Zitto Kabwe: Serikali inachekesha sana!

Zitto Kabwe: Serikali inachekesha sana!

Lissu mropokaji wakati ndo anaefafanua
vifungu vya sheria bungeni?...

Yeye ndo anaweka sawa miswada
kanjanja yote ya serikali dhaifu?...

Mwanasheria wenu alishindwa hata
kuweka sawa vifungu vya sheria akasubiri tamko la mwisho la lissu...

Acha kukurupuka...

Wewe tifautisha kati ya kurekebisha vifungu na kujenga hoja,siku zote marekebisho yake wabunge siooo ila hoja inaletwa bungeni, inajadiliwa,watu wanawajibika Hiyo ndo kazi ya Zito kama hauamini kaombe hansad bungeni utayapata yote kuhusu hoja hasa za zito.
 
Hata hivyo huyu jamaa walishamshtukia siku nyingi ila tu mahakama ikamkingia kifua lakini makosa yake yalishaonekana hata alipokuwa uwanjani.
Nyinyi ndumila kutatu mmeliona leo miaka yoye mlikuwa wapi, kumbe ukiwa nje ya uwanja ndio unaona makosa
 
Msiwe na akili za kitoto, hapa issue sio zitto wala lisu, kila mmoja ni mbora kwa lake, tunachoongelea hapa ni hizo issues zitto alizozisema. Ni katika kutetea generation ijayo bila kujali wewe ni ukawa au act. Tusiwe washakibi wakipuuzi, tuwe na uzalendo na issues za msingi na tuungane kwa pamoja.
 
wewe mzalendo wa tz uongo wangu mimi ni upi? Au umekwisha kula viroba?Mimi ni mjumbe wa baraza kuu la chama taifa na nimjumbe wa mkutano mkuu wa chama taifa! Jaribu kuwa na siasa za mlengo wa kati kama kilivyo chama chetu!Penye ukweli uongo hujitenga! Je ni kwanini wabunge wetu wa ukawa wamesusia bunge? kama sababu hazifanani na alizotoa zzk!
 
Huwezi kutenganisha sera na sheria. Haya mambo ya gesi yameongelewa sana , alikuwa wapi watu wamepigwa sana na imeshaamuliwa gesi kwa taifa zima, Tunao kinaKafulila wanatosha
tunao we na nani?ZITO mtaalam wa mambo hayo na hakuanza leo,kuisemea gas alidai inaweza ikawa neema au laana,acha kukaririshwa na mume wako Lisu.
 
Muswada wa mapato ya mafuta na gesi imeandikwa haraka haraka na umeacha kabisa kushughulikia suala la mgawo wa mapato ya mrahaba kwa maeneo yenye utajiri huo.

Kwa miaka mingi tumekuwa tukipendekeza kuwa sehemu ya mapato, hasa mapato kutoka kwenye mirahaba ibaki kwenye wilaya zenye rasilimali.

Muswada huu umekwepa eneo hilo na litaleta mgogoro mkubwa kwenye nchi yetu. Hivi sasa wananchi wanaotoka kwenye maeneo yenye Dhahabu wanapata mgawo kutoka tozo za halmashauri.

Muswada huu upo kimya eneo hilo na hivyo kukosesha mikoa kama Mtwara chanzo muhimu cha mapato.

Muswada huu ukienda bungeni bila kupata maoni ya watu wa Kusini itakuwa sio haki. Ni vema kuondoa muswada huu bungeni ili kupata muda wa kutosha wa kupata maoni ya wananchi.

Wananchi wa Mtwara, chama cha ACT Wazalendo ndio chama pekee cha siasa hapa nchini ambacho kimeweka wazi sera zake kuhusu utajiri wa Maliasili ya nchi.
cc Mkandara huyu jamaa yako ana matatizo makubwa msome tena akili zake

Sera hizo zimetamkwa ndani ya Azimio la Tabora lililozinduliwa tarehe 13 Juni 2015 mjini Tabora.

Azimio lina lengo la kuhuisha Azimio la Arusha ili kujenga Tanzania ya watu walio sawa na wananchi kumiliki uchumi wao wenyewe.

Tumewaletea chama chenu, mkipokee na kukilea. Chama cha Wanyonge chenye misingi imara na shabaha ya kuwakomboa watanzania kiuchumi.

