Zitto Kabwe mbunge wa kwanza kutumia iPad Bungeni

Zitto Kabwe wa CHADEMA ambaye anasoma bajeti mbadala ya upinzani sasa hivi Bungeni amekuwa Mbunge wa kwanza wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia teknolojia ya kisasa kufanya presentation kwenye Bunge kwa kutumia kifaa cha iPad kusoma hotuba yake.

Amemshinda Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, aliyetumia makaratasi na wabunge wengine wote. Nampa hongera Zitto kwa kwenda sambamba na taknolojia ya kisasa na kupunguza matumizi ya karatasi hivyo kuokoa miti isiendelee kukatwa.

Aisee uko makini kweli kwani nilikuwa nafuatilia hotuba yake ila siku- NOTICE mkuu, sijui ni umri wangu umeshindwa kuona details au vp . Nami nampongeza!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Kesho kutwa CCM wanenda kutangaza zabuni za kununua ipad mpaka kwa wakuu wa wilaya hata kama haiko kwenye bajeti ili tu wasionekane MIDUNDULIZA
 
Katika zama hizi za sayansi na teknologia, na hasa pale viongozi wetu wanaposisitiza matumizi ya teknohama, Zitto kafanya vizuri kuonyesha teknolojia inaweza kutumika vipi.

Pia kama alivyosema ndugu Sikonge, kutumia teknolijia kutalinda misitu yetu hivyo basi kuhifadhi vyanzo vya maji na ubora wa maji kwa ujumla (kutokana na mmomonyoko wa udongo) habitat na biodiversity; na pia kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.

If we are going to discuss trivial things lets ponder 'e-waste' too
 
Ndo mambo ya kizazi cha leo hayo. Je haujasikia ".......................... Mh. Zito Kabwe, umekiuka kanuni kaa chini ..............."
 
Usiombe ikakugomea wakati unaendelea na hotuba, wakati utaalamu wa kuitumia hadi usaidiwe. Budget ya Chadema imetulia sana siyo kama ya Mkulo. Hata kama ina mapungufu ni machache sana ukilinganisha ya Waziri wa fedha aliyowasilisha.
 
mnashangaa iPad ya zitto wakati record ilishawekwa na kocha wa kwanza wa taifa kutumia computer kufundishia kandanda - lol

Zitto Kabwe wa CHADEMA ambaye anasoma bajeti mbadala ya upinzani sasa hivi Bungeni amekuwa Mbunge wa kwanza wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia teknolojia ya kisasa kufanya presentation kwenye Bunge kwa kutumia kifaa cha iPad kusoma hotuba yake.

Amemshinda Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, aliyetumia makaratasi na wabunge wengine wote. Nampa hongera Zitto kwa kwenda sambamba na taknolojia ya kisasa na kupunguza matumizi ya karatasi hivyo kuokoa miti isiendelee kukatwa.
Nasikia John Komba yeye anatumia IPHONE
 
Mawenzi! Nawe uko kawa hawa jamaa wa magamba nini? Hilo neno km unataka kulijua! Tembelea ktk mtandao wa google bila shk utakuwa umeelimika ama utapata darasa zaidi.
 
iPad ndiyo nini jamani??

hiyo ndio i pad 23048530.jpg
 
Nasikia John Komba yeye anatumia IPHONE
teh teh huyu jamaa sindiye yule aliulizwa mbona uzungumzi mambo ya wananch wa jimbo lako,ili nawenyewe wasome habari za mbunge wao! Jamaa akadai wananch wake uwa awapati magazeti kwa muda muafaka wala mawasiliano ya tv na radio hayapatikani kwa urahsi ndio maana sioni umuhimu wa kuwazungumzia kwahiyo nibora niende nifanye mikutano ya ana kwa ana.mhhh iphone au ipod!
 
Nafikiri walinzi pale mlangoni hawakuiona, vinginevyo angeambiwa asiingie nayo kwa ajili ya usalama!
 
Back
Top Bottom