Zitto Kabwe: Wabunge hatujaamua kuwa serious

Spika ndio kikwazo cha uwajibikaji,mie nadhani anatakiwa aache sheria ichukue mkondo wake na si mambo ya busara za spika.,Ila yote yana mwisho
 
- Sisi wengine siku hizi tunali-appreciate bunge letu maana kama sasa mpaka Waziri Mkuu analazimishwa kuomba radhi, wakuu tumetoka mbali sana na hili bunge, I mean wanahitaji heshima japo kidogo!

Uncle Tom! tunajua ajenda yako humu
 
Asalamu alaykum.

Tunapojadili ubutu wa bunge letu sio lazima tulinganishe na bunge la nchi nyengine tunavyo vigezo hapa hapa kwatu katika bunge hili hili la dodoma ila tunaweza kusema mabunge yaliopita na hili ni tofauti, sasa utofauti upi ndio suala la kujadili labda tunaweza kusema bunge la mwaka fulani lilikuwa na changamoto hizi au bunge la mwaka fulani lilikuwa moto au lilikuwa baridi, baridi kidogo au baridi sana

kwa upande wangu naona bunge la mara hii limeongeza hamasa na wafuatiliaji wengi hasa wananchi wanaopenda kufuatilia suala zima la ufisadi.

kwenye wabunge waliotajwa huko juu sipingani na majina yaliowasilishwa ila kuna wengi hawajatajwa na ni miongoni mwa wachangiaji wazuri na waletaji hoja za msingi katika michango yao na baadhi yao walikuwemo tokea kipindi cha bunge lile lililopita ila bunge hili ndio wamepata wakuwapokea na kuwasaidia katika mapambano hayo.

bunge hili limesaidia kuwa na upinzani na nikisema upinzani sio kwa maana vyama vya upinzani bali hata katika chama tawala kuna upinzani yaani makundi ya wabunge kutofautiana katika hoja za msingi.

thanks
 
mkuu kana -ka -nsungu ni hivi bado huyo zitto hana haki ya kulalamika au kupiga kelele wakati ye yumo ndani habari kama hizi alitakiwa aongee mrema,,lipumba,,kama alikuwa anaona sheria zinapindishwa na anauhakika sheria ilishawahi kufwata mkondo wake juu yake why not her??then kwa nini asimwambie spika???kama ulimsikia namnukuu

mh spika kosa alilofanya ni kubwa kwa kuufuata sheria hata uwaziri angetakiwa avuliwe
"""""""""""""LAKINI NAOMBA TUSIFIKE UKO"""Why???mbona kwake walimfikia tena si uko
mpaka barabarani wakaendelea kudili nae !!!!ashukuru mungu wazee wa kigoma!!!

Kwanza hii kauli ya Zitto ya 'kama tungeamua kuwa serious...' ni matusi kwa wapiga kura waliowachagua na kuwatuma wabunge kama yeye wakawawakilishe huko bungeni. Ni matarajio ya wapiga kura kwamba mbunge 'akitumwa' bungeni kuwakilisha anakwenda huko kuwa 'serious' na si vinginevyo.
 
1.
Originally Posted by Field Marshall ES
- Sisi wengine siku hizi tunali-appreciate bunge letu maana kama sasa mpaka Waziri Mkuu analazimishwa kuomba radhi, wakuu tumetoka mbali sana na hili bunge, I mean wanahitaji heshima japo kidogo!

2.
Uncle Tom! tunajua ajenda yako humu

- Mods na Invisible, vipi huyu naye?
 
Back
Top Bottom