Asante sana
Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Atawakomboa watanzania kiuchumi wakati anataka wilaya husika zichukue sehemu ya mapato, does he even know how social democratic value are about in the first place and how policies are formulated under that perpsective; hawa vipanga wenu nao duh this guy is an economist apparently.
 
Huyo Tundu Lisu unayemkashifu ndio tishio la vibaraka kama nyie na hiyo serikali ya kijambazi na kifisadi mnayoikumbatia. Kosa lake kubwa ni kwamba ahongeki kama huyo Zitto anayefikiri anafahamu kila kitu.

wewe lisu n mtu wa vurugu tu na watu wa ivo ndo wamebaki cdm, pamoja na kwamba kutoka kwao bingen n la kupongezwa lkn hawajaweza kuongea n nn kinawatoa nje, inawezekana miswada n mizur na serkal ikaona n vema iharakishe maenemdeleo...
lkn ZZK ameweza kuainisha mapungufu ya hiyo miswaada hilo ndilo linalotakiwa
 
hamna asiejua ubora wa zito kwenye kujenga hoja ila ukigeugeu wake ndio ulipomfikisha alipo hata rais tulienae ni bingwa wa maneno matamu lkn ona alipoifikisha nchi huu c muda wa kujenga hoja tu bali ni kuisimamia ss kaonesha madhaifu ya muswada na umeshasainiwa yy anachukua hatua gani au anatushauri tufanye nn hilo ndio la muhimu
 
Hii posti ni ya 25/6/2015 kabla muswada haujaenda bungeni ,na ulienda baada ya wiki moja na wabunge wa ukawa wanabisha muda hautoshi ili hali zito keshausoma na kuuelewa toka tarehe hiyo.ukawa wanabishana na maneno na si hoja
 
ndoroooobo ww kaa kimya kama uelewi kitu watu wanakataa isije kwa hati ya dharura ww unajua mkataba wa kawaida watu wanapewa ck ngapi wausome ndio unajadiliwa mbona nyie team migebuka hamjielewi
 
cc Mkandara huyu jamaa yako ana matatizo makubwa msome tena akili zake

Atawakomboa watanzania kiuchumi wakati anataka wilaya husika zichukue sehemu ya mapato, does he even know how social democratic value are about in the first place and how policies are formulated under that perpsective; hawa vipanga wenu nao duh this guy is an economist apparently.
Mkuu wangu yaani kama ungeelewa wala usingeandika hili kwa sababu anachozungumza Zitto ndicho exactly happening ktk nchi za magharibi (Mabepari). Tembea kote utakuta mfumo bora wa ugawanaji keki ya Taifa na kila sehemu iliyojaliwa maliasili hizi imenufaika nazo na maendeleo zaidi yamejitokeza sehemu hizo. Nenda Texas inafaidika na mapato ya mafuta hata tunaona miji mipya kama Houston na Dallas zamani jangwa la wachunga ng'ombe - Cowboys... Alberta nchini Canada inafaidika na mapato ya mafuta nako ilikuwa wachungaji watupu. Mafuta yamebadilisha kabisa maisha ya sehemu hizo na yamevutia watu kutoka states zote. Kila state inafaidika na maliasili na rasimali zake ukiacha mbali taifa zima linafaidhika vipi na hawa ni Mabepari. Miji kama New York na Toronto imeendelea kuwa kitovu cha huduma (Services) wakifaidika na uwepo wasomi na wabunifu, hawalali milango wazi kwa kutegemea bahati za wenzao.

Tatizo lenu nyie mnapoambiwa Ujamaa mnafikiri ACT imekuja kurudisha nchi hii katika UJAMAA wa chama kimoja, badala ya kuitazama ACT kama chama cha kidemokrasia kinachofuata misingi ya Kijamaa kama NDP ya Canada au vyama vingine vya kisiasa vinavyosisitiza katika mgao bora wa keki ya Taifa. hii habari ya kutawaliwa kama anayoifanya Muingereza ambaye hana kitu kabisa lakini anabebwa na makoloni sisi wengine hatuikubali. Ebu nambie hiyo England yenu ya Malkia ina kitu gani? hawana kitu..lakini ndio wanaongoza duniani kwa unyonyaji kukusanya mapato kona zote za dunia kumridhisha Bi. Mkubwa..

