Na Andrew Mushi
KATIKA kipindi cha muda mfupi wa miaka minne iliyopita, Zito Kabwe amefanya mambo makubwa sana katika nyanja ya siasa za Tanzania. Ni mambo watu wachache sana wanaweza kuyafanya.
Katika utafiti wa Redet wa mwaka 2006, Zitto alikuwa anamfuatia rais Kikwete kwa umaarufu kwa wanasiasa hapa Tanzania. Unapouwa na kijana mdogo kama Zitto, ambaye jina lake likitajwa, inabidi watu wakae kimya kwanza kusikia kuna jipya gani, ni vizuri kufanya tafakuri ya hii hazina tulio nayo.
Kwa wale wanaofahamu watu wenye umaarufu kama Zitto, tunawaita ‘taasisi' (institution). Kwa hapa Afrika, watu tunowahesabu ni taasisi ni kama Mwalimu Nyerere, Mandela, Kwame Nkurumah, na Raila Odinga kwa uchache. Kwa kawaida taasisi zina nafasi kubwa sana ya kutoa mwelekeo wa mambo.
Nia kubwa ya kumleta Zitto kama mada hapa, ni ili kuweza kujifunza mikakati na mbinu mbalimbali anayotumia kuweza kuleta mabadiliko hapa nchini mwetu. Kwa hiyo, Zitto tunamtumia kama shule, pia ni njia ya kuweka kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Hapa wanasiasa ngazi ya taifa hadi mtaa, wanaharakati, wakulima, wafanyakazi, washika dini na hata machinga wanaweza kujifunza mengi toka kwa Zitto na kuyaingiza katika mikakati yao ya kujikomboa.
Wana-Kigoma Kaskazini waliona hii hazina iliyo ndani ya Zitto mapema na ndio maana mwaka 2005, Zitto akiwa na umri wa miaka 29 tu, wakamchagua kuwa Mbunge wao. Zitto kazaliwa 1976. Hawakujali umri wake wala chama chake cha upinzani-Chadema. Mpaka leo hii, jimbo lake linachekelea kwa mafanikio mengi walioyapata. Lakini pia, Watanzania wamebaidi maana ile kasi ya madini yetu kuchimbwa na sisi kuambulia asilimia tatu tu imekutana na matuta, inasuasua.
Mkakati mkubwa sana wa Zitto ambao amekuwa akiutumia tangu ameingia bungeni ni wa kuwa na hoja moja na kuisimamia siku zote. Hoja yake imekuwa ni madini au kwa lugha ya ujumla rasilimali za taifa. Kila akiongea yeye anaongelea rasilimali za taifa. Anataka kila Mtanzania afaidike na hizi rasilimali na si makampuni machache ya Ulaya, Marekani, na Afrika Kusini pamoja na wachache wazawa. Imekuwa rahisi kujua Zitto anasimamia nini.
Ukitaka kujua Zitto anajua anachofanya, hoja ya mafisadi iliyoletwa na Willbroad Slaa, Mbunge mwenzake wa Chadema, hajawahi kuhangaika nayo sana. Maana anajua akihamia huko, je ya kwake nani ataisimamia.
Ili kuweza kusimamia hoja zake vizuri anafanya sana utafiti kujua undani wa hilo jambo. Agosti 2007 wakati wa bunge la bajeti, alisimamishwa kuhudhuria bunge kwa madai ya kuwa alidanganya Bunge kwa kusema Waziri wa Madini na Nishati wa wakati huo, Nazir Karamagi alisaini mkataba wa madini hotelini London, Uingereza kinyume na taratibu za nchi.
Miezi mitatu baada ya kusimamishwa, Rais Kikwete akamteua kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati aliyounda ya kupitia upya mikataba ya madini. Ingekuwa Zitto alidanganya Bunge, isingekuwa rahisi, kwa Rais kumteua katika hii kamati. Rais Kikwete alikuwa mbele hatua moja zaidi ya Bunge. Kilichomsaidia Zitto, alikuwa amefanya utafiti na alichosema ndio maana wabunge walioshauri asimamishwe, wakaoneka wao ndio hawajui kinachoendelea.
Zitto anaongea kile kinachowagusa wanachi wengi. Mfano, suala la madini na rasilimali nyingine linamkera kila mtu. Tofauti na wanasiasa wengine wanaongelea vitu ambavyo haviwagusi wananchi. Ni mara ngapi tumesikia, wabunge akina ‘naunga hoja mkono ndugu spika' wakishabikia kampuni za wawekezaji wa nje, wakati wananchi hawataki. Zitto yeye anapinga haya makampuni kwa nguvu zote.
Kuna wanasiasa waliibuka kuwa maarufu, ila pale walipoanza kuongea mambo ambayo wananchi hawataki kusikia walizimika kama moto wa kifuu .Mfano, Mtikila ameshikilia sana hoja ya Utanganyika, hiyo haina uhusiano wa moja kwa moja na wananchi. Mrema yeye kila akiongea ni yeye kuhujumiwa, hana wananchi wala hata chama chake.
Nguvu nyingine ya Zitto ni kusimamia anachokijua na kukiamini kwa nguvu zote. Halegezi msimamo.Mwaka 2007 alipodaiwa amedanganya bunge alisimamia msimamo wake, hakutereka, ingekuwa hana msimamo, angekimbilia kuomba msamaha.
Kitu kingine ambacho tunaweza kujifunza ni kuweka msimamo wetu wazi. Mwishoni mwa 2006 Zitto alisema akimaliza kipindi chake cha ubunge wa miaka mitano hapo 2010, hatagombea tena, Mwaka 2007 akarudia tena huo msimamo wake. Mwaka huu pia amesisitiza hilo tena. Niambie ni mwanasiasa gani anaweka msimamo wake wazi kama yeye. Tunaomjua Zitto, mwakani hatakuwa katika mbio za ubunge.
Nihitimishe makala hii kwa kukumbushia sifa tano kuu zinazomfanya Zitto ang'ae na kupaa kuliko wanasiasa wengi hapa Tanzania. Zitto ana ajenda moja tu, hashiki mambo mengi kwa wakati mmoja. Anafanya utafiti. Tatu Zitto ni mtu wa msimamo, nne anaongelea vitu vinavyogusa wananchi moja kwa moja. Mwisho, anaweka msimamo wake wazi.
amushi1@yahoo.com
CHANZO: KwanzaJamii.com