Zitto kurudi Bungeni ni ndoto!

Zitto kurudi Bungeni ni ndoto!

Umepaniki mkuu... zitto ameleta maendeleo kigoma kwa fedha zake za mfukoni? Maendeleo yameletwa na serikali. Pia Acha ubaguzi wa kimkoa kusema siasa za kigoma waachiwe wakigoma wenyewe. Halafu mtoa hoja hakuna sehemu amemtaja Dr slaa ni wewe tu umekurupuka.

Hiyo serikali iliyoleta maendeleo ni hihi ya ccm mnayosema haijafanya lolote? Na kama Zitto pamoja na kuwa upinzani aliweza isimamia serikali ikapeleka maendeleo anastahili pongezi maana wengine walifikia uwaziri mkuu wameshindwa kuleta maendeleo kwenye majimbo yao ingawa wanajitapa wanachukia umaskini. Wameshindwa hata kuwasaidia watu wao wameishia kuwa walinzi wa bar halafu eti bila aibu wanajitapa wataleta MABADILIKO!!!
 
Mhnnnnnn.....unaweza kuukaribia ukweli. Wasiwas wangu ni kuiba kura akisapotiwa na magamba wenzie....wanamwitaji sana ktk harakati zao za kuifisadi nchi....simwaamini tena huyu kijana.
 
Wwe ni juha, acha siasa za mahaba. Zito ni mtu na mwanasiasa makini. Anastahili sana kuwepo bungeni.Ni miongoni mwa watu ambao tuwaombea kwa Mungu washinde uchaguzi huu na kuwepo bungeni.

Matusi ya nini tukisema unatolewa mbwa na mzungu utabisha?
 
Namshauri Zitto abalance muda na nguvu zake katika kumnadi Mghirwa na muda wa kujijenga katika jimbo jipya maana akiacha gap kaliwa anaweza akakosa yeye na wagombea wake wote bora atulie jimboni ushindani ni mkubwa sana
 
Kwa hali halisi tuliyoiona Kigoma Jimboni kwa Zitto Kabwe kuna kila dalili huyu kiongozi akaukosa Ubunge mwaka huu.

Tumetembea sehemu mbalimbali na tukafanya mazungumzo na wananchi wengi kuna kila dalili Zitto akashindwa kurudi bungeni.Wananchi wengi wanashangaa Zitto kutokuwa na muda wa kufanya kazi jimboni na kujihusisha zaidi na mambo ya kitaifa huku akisahau wananchi waliomchagua.

Wengine wanadai ni kwanini awe msaliti wa chama kilichomjenga na wanaonyesha dhahiri wanaichukia CCM ambayo Mbunge huyo anashutumiwa kutumiwa ili kuharibu harakati za mabadiliko.

Kwa kweli Zitto ana kazi kubwa sana kwani hawa wana Kigoma wanaonekana wameamka na wanajitambua kwelikweli!

ulikuwa unafanya mazungumzo na akina nani?

I mean unacho cha kueleza kabla ya kuitwa majina??
 
Zitto ni Rais wa Kigoma, jimbo lolote Kigoma akigombea lazma anashinda.
 
Mbona sasa HV mkisikia tu jina la Dr slaa matumbo yanachemka? Nilichokuwa nataka kueleza ni kuwa hakuna Wa kumzuia zitto kwenda Bungeni,uliza Jana kilichomkuta kafulila baada ya kumponda zitto jukwaani,poleni sana nyumbu Dr slaa ni kinyago mlichokichonga nyie mwenyewe lkn Leo hii kinawatisha nyie mwenyewe

kafulila kaupata ubunge??
 
Zitto hawezi kurudi bungeni mimi nakataa hata kama wapambe wake wanasema ametenga milioni mia tano ya kuhakikisha anashinda . Ukweli ni kwamba hawezi kushinda zitto huo ndio ukweli

Mbona karudi sasa?
 
Zitto alikuwa na wachawi wengi!
 
Last edited by a moderator:
Zitto hawezi kurudi bungeni mimi nakataa hata kama wapambe wake wanasema ametenga milioni mia tano ya kuhakikisha anashinda . Ukweli ni kwamba hawezi kushinda zitto huo ndio ukweli

hahahahaha zitoooo huyooooo mjengoni tenaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom