Asalaam aleykum Jf.
Kwanza kabisa naomba moderator huu uzi ukae hapa hapa umelenga hasa kutujenga zaidi kisiasa na kiroho.
Injili: Mathayo: 13:24-43
Yesu aliwatolea mfano, akisema, ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi magugu?
Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, la; msije mkakusanye magugu, myafunge matita matita mkayachome; Bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Ndugu zangu; nimetafakari huu mfano na mwenendo wa Zitto ndani ya chama cha chadema kumbe alikuwa ni Yale majani yaliyokuwa yanafanana na ngano baada ya kuzaa ndipo yakaonekana kumbe si ngano ni magugu!
Baada ya chadema kugundua kumbe Zitto na wafuasi wake yalikua magugu ndani ya chadema, mchakato wa kuyachoma moto ulianza mara moja. Moto umekuwa mkali sasa wanakimbia mmoja baada ya mwingine si mmesikia Kigoma, Temeke, Ubungo na huko kanda ya magharibi.
Ifahamike kwamba chadema walishajua haya magugu muda mrefu kwa kuwa viongozi ni wenye huruma waliwapa muda wa kujirekebisha ili warejee njia ya haki wao waliendelea kujimvinjari katika kukiumiza chama.
Rai yangu kwa chadema mnapo fanya chaguzi zenu ndani ya chama, epukeni mapema kupanda mbegu mkalala usingizi na kumpa nafasi adui, kupanda magugu katikati ya ngano itakuwa vigumu kutambua yupi ni chadema damu na msaliti.
Mwenye tafakari zaidi ya hii anakaribishwa kuchangia na kuboresha.
Naomba kuwasilisha.