Zitto Kabwe: "Wekeni akiba ya maneno"

Zitto Kabwe: "Wekeni akiba ya maneno"

😕Mara kadhaa Zitto amenukuliwa na mitandao ya kijamii akiwashauri wanaomwita yeye msaliti waweke akiba ya maneno. Na miongoni mwa walomponda ni Mnyika na Slaa pamoja na BAVICHA wengi hapa JF.

Sasa kwa haya yanayoendelea CHADEMA, je Zitto bado ni msaliti? Na Mbowe ataitwaje? Kwanini UKAWA walimwaminisha Lipumba anaweza kuwa Rais ilhali nafasi hiyo ilikuwa ni ya CHADEMA?

Dr. Slaa hakuwa sehemu ya ujanja/hujuma hiyo? Big up Zitto Zuberi Kabwe uliona mbali!
 
Nimekuwa nafuatilia watu wanavyo ripoti matukio mengi ya wagombea Urais wakiwa Eneo moja...hilohilo kila wakati wakifikiri Tanzania yote iko hivyo; naamini humu wapo waliobahatika kwenda shule kwa levo ya juu...wanaelewa maana ya kufanya resachi

Natahadharisha tena natahadharisha mchana kweupe.....Wekeni akiba ya maneno....

Wahenga walisema...usijaribu kina cha mto kwa miguu yote miwili.... Utazama!!!
 
Naona mparee anakapoint japo kaandika kifalsafa

Naona anatutahadharisha tusi ingie kwenye uchaguzi tukiwa na matokeo kwani yanaweza kubadilika.
Tuwe tayari kupokea Matokeo
 
That's true sasa kunawagombea wa nasema hawajui msamiati wa kushindwa wanajitambua kweli?
 
Hauhitaji kumwekea maneno msaliti, ni kumtimua na kusonga mbele. Tuko mbali mno kwa sasa adui amelegea mno, HAKUNA ALIYE JUU YA CHAMA. ULIPO TUPO.
 
Maneno hayajabadilka yanabaki kama yalivyo m1 ni msaliti no moja
 
Hamasa ya uchaguzi mwaka huu iko juu sana, hivyo lolote linaweza kutokea baada ya uchaguzi. Ni vizuri wadau wa uchaguzi (wananchi, vyama vya siasa, polisi, jeshi, serikali, tume ya uchaguzi, mahakama, vyombo vya habari na taasisi mbalimbali) kuweka akiba ya vitendo vyetu tunavyofanyiana na maneno tunayosema na kuandika kwenye kipindi hiki. Tuhakikishe kuwa kila mtu anafanya, kusema na kuandika kwa kuzingatia kilichoko kwenye katiba ya nchi, sheria za nchi, kanuni na taratibu za taaluma/kazi yako na kanuni na sheria za jumuiya za kimataifa pia ili ujiridhishe kuwa uko sawa kabla ya kutenda, kusema na kuandika hasa kwenye kipindi hiki cha uchaguzi.

Tukumbuke kuwa kuna watu ambao watawaruka na kuwakana watu wengine na kuwaachia mzigo wa lawama, tuhuma, kesi mahakamani, kifungo jela, na ushahidi pale mambo mabaya (mungu pishia mbali) yatakapojitokeza kwa sababu ya uchaguzi wao ndio walioagiza yafanyike. Lakini pia tunaweza kushindwa kutazamana usoni na kushirikiana baada ya uchaguzi kumalizika kwa salama kutokana na vitendo na maneno yetu wakati wa uchaguzi.

Kila mtu afanye, eseme na aandike kitu ambacho ataridhika kuajibika nacho bila kumlalamikia mtu mwingine kuwa ndiye aliyemsababishia hayo kwa kumtuma afanye, aseme au aandike jambo kwa niaba yake ambalo ndio chanzo cha shida itakayomkabili baada ya matokeo ya uchaguzi kutoka. Kila mtu atumie taaluma yake na kanuni zake katika kumuepusha na hukumu na mateso mbalimbali ya baada ya uchaguzi, maana uchaguzi huu unaweza kuishia kwa kupelekana mahakama za ndani na nje ya nchi, kuumizana, kununiana, kulipiziana visasi, n.k. Usije ukatumika vibaya na mwisho wa siku ukabeba lawama wewe mwenyewe na familia yako huku aliyekutuma akiwa yupo salama na familia yake nchini au nje ya nchi.

