Zitto Kabwe: Serikali haijawasilisha taarifa ya CAG bungeni leo, imevunja katiba

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Amendika katika ukurasa wake wa facebook,kwamba serikali hutakiwa kuwasilisha taarifa ya CAG bungeni ndani ya siku saba tangu kuanzia kwa bunge la bajeti.

Anasema mpaka sasa taarifa hiyo haijawasilishwa hivyo kuvunja katiba ya jamhuri inayotaka iwasilishwe ndani ya Siku saba.

N:B

Serikali wanaogopa nini kama wapiga dili wameshaondoka? Kama hesabu safi weka bungeni watu wasome mambo mbalimbali yakiwemo ya kuyumba kwa bandari, bombardier na dreamliner,wafanyakazi hewa,wanafunzi hewa,hosteli za chuo kikuu,utangazaji wa tenda,nyumba za magereza,makusanyo yaliyobomoa dari,miradi ya maendeleo imekwamaje,na mengine yaliyoandaliwa kitaalam na wanamahesabu,sio wanasiasa
 
Hii serikali ya awamu ya tano ni ya kifisadi kuliko zote zilizotangulia. Ni waoga kuweka matendo yao peupe yaonwe kuliko zile za nyuma zilizokuwa zikiweka ripoti peupe na kuruhusu kamati za bunge zinazo ongozea na wapinzani zichambue na kutoa maoni yao yaliyo huru kabisa bungeni. Hii serikali ni ya wezi walijishtukia wenyewe.
MUNGU ANAWAONA!!
 
Naona awamu hii uvunjaji wa Katiba ndio kipambele,mara kaimu jaji mkuu,mara mhasibu mkuu na mhizinishaji wa pesa Pogba,mtu anavamia kituo cha radio na..mitutu,anakujakusifiwa wazi na kuambiwapiga kazi bwana.

Mitaani majambazi nayo yameshaanza kupita na mijegeje huku wakikusanya ngawira,naamini soon nao atawapongeza na kuwaambia wapige kazi kwani wanatumia benduki pia kama wale wa Nape,Roma na waliovamia Clouds!!

Awamu ya VI-WONDER,awamu ya kuomba iombewe,sijui ili kuongeza speed ya utekaji ama uvunjifi wa katiba!!
 
Back
Top Bottom