Zitto Kabwe yuko kimya ishu ya January Makamba

Zitto Kabwe yuko kimya ishu ya January Makamba

Hivi unategemea zitto aongee nn wakati wote ni wapiga dili?
Zito ni mwanasiasa kijana ambaye yuko safi anajitambua hakurupuki,
kwa mwanasiasa mwenye wered hawezi kukurupukia mambo ya mitandaoni yasiyo muhusu ikitokea vinginevyo unaweza kupata aibu ya mwaka.
 
Pamoja na nia njema hii assurance ya Zitto kwa Janauri utadhani obituary. Question:is Januari politically dead?
 
HALAFU HAWA WAZUNGU TUNAWASHADIDIA SANA, KWAO HUWEZIKUPATA HII PUBLICITY YA NAMNA HII, HUO UKOLONI ULIPO KWENYE VICHWA VYA BAADHI YA WATANZANIA AMBAO BOB MARLEY AMEUPIGIA KELELE KITAMBO (EMACNCIPATE YOURSELF FROM MENTAL SLAVERY) MZUNGU TUNAMPA KIKI, WEWE JITU JEUSI UKIWA KWAO HAKUNA HATA MTU ATBOTHER KUKUJADILI, KWELI TUNA MIKA MINGI YA UTUMWA KWENYE AKILI ZETU! MUNGU ATUEPUSHIE WENGINE MBALI!!
Aliyesababisha ajadiliwe ni yule aliyekubali kutengeneza urafiki wa mashaka na hawa wazungu.

nadhani hoja yako inawahusu pia viongozi wetu wa kisiasa ambao wanawathamini wazungu na wageni kuliko wazawa.
 
Mtoa maada umenichanganya kidogo ulivyo andika Zitti kabwe nikajua nimtu mwingine lakini naona wachangiaji sana andika Zitto sijui uunamaanisha hivyo
 
Tunayoyasikia kuhusiana na January ni kielelezo cha njia nyingine ya viongozi wa kisiasa wanavyopata hela za haramu kwa njia tofauti. leo hii mmoja tuhuma zake zimeanikwa,wapo wengi wanatembea vifua mbele kwakuwa siku zao za kuumbuka hazujafika.

Nimeingiwa na mashaka ninavyoshuhudia ukimya wa ZZK,mara zote yupo online na anakuwa wa kwanza kuzungumzia maswala ya maadili yanaposiginwa na viongozi. Najiuliza
kwanini amekuwa kimyaa kwenye hili sakata.ajitokeze tujue msimamo wake na chama chake.tunaamini yeye ni kijana wa kupigiwa mfano kwa maneno na vitendo.urafiki haupo kwenye ukweli naamini.
Umekosea hapo ulipo sema kuwa ni kijana wa kupigiwa mfano,mfano upi huo wa ufisadi kama makamba au uadilifu?
 
Kwani lazima yeye aseme.Si wengine waseme wakitaka au kama wana hoja?
Huyu mleta uzi naona yupo mbali na mitandao maana tayari zzk ameshatupia msg za kumtia moyo swahiba wake waanzilishi wa act
Cc MOTOCHINI
Cc mcubic
 
Umekosea hapo ulipo sema kuwa ni kijana wa kupigiwa mfano,mfano upi huo wa ufisadi kama makamba au uadilifu?
katika kujenga hoja kwa kile anachokiamini.Tz vigumu kupata mwanasiasa asiyekuwa fisadi.wanaumbuliwa ni wachache kuliko walio nyuma ya pazia
 
kwa political analyst kama wewe unapaswa kuelewa kuwa maswala kama hayo yanapotokea yanatoa nafasi kwa vyama vinavyochipukia kama ACT kuonyesha misimamo yao ili kukijenga zaidi chama chao kwa kujipambanua na wanachokiamini.nadhani umeshuhudia ZZK aki tweet kukiwa na hot news za kisiasa.ukizingatia kuwa vyama vyetu vya siasa vinaimarishwa zaidi na matukio kuliko sera.Hivyo naamini yeye anaumuhimu wa kuonyesha msimamo hususani ambapo rafiki yake kaguswa,ili wananchi tupime ukomavu wake wa kisiasa.
Kazi ya act ni kupambana na ukawa..........
 
katika kujenga hoja kwa kile anachokiamini.Tz vigumu kupata mwanasiasa asiyekuwa fisadi.wanaumbuliwa ni wachache kuliko walio nyuma ya pazia
Kujenga hoja zipi hasa?za kifisadi au kimaadili?
 
