Zitto Kabwe: Nitampeleka Abdul Nondo Uhamiaji tarehe 20/4/2018 kwa mamlaka yangu kama Mbunge wa Kigoma Mjini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,023
144,381
Abdul Nondo Abdul Omar Mitumba, mjukuu wa Marehemu Mzee Omar Mitumba, mwasisi wa TANU na mpigania Uhuru wa Tanganyika leo anaitwa na maafisa Uhamiaji eti kuhojiwa uraia. Hao maofisa uhamiaji na aliyewatuma hawana credentials ambazo Babu yake Nondo, Mwenyekiti wa TSNP anazo. Hii Serikali inatutafuta ubaya.

Wazee wa Ujiji sasa mkae. Tumalize haya mambo ya kipuuzi

Pia soma > Uhamiaji wamhoji Abdul Nondo kuhusu uraia wake. Wamtaka apeleke cheti cha kuzaliwa chake, wazazi wake,mababu na mabibi

470AEE58-DB75-4B65-805B-C79953E6E221.jpeg

Hababri zaidi...
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema Aprili 20 ataongozana na Mwanafunzi Abdul Nondo kupeleka vyeti vya kuzaliwa katika ofisi za Idara ya Uhamiaji kama alivyotakiwa kuthibitisha uraia wake

Zitto amesema yeye kama Mbunge wa Kigoma ambapo ndipo nyumbani kwa mwanafunzi huyo, ataruhusu wapiga kura wake kumsindikiza ili kuhoji kama Wanakigoma sio Watanzania maana kila mara wamekuwa wakihojiwa juu ya uraia wao

Abdul Nondo alifika Idara ya Uhamiaji mapema leo kuitikia wito ambapo baada ya mahojiano akaamriwa awasilishe cheti chake cha kuzaliwa pamoja na vya wazazi wake ifikapo tarehe 20 mwezi huu

=====

“ Huyu Kijana (Abdul Nondo) Ni Mjukuu Wa Omar Athuman Kagobe, Babu yake Ni Veteran Wa Vita Kuu ya Dunia, na Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ndiye aliyeileta TANU Ujiji, Na ndio Kambarage Nyerere alipofikia Mara Mbili, akiwa na Bibi Titi na Sheikh Suleiman Taqadir, nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe, Ndio pia alipofikia Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy mara mbili na Sheikh Hassan bin Amir, na huyu kijana ubini kwake ndio kwa Mama yake Sherry Taki,

Aliyekuwa mjumbe Wa CC ya CCM, na mama huyu ndio alimuuliza Kambarage Nyerere kama atawanyang'anya Wahindi na Waarabu na Wazungu majumba na Mashamba, Bwana Kambarage Nyerere akasema hapana Utawala wa TANU hautofanya hivyo ingawa ulifanya hivyo, Na hili la Mwanafunzi huyu lilifanywa na Utawala wa Kambarage Nyerere chini ya Said Maswanya akiwa Waziri Wa Mambo ya Ndani, likapingwa sana na Watu Wa Ujiji Nyerere akarudia nyuma”

Halafu kuna watu wanajifanya Watanzania zaidi kuliko huyu Mtoto. Aliyewatuma kunyanyasa watu hana sifa hizi alizonazo Abdul. Hana

By

David kagoma
 
....serikali ya dhulma hii..waweke cheti cha mhutu cha kuzaliwa hadharani... Kama kweli wanataka haki....hawa wanamvumilia bashite mwenye vyeti feki...lakini wanawasumbua RAIA wema wasio na hatia...hao immigration wako makao makuu ya Polisi...wanafanya dhulma kukumbatia watu kama bashite...wanahangaika na mwanafunzi asiye na hatia...wamelaaniwa hawa..
 
Back
Top Bottom