Nchi yetu inakabiliwa na tatizo kubwa kweli, tatizo la wananchi wake kuugua ugonjwa wa uzushi. Uzushi ni ugonjwa unaolitafuna sasa taifa letu. Na bahati mbaya sana ni kwamba wanaoongoza kwa ugonjwa huu ni vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa, inasikitisha sana.
Na vijana wanaoongoza kwa ugonjwa huu ni wale wanaojiita wafuasi au waungaji mkono wa mbunge wa kigoma kaskazini-Zitto kabwe. Wao kila zuri linaloonekana Chadema eti limeletwa au kufanywa na zitto, kwa watu hawa zitto ndiyo chadema na chadema ni zitto, kwamba zitto akiondoka ni mwisho wa uhai wa chadema.
Sikiliza uzushi wao, eti mahusiano ya CDU/CSU na Chadema yamewezeshwa na zitto, na eti zitto aliwashawishi wajermani hao kufadhili chadema ikiwemo kuanzisha vyombo vya habari vya chama, na kwamba hela walizotoa ili kuanzisha vyombo hivyo mbowe aliziiba na kuanzisha gazeti lake la Tanzania Daima!
Kwa hakika huu si uzushi tu, bali ni ujinga na ushetani uliopindukia mipaka.Waingereza wanasema bila utafiti huna haki ya kuzungumza. Yaani huyu bwana anaandika upuuzi hapa alimradi tu amfurahishe huyo anayempenda, huu ni uzuzu, upopotenge wa akili, ni ujuha, ni ulimbukeni, ni ukuadi wa kijinga.
Nenda kawaulize waliolianzisha gazeti hilo, Deodatus Balile na Manyerere Jackton ambao kwa sasa ni wamiliki wa gazeti la jamhuri watakuambia nani alitoa hela za kuanzisha Tanzania Daima, hawa wanajua kila kitu, usizushe ujinga tu eti kwasababu hulipii chochote JF.
Halafu kuhusu mahusiano kati Chadema na CDU/CSU hujui chochote, unaropoka tu. Mahusiano hayo yameanzishwa na mbowe, baada ya kuchaguliwa mwenyekiti. kabla ya hapo Chadema kilikuwa karibu na SPD, chama cha kijamaa ambacho Zitto binafsi anakiunga mkono, maana kama hujui zitto ni mjamaa na alitangaza hilo hadharani mwaka 2009 wakati alipoomba kugombea uenyekiti wa chadema, kwahiyo zitto yupo chadema kama boya tu maana hakubaliani na itikadi ya chama ya mlengo wa kati, mlengo unaokubaliana na itikadi ya kibepari, CDU/CSU ni vyama vya kibepari.
Mahusiano na vyama vya kibepari yaliyoanzishwa na Mbowe hayakuishia kwa CDU/CSU pekee, bali yalikwenda mpaka kwa vyama vya Republican cha Marekani, Conservative cha Uingereza, na vyama vingine vya mlengo huo katika nchi za Denmark, Norway, Sweden, na kwingineko.
Halafu kuhusu fedha za Sabodo, huu nao ni uzushi wa kijinga, Sabodo amekuwa akisaidia chadema kwa mapenzi yake na siyo kwa ushawishi wa andiko la mradi, anasaidia harakati za siasa za chadema chini ya mbowe, kama hujui kitu nyamaza maana hiyo nayo ni busara.
Na kuhusu madai kuwa eti chadema inakubalika kanda ya ziwa kwasababu ya zitto huu nao ni ujuha mwingine, mimi ni msukuma kwetu kahama na chama hiki kimekuwa imara suklumaland na miko ya kagera na mara tangu kiloposajiliwa mwaka 1992, na mtu aliyekijenga sana mika ya karibuni ni mbowe hata kama hampendi kusikia jina lake, lakini hamwezi kuzuia ukweli usisemwe, wasukuma siyo washabiki wa mtu, ni washabiki wa hoja, kama ni kushabikia watu tungemshabikia John cheyo mzee wa mapesa, lakini hali siyo hivyo.
Na la mwisho sisi wasukuma siyo wabaguzi na hatuna harufu ya ubaguzi, hivyo msituletee ubaguzi wenu na chuki zenu dhidi ya mbowe na wachaga kwa ujumla. wasukuma ni watu wakarimu na wenye upendo kwa wote, na kama mnataka kutufundisha ubaguzi miaka ijayo tanzania itatawaliwa na wasukuma na mtalazimika kupigana vita ili kutuondoa madarakani kama ilivyofanyika rwanda na Burundi, maana hatutakubali kuruhusu vikabila vidogo vidogo na maskini kututawala, hata huyo zitto hana sifa za kututawala wasukuma, en delezeni ubaguzi mtajuta.
Mimi ni George Maziku, mwandishi wa habari na mchambuzi wa mambo ya siasa.