Mkuu Mtwara itafaidika na gas na mafuta yake ina maana hata wewe utakimbilia Mtwara kuwepo kwa sheria hii hakumaanishi wewe ulioko Dar au Arusha huruhusiwi kuhamia Mtwara ukanufaike na maliasili hizo bali tunachotaka kuona ni Mtwara ikivutia uwekezaji zaidi. Ikiwa Texas ilokuwa Pori baada ya kuvumbuliwa mafuta sasa hivi ni miji inayoongoza katika maendeleo kwa nini isiwe Mtwara? Ni Ubepari gani mnaoufuata nyie CDM.

Na kwa uhalisia uliopo nchi nyingi zinavunja muungano, mikoa kujitenga na kuomba Uhuru ni kutokana na Utawala kutozingatia swala hili. Sisi kama binadamu hupigania mali, Inequality baina yetu ndio sababu kubwa ya kero zote zinazotokea nchini ama nje. Ukiweza kuweka mfumo bora wa ugawanaji pato la Taifa umeondoa husda, inda, chuki, unafiki na ndicho kitu pekee nchi zlizoendelea wameweza kujenga mfumo unaokubalika Kitaifa kama vile - NCHI haina MATABAKA isipokuwa watu wake. (yale yale ya kusema Tanzania haina dini isipokuwa watu wake)..

Habisa sehemu yenye maliasili kama dhahabu, mafuta na kadhalika ndio wawe maskini zaidi hii haina tofauti kabisa na Ukoloni ambao nchi kama yetu ulokuwa na Utajiri mkubwa mafao yake yalikuwa yakienda Ulaya tukiachwa maskini. Labda tofauti iliyopo ni mipaka na rangi za wanyonyaji na ndio maana nchi za kiafrika zimekuwa zikipigana vita kwa sababu hakuna mfumo mzuri wa kugawa keki ya Taifa. Wewe unadhani kwa nini Sudan kusini walijitenga? kwa Nini Congo na Nigeria kuna vita hadi kesho, kila nchi yenye vita ama kero za kutengana kiini chake ni ukosekanaji wa mfumo bora wa ugawaji keki ya Taifa.
 
Uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo wewe daima unajua mwenye uwezo wa mambo ya kisheria ni Tundu Lisu tu, nchi hii sijui inakwenda wapi yani vijana wamekuwa wavivu wa kufikiri kwelikweli.
 
Mkuu Mkandara

Mie siwezi kuongelea ya Texas sana kwa sababu USA kama taifa atulingani nao kwenye swala la muundo wa serikari wao wakiwa kama a federal constitution na sisi kama a unitary constitution; hivyo kuna complexity on 'social capital', how unit is fostered nationally and how polices are advocated nationally and within states.

Kwa hivyo napenda kuangalia mazingira ya Tanzania, kupitia katiba ya Tanzania na muundo wa jamii ya Tanzania, having said that sina tatizo na dhamira ya ACT or Zitto ispokuwa anajikanganya sana huyu mtu, uwezi kujenga 'social capital' even in egalitarian terms za ACT halafu ukataka mtu wa Mtwara na Mwanza wajione watanzania wamoja na wapo chini ya taifa moja lenye katiba moja na waheshimiane.

How exactly are you going to build a policy inayosema kiasi fulani kibaki sehemu husika, utawapa watu hela, utawawekea mazingira mazuri ya huduma za afya or which methods of income distribution utakayo ifanya huko mtwara ili wafaidi hilo pato la taifa? Zingatia umuhimu wa gesi na kipato chake iwapo utafanikisha hiyo agenda where are the social democracy values unayo hii promote in the first place nationally in relation to social capital and state duty to its people nationally.

Hizo sera sio za taifa kama la Tanzania ni hatari, azilingani na social democratic views nationally mfano how are you going to match the life of a person in Morogoro na Mtwara iwapo kila mtu asaidiwe na chake?

Si ndio unajiuliza does he even know what the concept of social democracy translate into national kwenye nationa politics; maana anacho hubiri na anachoamini tofauti na sera za kitaifa; unitary states do not discriminate all they do is foster regional advantages gesi inakuja wananchi wa sehemu hizo automatic wana fursa za kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazo compliment uzalishaji wa gesi na huduma zake.

