Viongozi wanaotumia ukoloni kama kisingizio cha umaskini wetu ni wa kuwaogopa kama ukoma. Wengi wao hutumia excuse hiyo kutowajibika kwa wananchi, huku wakijilimbikizia mali ya umma, na hali ikiwa mbaya, hukimbilia huko huko kwa hao wakoloni ambako wameshajinunulia majumba ya kifahari, na kujiwekea akiba za mamilioni ya dollar. Zitto has to be very careful na kauli yake hii, kwani ni rahisi sana kuzidi kubomoa kuliko kujenga.
Makombo ya mezani unaita reparation? Mbona wanafurahi wenyewe.
Viongozi kama Zitto wanaoendekeza kutafuta majibu rahisi kama ukoloni kwa maswali magumu kama "kwa nini sisi masikini?", au hata kujivika kilemba cha ukoka kwamba wanaweza kuongelea "reparation" inavyotakiwa tu.
Kuna proponents wa reparation wa kweli wanatokea kwenye Garveyite families huko wanajua reparation ni ninii wakimsikia anai debase na kuilinganisha na vimsaada anavyotoa Muingereza kwa hiyari yake wanaweza kutaka kumtundika mtini.
Utasemaje msaada unaotolewa baada ya watu kuridhika na bajeti zao, kubakisha crumbs on the table ngoja tuwatupie waafrika wana njaa hawa ndio ziwe reparation?
Lakini wa kuogopwa zaidi ya hawa wanaotaka kupanda mgongo wa common least denominator ya Watanzania karibu wote (kuchukia dhuluma tuliyofanyiwa wakati wa ukoloni, ambayo ni ya kweli) ni wale viongozi wanaoendeleza ukoloni wa mtu mweusi dhidi ya mtu mweusi, mtanzania dhidi ya mtanzania.
Kama utawala wa CCM vile.
Kwa sababu, hata tukisema tusihesabu mabaya yote, CCM wangetupa elimu tu, utawala wa CCM ungehakikisha mtoto wa Kigoma anapata elimu bora, labda tusingekuwa na kina Zitto leo.
Naamini kabisa kama wao waliweza sisi pia tunaweza kama tutawezeshwa kwa Policies ambazo zitawajenga kwanza wananchi wake na sio kutegemea wageni iwe kwa misaada au uwekezaji..Kuna matajiri wengi sana Dar nimewaona mimi enzi zetu wakiwa na vibanda (kiosk)vya kuuza urembo wa wanawake, kimbo na sabuni mitaani leo ni mabillionea, Kina Bakhresa walianza kama washona viatu leo mabillionea tena tajiri kuliko mashirika ya wazungu wengi tu..Kwa nini taifa liwe tegemezi kwa wazungu ikiwa tunaweza kabisa kuanza toka ndani..
sababu na misingi ni UNAFIKI wa Mwafrika!... tunauzana wenyewe kwa kupewa Unyapala.. viongozi wetu wote ni manyapala na ukielewa hilo sidhani kama utaona taabu kuelewa kwa nini sisi maskini.. How can we have Gold yetu ndani ya ardhi yetu waje watu wachimbe watuachie ruzuku ya 3% na tunadai hii inatosha tena kubwa sana ukilinganisha na....Hivi Amerika miaka ya 1700 walipogundua dhahabu waliwaita kina nani kwenda kuichimba?
yap na ndio maana huwa nawauliza watu hivi hawa wazungu walipogundua dhahabu na mafuta huko kwao walimwita nani kuja kuchimba? Si walichimba wenyewe, tena wakati huo hawana uwezo, nyenzo wala usafiri kama tulonao leo ktk masoko... Sasa kwa nini sisi tunataka Utajiri wa haraka sana kwa kufanya Umalaya ili tuwe kama wao ama tupewe ranks kulinganisha na wao?.
Hawa watu wote wanaopongeza Ukolonimambo leo hawana tofauti na malaya ambaye anafikiri akiuza mwili wake atatoka ktk umaskini na kupata utajiri haraka sana...Na hakuna kitu kibaya zaidi kama kufanya umalaya kwa shida, hapo ndipo utalishwa hata unga na kuwa kijiwe((addicted)..sio tu hutakuwa tajiri bali utafupisha hata maisha yako. Hizo HongKong, SouthAfrka na kadhalika walitumiwa tu kama malaya wa Cuba Club.. Yes ukiwaona mitaani wana magari ya nguvu na nyumba Masaki lakini nyuma ya pazia, wanawake hawa hulala na hata mbwa kuwafurahisha mabwana zao... Mtanisamehe kutumia lugha mbaya, lakini my message ni kwamba hatuna sababu ya kujifananisha na Hongkong wala South Afrika..We are who we are!..
