mbunge. Swali hili litatoka nje ya Mara kidogo lakini siyo mbali sana.

SWALI LENYEWE:
Polisi wanaapa kuzitunza siri zote za kipolisi na nchi kwa ujumla. Huku ni pamoja na shughuli za intellijensia zinazoendelea.

Pamoja na kuwa huenda vijana wanaokupa taarifa za matukio unadhani wanafanya vema, lakini ukweli ni kwamba wanavunja taratibu za kazi yao. Ipo siku nawe huenda ukafanya jambo litakalotishia usalama lakini kwa kuwa kuna vijana wanaokupenyezea taarifa basi kushughulikiwa kwako kutashindikana ama kuchelewa kwa sababu taarifa utakuwa umezipata.

Mara nyingi umekuwa mstari wa mbele katika kupigia kelele juu ya suala la weledi hasa kwa jeshi la polisi pamoja na UWT huku ukisahau kuwa wewe ni mmoja wa wanashusha weledi huo kwa kuvujishiwa taarifa zisizopaswa kutoka nje ya wahusika.
Na hilo umekiri mwenyewe kabisa katika andiko lako hili.

Je, unapata wapi ujasiri wa kulipigia kelele juu ya kufuata taratibu huku mwenyewe ukivunja taratibu zilizowekwa?
 
Word! Lakini Mkuu, kila Serikali huwa na itikadi, msimamo na sera zake. Hii ya sasa inatazama wachunguzi wa nje/wakimataifa kama watakaoionyesha Serikali kushindwa katika kuchunguza na kushughulikia masuala ya kiusalama. Kwa msimamo wao, wako sahihi ingawa demokrasia inaruhusu kutofautiana nao.Piga kazi Mkuu Zitto. Mambo yote yapo 2020!
Hatukatai kuwa kila serikali ina msimamo wake.......

Lakini sasa unawezaje kulinda msimamo huku Jeshi lako likishindwa kuwabaini watekaji??

Ndipo hapo sasa wananchi tunashinikiza kuwa serikali iruhusu wachunguzi wa nje, ili ijinasue katika mtego huu wa kuonekana kuwa "wao" ndiyo wanaohusika
 
Upinzani chadema, Zito Kabwe wanavalia njuga kupotea kwa mwana CCM Dewji kwamba, Serikali inayoongozwa na CCM haimtendei haki Mwanachama wake, yaani chadema na Zito Kabwe wanamtetea mwana CCM hapo sasa, kweli siku za mwisho alizoahidi Yesu zimekaribia kufika, Chadema wanamtetea mwana CCM???
Hivi kutetea haki za binadamu au Uttu ni lazima muwe mnatoka chama kimoja eti?
Ninyi mna matatizo sana na huu ushabiki wenu.
 
Upinzani chadema, Zito Kabwe wanavalia njuga kupotea kwa Mwana CCM Dewji kwamba, Serikali inayoongozwa na CCM haimtendei haki kada wake, hapo sasa, kweli siku za mwisho alizoahidi Yesu zimekaribia kufika, Chadema wanamtetta mwana CCM???
Unaleta UBAGUZI wa kichama eti kisa ni mwanaccm wasilivalie njuga. Huyo ni Mtanzania na amepotea akiwa Mtanzania. Kila Mtanzania mwenye akili timamu lazima avalie njuga jambo hili mpaka MO apatikane!
 
Hapa nimeelewa jambo, Zitto anasema Taasisi ya serikali ina mkono katika upoteaji wa Ben saanane!

Hii ni kwa mujibu wa taarifa alizopata kuwa jeshi lilishindwa kuendelea na uchunguzi baada ya kugundua kuna taasisi ina mkono!Je,taasis hii ni idara ya usalama wa taifa????

Nchi hii imekuwa ya ajabu sana,nchi inashiriki kuwapoteza raia wake kisa itakadi za kisiasa?shame
 
Hatukatai kuwa kila serikali ina msimamo wake.......

Lakini sasa unawezaje kulinda msimamo huku Jeshi lako likishindwa kuwabaini watekaji??

Ndipo hapo sasa wananchi tunashinikiza kuwa serikali iruhusu wachunguzi wa nje, ili ijinasue katika mtego huu wa kuonekana kuwa "wao" ndiyo wanaohusika
Umeambiwa serikali imeshindwa?
 
Back
Top Bottom