ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Zitto Ziarani Nchini Kenya
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto yupo nchini Kenya kwa ziara ya ukaguzi wa miradi ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Ziara hii ni sehemu ya kazi za Mtandao wa Wabunge wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia (WB). Katika ziara hii kuna jumla ya wabunge 25 kutoka nchi mbalimbali duniani. Tanzania inawakilishwa na Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Sikonge ndugu Joseph Kakunda.
Katika ziara hiyo wabunge wanakagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na mashirika hayo na namna gani miradi hiyo inachochea maendeleo ya nchi husika. Benki ya Dunia Ina miradi ya thamani ya USD 2.3 bilioni (sawa na wastani wa Shilingi Trilioni 5) nchini Kenya. Wabunge watakutana na Asasi za kiraia na sekta binafsi ya Kenya. Upande wa Serikali watakutana na Waziri wa Fedha, Gavana wa Benki Kuu na tume ya mipango.
Asubuhi ya Leo ndugu Zitto alimtembelea bungeni Spika wa Bunge la Kenya, Mheshimiwa Justin Bedan Njoka Muturi. Pichani akiwa pamoja na Spika Muturi (katikati) pamoja na Mbunge wa Bunge la Uganda, mheshimiwa Nandala Nandala - Mafabi (kulia) ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Forum for Democratic Change (FDC) cha Uganda kinachoongozwa na ndugu Kizza Besigye. Mafabi naye ni mjumbe wa Mtandao wa Wabunge wa IMF na Benki ya Dunia (WB).
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto, ni mwanachama mwandamizi wa Mtandao wa Wabunge wa IMF na Benki ya Dunia (WB) kwa muda wa miaka 8 Sasa.
Imetolewa na Ofisi ya Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Februari 20, 2017