Ni wakati watanzania tunatakiwa kuipenda nchi yetu, tufikirie sisi tunaweza vipi kuijenga nchi yetu maana haiwezekani misaada hii kutusaidia ikiwa inatulazimu kuwa malaya or to be Down low!..tukilaani ushoga kumbe!...
Money given in aid by the people of the United Kingdom to Tanzania is reparationfor colonial exploits states Tanzanian M.P. Zitto Kabwe.
The "country was built by colonial exploitation. Whether your born or not. We can as well survive without youraid, take it" he says.
Zitto Kabwe is a member of the Tanzanian Parliament (CHADEMA), representingKigoma North and is Shadow Finance Minister and Chairperson for Tanzania'sPublic Investments Committee. He is therefore a man that shapes governmentpolicy in Tanzania.
In times of unprecedented recession in the UK, I am sure that most would indeed like to stop aid to a country whose policy makers display these kind of sentiments when you scratch the surface!
Pole Sana Tanzania!
Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe
@Chomachomp your country was built by colonial exploitation. Whether your born or not. We can as well survive without your aid, take it.
Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe11 Jan11 Jan@Chomachompyour case is genuine totally but don't link to aid Tanzania gets from UK. Your country's aid is reparation for colonial exploits
--------
Zitto's response to this thread:
Evidence Mr. Kabwe?
Ndugu zangu. Nadhani ni hekima kujua Jambo kwa kina kabla ya kuanza kulitolea maneno na hukumu.
Ninaomba kueleza kifupi sana nini kilitokea huko twitter
yap na ndio maana huwa nawauliza watu hivi hawa wazungu walipogundua dhahabu na mafuta huko kwao walimwita nani kuja kuchimba? Si walichimba wenyewe, tena wakati huo hawana uwezo, nyenzo wala usafiri kama tulonao leo ktk masoko... Sasa kwa nini sisi tunataka Utajiri wa haraka sana kwa kufanya Umalaya ili tuwe kama wao ama tupewe ranks kulinganisha na wao?.
Hawa watu wote wanaopongeza Ukolonimambo leo hawana tofauti na malaya ambaye anafikiri akiuza mwili wake atatoka ktk umaskini na kupata utajiri haraka sana...Na hakuna kitu kibaya zaidi kama kufanya umalaya kwa shida, hapo ndipo utalishwa hata unga na kuwa kijiwe((addicted)..sio tu hutakuwa tajiri bali utafupisha hata maisha yako. Hizo HongKong, SouthAfrka na kadhalika walitumiwa tu kama malaya wa Cuba Club.. Yes ukiwaona mitaani wana magari ya nguvu na nyumba Masaki lakini nyuma ya pazia, wanawake hawa hulala na hata mbwa kuwafurahisha mabwana zao... Mtanisamehe kutumia lugha mbaya, lakini my message ni kwamba hatuna sababu ya kujifananisha na Hongkong wala South Afrika..We are who we are!..
Ni wakati watanzania tunatakiwa kuipenda nchi yetu, tufikirie sisi tunaweza vipi kuijenga nchi yetu maana haiwezekani misaada hii kutusaidia ikiwa inatulazimu kuwa malaya or to be Down low!..tukilaani ushoga kumbe!...
All said ukweli utabakia kwamba hii misaada wanayoitoa ni aibu yao wenyewe kama reparation...Can't fool me! huwezi nambia Muingereza ana huruma saaana kutusaidia sisi wakati anatumia - When we were rulers they were better off! Hizi ndio story nazisikia sana kuhusu Oman na Zanzibar ati Zanzibar ilikuwa imeendelea sana chini ya Sultan na wajinga wanaamini wanataka kuvunja muungano bora warudi kwa Sultan. Hii misaada yote anayoahidi ni aibu ya kukoloni watu ati huruma!.
Siwezi kumsemea Zitto lakini size yake kuwaambia They can stick that shit in their ashakum!...huwezi kumsaidia mtu na matusi juu ukitegemea sisi tutakaa kimya kama tulivyotukanwa na Israel..
Pamoja na ukweli kwamba UK was built in that way, we should not be fooled by politicians who use it as an excuse to justify their poor perfomance. Mkoloni aliondoka miaka 50 iliyopita, mbona hakuna kikubwa cha maana kilichofanyika? Kikubwa tulichofanya ni kuvuruga hata yale mazuri yaliyofanywa na wakoloni. Angalia shule alizoacha mkoloni uone hali yake ya sasa ikilinganishwa na mwaka 60, angalia hospitali, angalia barabara ovyo ovyo. Bado tunamlalamikia mwingereza?? Ukiangalia misaada iliyopata Tanzania toka kwa Uingereza, na nini kimefanyika na misaada hiyo unaweza kuonesha ni nini kimefanyika?