Wakati ambapo sakata la kumchafua January Makamba likifikia ukomo baada ya muazilishi wa swala hilo kukiri kwamba hakuwa ushahidi, Zitto Kabwe ametoa za "kibabe".

Kupitia instagram Zitto ameandika " Hasira za MWANAUME mmoja zinaweza kuzuia ukuaji wako kisiasa. Lakini kumbuka SIASA ni mbio ndefu na sio mbio za vijiti kama tulivyoelezwa.

Maneno ya Zitto yanaakisi vyema juhudi za kumchafua Makamba ambazo zimekwama.

Kwa vipi?:

1. Hasira za MWANAUME mmoja kuzuia ukuaji kisiasa : Kumekuwa na juhudi za wanasiasa waovu kuzuia ndoto za Wanasiasa vijana wenye uwezo mkubwa. Jambo hili liliwahi kumkumba Zitto kwamba na sasa limejaribiwa kwa Makamba.
Wanasiasa waovu ndani na nje ya CCM wanatamani kuona Makamba anaanguka : kwanza ili kuchukua nafasi ya Uwaziri na pili ili kulipa visasi dhidi ya kile wanachoamini Makamba aliwaadhibu wapinzani katika uchaguzi mkuu (Rejea jina la KUBWA LA MAADUI ).

Haikuhitaji kuwa mnajimu ili kufahamu kwamba Makamba ni hazina kubwa kwa Taifa, na ni kati ya nguzo muhimu za CCM na hivyo kumchafua sasa itawasaidia katika chaguzi zijazo.

Mange Kimambi alikuwa anatumika kuhakikisha anazuia ukuaji wa Makamba kisiasa. Ifahamike Mange hajaanza kumchafua Makamba sasa alishaanza lakini Jambo jema ni kwamba amekuwa akishindwa kufanikiwa na jaribio la sasa ameshindwa kwa aibu zaidi.

Zitto anamaliza kwa kusema.

maneno haya yanakuja wakati ambapo "kamaradi" Makamba anapata ushindi dhidi jaribio la kumchafua. Mange Kimambi ameshatangaza kwamba hakuwa na ushahidi kwa jambo lake, hivyo amekaa pembeni.
Muitaliano waliyedai ametapeliwa na Makamba , amejitokeza na kuueleza ulimwengu kwamba Mange ni muongo. Amethibitisha kwamba January hakuwahi kufanya aina yoyote ya utapeli.
Mange na mabosi wake wamebaki na aibu ya karne.

Asante Zitto kwa maneno hayo ya kishujaa.

Hongera kamaradi January Makamba kwa "ushindi wa dhahiri".
 
walewale. wote wanatumika na haya nnayoyasoma ni matumikizi....sijui lini tutapata wakweli.
 
Kama kweli kachafuliwa na waliomchafua wapo na wamekiri ni uchafu tu, Makamba awachukulie hatua za kisheria mambo yakaishie mahakamani, sio swala la kusameheana, tunajuaje kama wamepewa walivyokuwa wanadai? Muitaliano anadai hela zake, January alituambia Mange anataka urafiki na dadake baada ya urafiki wao wa awali kufa, bila kufikishana mbele tunajua makambas wamelipa hela muitaliano hana haja na makamba bali hela yake, lazima akae pembeni, January kacahfuka hata akioga hatakiwi kwenda mjini amechelewa gari imeondoka.
 
Tulishayaona mapema na kutahadharisha kuwa sio ccm wala Makamba mwenyewe watakua tayari kuchafuliwa na mgeni huyu na huyo Mange wake iwe kwa utashi wao au kwa kutumiwa. Nafikiri sasa hili jambo limefikia kikomo na wengine muendelee na shughuli zenu za kujitafutia riziki badala ya kuendelea kufurahia anguko la kiongozi tena katika hali ya uonevu. Zitto nawe ubarikiwe kwa kumtia nguvu waziri kijana na ni kweli kwenye siasa kuna upuuzi mwingi wa kuchafuana.Wengine walifika mbali wakimtaka January ajiuzulu eti kupisha uchunguzi.Ajabu! Wengine wakafikia hatua ya kumtaka raisi wa nchi amwajibishe waziri Ebo! raisi aache kazi za kikatiba alizoapa kushughulikia kwa maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla akashughulikie masuala ya mapenzi tena yasiyomhusu waziri wake bali dada yake waziri?
 
Back
Top Bottom