Lakini kusema sehemu fulani lazima ipewe kiasi fulani cha hela kwa maendeleo yepi hayo and how exactly whilst maintaining national egalitarianism principles in developing the wider society.

Anyway aache kuongea hizi hadithi za makundi kwenye kuongelea rasimali za watu wote na tiafa zima, mara Zanzibar mara mikoa dude is non stop, wala afanyi kwa bahati mbaya ndiyoo anavyoamini mambo ya makundi makundi ndani ya jamii.

I just though I should highlight that sina makusudi ya kuingia kwenye mjadala wa kiuchumi; unao tayari kule kwengine kuhusu akili ya huyu jamaa.
 
Erick Please wala usiende huko sio muundo wa Constitution unaounda mfumo bora wa ugawaji keki ya taifa. Kuwa Federal au Unitary haina maana yoyote ikiwa nchi zote duniani hazina mfumo mmoja na zimeweza kujenga mfumo bora wa ugawaji keki ya Taifa. Ni nchi za Kiafrika tu ndiko tunaendeshwa na ulafi kama mifisi bado tunagombania hadi mifupa.

Labda nikuulize hivi kwa nini wewe una mshahara mzuri kuliko wafanyakazi wengine? na kwa nini watu wote tusiwe na mshahara mmoja,sawa ili kutokuwa na ubaguz unaozungumzia. Ipo mikoa leo watumishi wa umma kama walimu/madaktari hawajalipwa mishahara wakati mikoa mingine wamelipwa!. Kuna usawa gani hapa unaozungumzia au dicrimination unayozungumzia inatokana na Mikoa tu au?

Hivi mtu nikisema kuwa na kijakazi anayefanya kazi nzito za nyumbani kwa malipo hafifu ni UTUMWA! Inakuwa namtetea Kijakazi au nataka wenye vijakazi wapungukiwe pato lao? Sasa huyu Kijakazi achangamkie fursa zipi ikiwa humuwezeshi? Kesho akianza kukuibia unasema mwizi wakati kwake yeye hizi ndizo fursa zilizokuwepo!. Hivi nikisema Madaktari wetu wanastahili mshahara zaidi ina maana nafanya Ubaguzi ama tunatakiwa kutazama demand/supply na kazi yao kuwa kipimo cha kustahili..

Kifupi mkuu wangu nchi za magharibi walichotushinda sisi ni kuweza kuweka mfumo bora wa ugawaji keki ya Taifa na kila mahala panapokuwa na mfumo bora basi wananchi wake huwa na maisha bora zaidi na tumeona kote nhci za magharibi bila kujali wana muundo gani wa seirkali wamefanikiwa kugawama keki hii kwa kuweka fursa zaidi za uzalishaji sehemu zilizokuwa na maliasili. Ngoja nikuguse nyumbani...Jiulize hivi unafikiri kuwepo Uwanja wa Ndege Kilimanjaro haikusaidia zaidi uwekezaji katika Utalii na makuzi ya mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro!. was it a good Idea or bad? ikiwa mikoa mingine ilikuw ahaina hata kiwanja cha ndege ndogo..Kwa nini ilihitajika ku invest katika kiwanja kile. Je kama serikali isingejenga Uwanja ule unadhani hali ingekuwaje..

Sasa iweje Mtwara wawe na gas lakini bandari ya kusafirisha gas hiyo ijengwe Dar! makao makuu ya shirika la gas hiyo liwe Dar, Account zake ziwe Dar, mzunguko wa fedha zote za mauzo ya Gas ya Mtwara yanafanyika Dar badala ya Mtwara. Na kosa kubwa mnalofanya vyama vya siasa Ni kuzungumzia jarida (heading) pasipo kutazama ndani kuna nini. Kuna jamaa mmoja jana kanambia hili ya kwamba sisi hamwe hatuzungumzii Content wala Context siku zote tunabishania Process na huishia. Hii ni kweli kabisa na naanza kuelewa ama kuwasoma vizuri zaidi Wadanganyika.

Hizo banki account ndio zingewawezesha wananchi wa Mtwara kuchukua mikopo wakafungua biashara, au hata wewe kuhamia Mtwara. Government expenditure, upatikanaji wa mitaji, matumizi na gharama za uzalishaji na huduma zinavyoongezeka ndivyo maendeleo ya wananchi yanavyozidi kupanda.
 
Back
Top Bottom