Zitto Kabwe: "Wekeni akiba ya maneno"

Zitto Kabwe: "Wekeni akiba ya maneno"

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,522
Mara kadhaa Zitto amenukuliwa na mitandao ya kijamii akiwashauri wanaomwita yeye msaliti waweke akiba ya maneno. Na miongoni mwa walomponda ni Mnyika na Slaa pamoja na BAVICHA wengi hapa JF.

Sasa kwa haya yanayoendelea CHADEMA, je Zitto bado ni msaliti? Na Mbowe ataitwaje? Kwanini UKAWA walimwaminisha Lipumba anaweza kuwa Rais ilhali nafasi hiyo ilikuwa ni ya CHADEMA?

Dr. Slaa hakuwa sehemu ya ujanja/hujuma hiyo? Big up Zitto Zuberi Kabwe uliona mbali!
 
Nakumbuka bwana ZZK na Prof Kitila Mkumbo wakati wanafukuzwa chadema walitukanwa matusi yote ya dunia hii na matusi hayo yaliongozwa na Tundu Lissu akifuatiwa na Mnyika.

Wengine kidooogo walikuwa na staha kwa sababu walijua kuna ukweli fulani Zito alikuwa anausimamia. Sitayasahau matusi yale na ndio mengine yalisababisha wengine tukajivuta chadema.

Naona sasa kibao kimegeuka! KIME TURN AROUND vibaya mno. Yaani sipati picha bwana Zito na group lake watasema nini katika ku revenge kwa mafisadi hawa. Tumedanganywa kiasi hiki jamani. Tumekumbatia mauchafu yote! Aibuuuu.... hata wewe Mbowe.

Angalia umewatia viongozi wenzako matatani na madoa ambayo hayatafutika.

Labda kwa ushauri tu. Wajipambanue mapema wasepe zao, bora tubaki wenyewe kwa wenyewe tupigane mijeledi mpaka kieleweke. Hatukubali ushenzi huu
 
Hamna vitu vya kufanya kuliko porojo? Tupo kwenye kikao mnazingua aiseeee. Tuna vitu vya maana vya kufanya
 
Inasikitisha kuona kuwa waliofanikisha movie ya kufukuzwa ZZK wamekuwa victims kweli malipo hapa hapa duniani na upinzani una safari ndefu sana kufikia peak ya mafanikio unless vitu vifuatavyo vitokee.

1. Kuwe na alliance ya ukweli kama zilizopata kutokea Kenya i.e ODM
2. Kuwe na wanasiasa watakao weka maslahi ya Taifa kwanza vyama na uroho wa madaraka baadae.
3. Miujiza

Sioni nafasi yoyote ya ushindi as long as tume ndio yenye kauli ya mwisho kutangaza mshindi kinyume na hapo ni ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi. Sheria hii ina lenga wale wanaochukulia matokeo ya sehemu wanazoongoza bila ku align na zile sehemu wanazoburuzwa.

Safari ni ndefu ila naamini ipo siku ki mzaha mzaha tutafika "autopilot" 😊
 
Nakumbuka bwana ZZK na Prof Kitila Mkumbo wakati wanafukuzwa chadema walitukanwa matusi yote ya dunia hii na matusi hayo yaliongozwa na Tundu Lissu akifuatiwa na Mnyika. Wengine kidooogo walikuwa na staha kwa sababu walijua kuna ukweli fulani Zito alikuwa anausimamia. Sitayasahau matusi yale na ndio mengine yalisababisha wengine tukajivuta chadema. Naona sasa kibao kimegeuka! KIME TURN AROUND vibaya mno. Yaani sipati picha bwana Zito na group lake watasema nini katika ku revenge kwa mafisadi hawa. Tumedanganywa kiasi hiki jamani. Tumekumbatia mauchafu yote! Aibuuuu.... hata wewe Mbowe.
Angalia umewatia viongozi wenzako matatani na madoa ambayo hayatafutika.
Labda kwa ushauri tu. Wajipambanue mapema wasepe zao, bora tubaki wenyewe kwa wenyewe tupigane mijeledi mpaka kieleweke. Hatukubali ushenzi huu

.
Ukitaka kujua kuwa chadema wamepiga hatua kutoka walipo kua kwenda mbele zaidi, tafuta comment za Kitilya Mkumbo juu ya ujio wa Lowasa ndani ya chadema/ukawa.
yaonekana wenye mtizamo kama wako ndio wanaohitaji msaada kwani mahitaji ya wakati yamewaacha nyuma.
.
 
Nimekuwa nikisema hapa kwa wanachama na wspenzi wa chadema Kuwait viongozi wenu wanaweza wasiwe sahihi hivyo wajifunze kufikiri wao wenyewe
 
Ni kweli kabisa kama alivyosema ZZK ni bora kuwa na akiba ya maneno, yeye mwenyewe ZZK alishasema siasa basi anaenda kufundisha lakini leo yuko wapi?

kwenye siasa kuna mtelemko wa kupata vijisent bila kuumiza kichwa sana...kufunddisha lazima ujiandae vizuri kwani pale unajenga akili za watu na mwisho wa siku vijesnti vinageuka kuwa vithumuni tena vya kuhesabiwa na makato juu...sasa hapo pima mwenyewe
 
Wewe pia neno hilo linakuhusu, weka akiba ya maneno", siku Zitto atakapotangaza kumuunga mkono mgombea wa UKAWA sijui utaficha wapi sura yako, safisheni bafu maana naona mshaanza pigana mabao ya mkono nyiinyi kwa nyinyi.
 
Nakumbuka bwana ZZK na Prof Kitila Mkumbo wakati wanafukuzwa chadema walitukanwa matusi yote ya dunia hii na matusi hayo yaliongozwa na Tundu Lissu akifuatiwa na Mnyika. Wengine kidooogo walikuwa na staha kwa sababu walijua kuna ukweli fulani Zito alikuwa anausimamia. Sitayasahau matusi yale na ndio mengine yalisababisha wengine tukajivuta chadema. Naona sasa kibao kimegeuka! KIME TURN AROUND vibaya mno. Yaani sipati picha bwana Zito na group lake watasema nini katika ku revenge kwa mafisadi hawa. Tumedanganywa kiasi hiki jamani. Tumekumbatia mauchafu yote! Aibuuuu.... hata wewe Mbowe.
Angalia umewatia viongozi wenzako matatani na madoa ambayo hayatafutika.
Labda kwa ushauri tu. Wajipambanue mapema wasepe zao, bora tubaki wenyewe kwa wenyewe tupigane mijeledi mpaka kieleweke. Hatukubali ushenzi huu
hujui kwamba EL ni mshikaji wa karibu sana wa ZZK? ... hutamsikia hata siku moja anamponda maana hata humu JF kuna uzi zzk alikuwa anamkaribisha EL ACT...
 
Hao mafisadi walipokuwa CCM hawakuonekana na hata hao waliopo akiwemo baba yenu na mwanaye na huyo mwalimu wa upe hamuuoni
 
Back
Top Bottom