Si siri kuwa mkoloni alikuwa mwizi, lakini viongozi wetu wa sasa ni worse kuliko mkoloni, hawana haki ya kumlaumu mwingereza.
Quote from Zitto:
Mh. Zitto, nadhani ni hekima zaidi ukiwa na ufahamu kwamba wewe ni mmoja wa viongozi wetu muhimu sana wa kizazi hiki, katika nyakati hizi muhimu. Kwahiyo kila unapotoa tamko, watanzania wanakusikiliza, wote - wale wenye nia njema na nia mbaya na wewe. Ni muhimu ukalijua hilo ili kama ikibidi kukwepa kutoa kauli au misimamo yako pale pasipo na ulazima basi ufanye hivyo. Lakini endapo kuna umuhimu wa kutoa msimamo au kauli yako, kama hiyo mada, ambayo sasa tumeelewa baada ya ufafanuzi wako, jaribu kutafuta jukwaa ambalo utakuwa na nafasi ya kujieleza ili watu wakuelewe, na wasipinde mambo. Kwa mtazamo wangu, tweeter sio sehemu nzuri ya kufanikisha hilo.
Money given in aid by the people of the United Kingdom to Tanzania is reparationfor colonial exploits states Tanzanian M.P. Zitto Kabwe.
The "country was built by colonial exploitation. Whether your born or not. We can as well survive without youraid, take it he says.
Zitto Kabwe is a member of the Tanzanian Parliament (CHADEMA), representingKigoma North and is Shadow Finance Minister and Chairperson for TanzaniasPublic Investments Committee. He is therefore a man that shapes governmentpolicy in Tanzania.
In times of unprecedented recession in the UK, I am sure that most would indeed like to stop aid to a country whose policy makers display these kind of sentiments when you scratch the surface!
Pole Sana Tanzania!
Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe
@Chomachomp your country was built by colonial exploitation. Whether your born or not. We can as well survive without your aid, take it.
Zitto Zuberi Kabwe@zittokabwe11 Jan11 Jan@Chomachompyour case is genuine totally but don't link to aid Tanzania gets from UK. Your country's aid is reparation for colonial exploits
--------
Zitto's response to this thread:
Evidence Mr. Kabwe?
Unajuwa sisi tuna tatizo kubwa sana.Mkiuu, inasikitisha na inauma sana unapoona kwamba tulilonalo wa TZ ni kulalamika na kutoa visingizio tu. M
bona Malaysia, na nchi zingine za Asia nazo zilitawaliwa na kupata uhuru karibu wakati sawa kama sisi. Lakini angalia walipo sasa kimaendeleo! W
ao ni kazi tu, hakuna visingizio.
FJM
Tafadhali soma background ya Jambo hili kabla hujahukumu. Nimeeleza nini kilileteleza mjadala kati ya mimi na mwanamama wa kiingereza Sarah kiasi cha kumwambia wakitaka waondoe misaada Yao.
Ninaamini ukoloni uliofanyika Afrika ulikuwa na madhara zaidi kuliko Malaysia, Singapore na kwingine kokote. Ukoloni uliofanyika Afrika una madhara makubwa zaidi ya Kisaikolojia kuliko mahala pengine au jamii nyingine duniani.
Ukoloni uliofanyika Afrika mizizi yake bado haijakatwa. Bado mfumo wa uchumi wa dunia umelifanya bar a la Adrika kuwa Soko la malighafi. Bado wakoloni wana ushahiwishi mkubwa sana katika sera zetu mbalimbali.
Miaka 50 Baada ya Uhuru tusiendelee kusema matatizo yetu yanatokana na ukoloni. Hii ndio lugha wakoloni wanapenda kuisikia kutoka kwetu. Lugha inayowaondoa kwenye picha. Lugha inayowaonyesha wao wanatusaidia kwa usamaria mwema. Lugha hii sitaisema kamwe maana najua bado nchi hii imeshikwa na makucha ya ukoloni.
Leo hii Barrick kwa mfano hawakulipa kodi Tanzania mwaka 2010 lakini wamelipa kodi UK. Kuna Mgodi kule Uingereza? City of London is the largest tax haven. Tax dodging investors have camped within the ring fenced cityn of London exploiting developing countries billions of USD every year through tax avoidance.
