Zitto Kabwe: Serikali inachekesha sana!

Zitto Kabwe: Serikali inachekesha sana!

ZZK katika ubora wake,eti bado kuna jamaa anaandika "Mnafiki@work",we unaipenda Tanzania au Chadema?
 
Umenifurahisha sana hapa, watu wanaumia moyoni tu

BAdo wapo kwenye hizi stage, wakivuka hizo utawaona tu hapa.

“First they ignore you, then they ridicule you, then they fight you, and then you win.”

Mahatma Gandhi



Wamevuka stage ya kwanza ya kum-ignore, ndio maana wanamfuatilia kila anapopita.

Saizi wapo kwenye stage ya pili,kumkashifu na kumzomea,

Kisha Zitto atafight back kwa kuendelea kusimama na hoja zenye nguvu,kushinda ubunge, kuendelea kuwa kinara wa hoja zenye maslahi ya taifa, kupambana sana na serikali bungeni.

Baada ya hapo hawa hawa, watasalimu amri na kukukubali kuwa alionewa, watampa ushindi.

Mkuu nimeipenda hii,Very very true...
 
Ni kichekesho na Serikali kuahidi kwa wazanzibari kuwa mafuta na gesi sio suala la Muungano halafu inatunga sheria za mafuta na gesi za kutumika Zanzibar. Miswada hii haikufikiriwa vizuri na hivyo iondolewe.

Muswada wa mafuta na gesi Asilia hauzingatii haki za wananchi. Imerundika mamlaka kwa Waziri wa Nishati na Madini na haki ya wananchi kushiriki na kutoa ruhusa utafutaji na uchimbaji haikuainishwa kwenye sheria. Chama cha ACT Wazalendo kinataka haki hii iwepo kwenye sheria.

Haki ya ' free prior informed consent ' ni suluhisho la migogoro kati ya wananchi na wawekezaji.

Muswada wa mapato ya mafuta na gesi imeandikwa haraka haraka na umeacha kabisa kushughulikia suala la mgawo wa mapato ya mrahaba kwa maeneo yenye utajiri huo.

Kwa miaka mingi tumekuwa tukipendekeza kuwa sehemu ya mapato, hasa mapato kutoka kwenye mirahaba ibaki kwenye wilaya zenye rasilimali.

Muswada huu umekwepa eneo hilo na litaleta mgogoro mkubwa kwenye nchi yetu. Hivi sasa wananchi wanaotoka kwenye maeneo yenye Dhahabu wanapata mgawo kutoka tozo za halmashauri.

Muswada huu upo kimya eneo hilo na hivyo kukosesha mikoa kama Mtwara chanzo muhimu cha mapato.

Muswada huu ukienda bungeni bila kupata maoni ya watu wa Kusini itakuwa sio haki. Ni vema kuondoa muswada huu bungeni ili kupata muda wa kutosha wa kupata maoni ya wananchi.

Wananchi wa Mtwara, chama cha ACT Wazalendo ndio chama pekee cha siasa hapa nchini ambacho kimeweka wazi sera zake kuhusu utajiri wa Maliasili ya nchi.

Sera hizo zimetamkwa ndani ya Azimio la Tabora lililozinduliwa tarehe 13 Juni 2015 mjini Tabora.

Azimio lina lengo la kuhuisha Azimio la Arusha ili kujenga Tanzania ya watu walio sawa na wananchi kumiliki uchumi wao wenyewe.

Tumewaletea chama chenu, mkipokee na kukilea. Chama cha Wanyonge chenye misingi imara na shabaha ya kuwakomboa watanzania kiuchumi.

Asante sana
Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo

Kwani huyu zitto ndio nani? Kwani serikali ni ya baba yake?
 
Tundu lisu hana uwezo wa kuongelea mambo ya kitaalam kama hayo! Tundu Lisu ni mropokwaji tu. Kwa hiyo utasubiri sana.
Huyo Tundu Lisu unayemkashifu ndio tishio la vibaraka kama nyie na hiyo serikali ya kijambazi na kifisadi mnayoikumbatia. Kosa lake kubwa ni kwamba ahongeki kama huyo Zitto anayefikiri anafahamu kila kitu.
 
Mimi nadhani ni vema Zito akaelewa kuwa uwezekano wa kurudia enzi zake za umaarufu wa kisiasa kamwe haziwezikurudi.asifikiri Mrema alipenda kuisha hivi ni kwamba jamii huangalia kwa makini mwenendo wa mwanasiasa tapeli.Nasikitika kukuambia nawe uko njia hiyo hiyo ya Mrema
Tatizo mnapenda kuangalia na kutaja wanayofanana tu bila kutaja wanayotofautiana,Tofauti yao ni kuwa ZZK is by far very capable,na hiyo ndio silaha yake,so unachokitegemea kimtokee utasubiri sana.
 
Nyinyi ndumila kutatu mmeliona leo miaka yoye mlikuwa wapi, kumbe ukiwa nje ya uwanja ndio unaona makosa
 
Haka kajamaa tumekafujuza kameanzisha chama chake bado kanatusumbua tu. Dawa ni kumzomea kwenye mikutano yake ili asisikilizwe maana ukikasikiliza tu, ubavicha unakutoka.
ha ha ha umenifurahisha sana bora mfia nchi kuliko chama
 
Dua la kuku! Kabla ya hayo kumfika nadhani ww na saccoss yenu tayari mtakuwa mshakuwa marehem
Mimi nadhani ni vema Zito akaelewa kuwa uwezekano wa kurudia enzi zake za umaarufu wa kisiasa kamwe haziwezikurudi.asifikiri Mrema alipenda kuisha hivi ni kwamba jamii huangalia kwa makini mwenendo wa mwanasiasa tapeli.Nasikitika kukuambia nawe uko njia hiyo hiyo ya Mrema
 
Acheni unafiki nynyi chadema leo kafulila mbona hammwiti msaliti na mlifukuza ktk chama chenu but zitto ndo mnafik.zitto ni mjenga hoja pekee ambae hana mpinzani.
 
Acheni unafiki nynyi chadema leo kafulila mbona hammwiti msaliti na mlifukuza ktk chama chenu but zitto ndo mnafik.zitto ni mjenga hoja pekee ambae hana mpinzani.

Amejenga hoja,ipi?!
Ya kutupa majina ya wahindi kutuambia ndio majina ya watu walioweka fedha ughaibuni?

Kweli wew kichupi
 
Tundu lisu hana uwezo wa kuongelea mambo ya kitaalam kama hayo! Tundu Lisu ni mropokwaji tu. Kwa hiyo utasubiri sana.

lisu ni mwanasheria na zito ni mchumi, ivo kwa maswala ya kisheria kama hayo ya miswaada,nk,tunamsubiria kamanda lisu. Anasemaje na kuhus ile skendo ya kutengua adhabu,cjui itakuaje.?
 
zitto alienda kutibiwa apollo india,alikuwa akitibiwa huku akistadi majina ya kihindi,juzi mwembeyanga akatupatia majina 97 ya kihindi...that's how zitto dharmendra is trying desperately to remain relevant!
 
Eti Zitto ni kiboko ya Wapinzani
 

Attachments

  • 1436209371469.jpg
    1436209371469.jpg
    41.5 KB · Views: 215
Zzk sikuwahi hata siku moja kukusifu humu jf lkn kwa hili tupo pamoja japo kuwa mimi ni kiongozi mkubwa tu ndani ya chadema!Penye ukweli wacha uongo ujitenge!
 
Back
Top Bottom