Tusiwe kama maroboti wanaotekeleza maagizo bila ya kutumia weledi na taaluma. Mfano, Mh. Mwakyembe kwenye ripoti yake ya Richmond alilazimika kuweka hadharani nusu tu ya ukweli kuhusu Richmond na kubakisha nusu nyingine ambayo hutujui ilikuwa na madhara gani kwa watu wengine zaidi ya akina Lowassa. Hii inaonyesha kuwa akina Lowassa waliachiwa zigo looote la richmond na watu ambao hatujui ni akina nani. Sakata la escrow liliwakumba watu waliowekewa pesa Mkombozi bank tu na kufichwa wale waliowekewa Stanbic bank. Hii ni kusema kuwa siku zote kuwa tayari kuwajibika kwa kile ulichokitekeleza wewe kwa mikono, mdomo au kalamu yako sio kile ulichotumwa au kuagizwa na mtu mwingine, unaweza kwenda jela mwenyewe na kumuacha aliyekutuma. Kila mtu anapaswa kuilinda katiba na sheria za nchi, kama mtu atakuagiza ufanye kitu kinachokinzana na katiba na sheria kataa kukitekeleza hata kama ni boss wako. mkumbushe kuhusu katiba na sheria zinavyosema kuhusu jambo analokutaka utekeleze.
 
ukweli ni kwamba tunachotaka ni habari sahihi. habari sahihi huwa haziangalii nani atanuna na nani atafurahi. na wala haziangalii ni za muhusika aliyezileta au za kutumwa. hizo zingine ulizoandika ni porojo tu.
 
ukweli ni kwamba tunachotaka ni habari sahihi. habari sahihi huwa haziangalii nani atanuna na nani atafurahi. na wala haziangalii ni za muhusika aliyezileta au za kutumwa. hizo zingine ulizoandika ni porojo tu.
Aliyekutuma atakuruka tu pale safari ya kwenda ICC itakapokamilika, atakwambia kuwa una akili timamu hata wewe ulipaswa kuwa unaifahamu katiba na sheria za nchi na kutenda kwa mujibu wa katiba na sheria hizo.
 
Ndugu zangu wana ukawa kosa si kufanya kosa ila kurudia kosa lilelile mtakua hamueleweki,
Tunawaona mitandaoni na majukwaani mshaanza kumponda nakumkejeli mzee Beni,
Hivi mnarudia kosa lilelile tena mlilolifanya kwa EL?
2020 sio mbali hamuezi jua huenda CCM wakamtosa mzee na nyinyi fastaa mkadaka, jipunguzieni mzigo ili mkianza mchakato muanze na kampeni moja kwa moja sio kwanza muanze kumsafisha then ndio mmwage sera.
 
Pumbavu na lofa ni yeye aliekimbia kwao na kukaa ukweni
 
Ndugu zangu wana ukawa kosa si kufanya kosa ila kurudia kosa lilelile mtakua hamueleweki,
Tunawaona mitandaoni na majukwaani mshaanza kumponda nakumkejeli mzee Beni,
Hivi mnarudia kosa lilelile tena mlilolifanya kwa EL?
2020 sio mbali hamuezi jua huenda CCM wakamtosa mzee na nyinyi fastaa mkadaka, jipunguzieni mzigo ili mkianza mchakato muanze na kampeni moja kwa moja sio kwanza muanze kumsafisha then ndio mmwage sera.
Hizi akili za mafuriko sijui kama zitakuekewa
 
Pumbavu na lofa ni yeye aliekimbia kwao na kukaa ukweni

Wekeni akiba ya maneno maana nyie mshavurugwa mtamponda mzee beni ila ikitokea amekatwa tu tayari mtageuza kibao
 
Back
Top Bottom