Hivi vi misaada hivi ni vi reparation tu ambayo haipo kwenye makubaliano tu. Unaweza kuiita vingine. Lakini nchi Kama Uingereza wala isijidai au kujitapa na misaada Yao kwetu. Wanachukua zaidi kutoka kwetu kuliko tunavyopata katika misaada. Wakitaka wachukue misaada Yao. Tutabaki Kama Taifa
Narudi pale pale, ya kwamba hawa wazungu hata kama wangekuwa waafrika wenzangu kama wana mawazo sawa na huyu mama na kufiiria misaada ni mtego wa sisi kuendelea na Utumwa wa fikra tuwashabikie misaada tunayoipata kama ndio hatuna jinsi, believe me sintokubaliana nao hata siku moja kwa sababu ni akili ya UTUMWA sawa kabisa na akili ya MANYAPALA wanayoitukuza viongozi wetu kina Kikwete na wengineo...
Kama tunawafuata na kuwalalamikia matatizo yetu badala ya kuyatatua wenyewe kwanini wasitudharau?. Kama tunaweza kutumiwa kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa faida ya mabeberu kwanini wasitukebehi? Tumeshindwa kujiongoza hadi leo miaka hamsini bado tunategemea misaada kwanini wasituone tuna mapungufu? Kama wanatusaidia Pesa ya maendeleo yetu wenyewe tunaitafuna na kuitumia kuhongea kwanini wasituone tuna kasoro?
Namwambia mweshimiwa zitto zuberi kabwe Waingereza hawana haki hiyo ya kutulipa kutokana na ukoloni. Kama wao wasivyokuwa na haki ya kuwadai Warumi. Tusipojitayarisha na kujijenga tutatawaliwa mpaka sasa hadi milele. Lakini fursa ya kujitegemea ipo ni utayari wetu na jitihada zetu za pamoja na umoja wetu. Kuwaambia waingereza watulipe kwasababu walitutawala na kuchukua resources zetu wakati wenyewe tulikuwa bado hatujajitawala sidhani kama ni sahihi. Tulikuwa bado ni makabila madogo madogo ya wakulima na wafugaji, Tulikuwa hatuijui hata hiyo dhahabu maana yake nini na mpaka sasa tunashindwa kui process sababu ya Uvivu wa kufikiri wa viongozi wetu na utayari wao kulifanya taifa hili lijitegemee. Nasema sidhani labda niwasikilize wadau huenda mkawa na hoja nzito zaidi yangu.
Ni sawa lakini lazima ujue kwamba baada ya Uhuru kulikuwepo na makubaliano mengi tu ya kiutawala Memorundum of understanding. Na kama unakumbuka uasi wa wanajeshi wetu mwaka 1964 uingereza walipeleka majeshi yao Tz why?..Sasa ni vigumu sana kukataa ya Zitto ikiwa kuna kaukweli fulani maana itakuwa ajabu sana leo Iraq ikatae kwamba misaada wanayoipata haitokani na repatarions.. unaweza kutumia neno ama lugha yoyote ile unayotaka lakini ukweli upo pale pale kwamba marekani wanisaidia Iraq kwa sababu hizo na kuiweka kama koloni lao kinamna na WaMarekani raia wanatukana kila siku kwa nini wanatumia fedha zao nyingi kuisaidia Iraq nchi.Wakuu vyema sana.
Lakini habari mbaya ni kwamba aina ya viongozi tulio nao sasa hivi fikra zao zinawatuma kuona misaada kama ni haki yao (malipo ya ukoloni). Ndio maana mzee Kiranga akapinga suala la Zitto kutumia notion ya reparations kujustify hiyo misaada!!
Kusema kweli mimi nimepoteza imani kubwa na wanasiasa wa Tanzania, kuna kitu kinanambia kwamba tunachezewa akili zetu tu maana haiwezekani mambo yamekaa vibaya lakini hakuna mtu hata mmoja anajitokeza kupigania haki na kuinua maisha ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI..Something ain't right!..hasa napoona viongozi wanagombania madaraka, kuingia/kung'ang'ania Ikulu au Ubunge!..Nakumbuka siku zile Bush jr. alikvyokuja mara kwanza Tanzania, kuna kikundi cha waislamu walitaka kuandamana kuonyesha hisia zao juu ya Bush jr. na sera zake za "shock and awe". Basi, pale bungeni kuna mbunge mmoja (nimemsahau jina) alisimama na kuropoka kwamba anawashangaa hao waislamu kwa kuandamana kwao wakati Bush jr. anakuja na mapesa mengi ya misaada, kuandamana huko kutayafanya mataifa mengine yashindwe kutoa misaada kutokana na kutoridhika kwetu!! Sasa fikira kauli na fikra kama hizo zinatoka kwa kiongozi tena mtunga sheria!!