Zitto Kabwe, lini utaacha kuwadanganya wananchi?

Nimesoma hili gazeti la kishetani nimeligundua na mbinu zake za ki ibilisi!!
Hata kama wewe ni mwanachama wa ACT lakini upinzani wa kisiasa, demokrasia na utawala wa kisheria ndivyo vitu ninakutaka urudi shule.
Huyu kijana unayemshawishi afikiri kama wewe hutaweza!! huwezi kwa sababu amekuzidi kupita kiasi!! Hutamwelewa!! Hebu rudi ukaandikie kile kijarida cha uhuru.
By Godlisen Stephen, ACT-Pwani

Zitto Zuberi Kabwe ni miongoni mwa wanasiasa waliochipukia hapa nchini katika kipindi cha miaka takribani kumi iliyopita akipitia mlango wa vyama vya upinzani.
Kwa upande ule wa upinzani haina mashaka kuwa ameonekana kuwa ni mwanasiasa machachali na mleta uhai katika dhana ya siasa za upinzani.

Sio nia yangu kuangalia historia yake ya safari ya kisiasa wala historia ya amefikaje hapa alipofika leo katika maisha yake mengine yanayofunikwa na wadhifa wa Ubunge wa Kigoma Mjini.

Huyu ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge hili la 11 lilizinduliwa tarehe 11 Novemba, 2015.

Ninachojiuliza mimi haya anayoyafanya na kuyasema sasa mwanasiasa huyu kijana ambaye amejivunia sifa nyingi katika miaka takribani kumi iliyopita, ni yeye kweli? Ama naota?
Zitto ni Kiongozi wa chama changu cha ACT- Wazalendo, ndiye mbunge pekee katika chama hiki, tunajua alifikaje kwenye chama hiki kichanga akitokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Baadhi ya tuliokuwa tunamshabikia wakati wa mgogoro wake na viongozi waandamizi wa CHADEMA tulifanya vile kwa kuwa tulikuwa na imani na hoja alizokuwa akijenga na tulichukia mambo kadhaa yaliyofanywa ndani ya CHADEMA ambayo yalituvunja moyo juu ya matumaini ya kujenga upinzani wenye manufaa kwa nchi. Tulitamani siasa za Zitto ambazo zilituaminisha kuwa huyu ndiye mwanasiasa ambaye anavunja maswali na wasiwasi dhidi ya dhamira za wanasiasa wa upinzani Tanzania.

Niyaache hayo, baada ya kuanza kwa Bunge la 11 Zitto alikaririwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambayo kwa sasa haina mashaka kwamba ndio sehemu anayoitumia zaidi kuwasiliana na wananchi, alidai ameomba kuungano na kambi rasmi ya upinzani bungeni lakini hakukubaliwa.

Hata hivyo baadaye tukaona ushirika mkubwa wa Zitto Kabwe na wabunge kambi rasmi ya upinzani bungeni ambao wanaundwa na mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Nionavyo mimi hii ni karata nyingine nzuri kwa Zitto Kabwe ambaye hakuwa na ujanja mwingine isipokuwa kuungana na UKAWA ili awe na nguvu ya umoja.

Nilianza kumuelewa siku Rais Magufuli alipokwenda kuzindua Bunge la 11 pale nilipomuona kabaki bungeni kusikiliza hotuba ya uzinduzi tofauti na wabunge wa UKAWA ambao waliamua kutoka nje kwa madai ya kutomtambua Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein ambaye alihudhuria uzinduzi huo akiwa Rais Zanzibar anayeendelea kuwa madarakani baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi ya tarehe 25 Oktoba, 2015 kule Zanzibar kutokana na dosari kubwa zilizojitokeza. Kwa wakati ule nilimuona Zitto ninayemfahamu.

Sasa baada ya hapo nikaanza kumuona Zitto anayekuja na kutoka kama homa za vipindi, anaongea hoja ambazo sizielewi, anatetea mambo ambayo hayafanani nae, anashabikia hoja nyepesi nyepesi ambazo sio saizi yake, najiingiza katika migogoro isiyo na mashiko, anatoa takwimu za uongo na uchochezi, anataka kupingana na kupambana na vyombo vya dola bila sababu na analeta janja ya nyani kama vile bado yupo shule ya sekondari.

Hili alilolifanya mwisho wa wiki hii ndio limenifuruga kabisa. Najiuliza hivi Zitto ameshindwa kujua kuwa nchi hii ina vyombo vya dola na serikali inayotambua kuwa baada ya kupigwa marufuku kwa mikutano ya hadhara wapo watakaothubutu kujifanya wanaendesha makongamano?

Ameshindwa kutambua kuwa baada ya mkutano alioufanya Mwembeyanga na kuporomosha shutuma nyingi kwa serikali atakuwa ametibua nyuki waliokuwa wametulia? Hajui kuwa hawezi kupata tena fursa nyingine?

Hivi Zitto huyu ninayemfahamu mimi hajui ubora wa bajeti hii ya kwanza ya Rais Magufuli mpaka atake kupanga mbinu za kuibeza na kuwaaminisha wananchi kuwa ni bajeti mbovu kabisa?

Kwenye mitandao ya kijamii anakokutumia mara kwa mara na pia akichangia bungeni kuna siku nilimsikia akiponda uamuzi wa kutenga Shilingi Bilioni 5 za ununuzi wa ndege 3 za ATCL, nikajiuliza hivi Zitto ninayemfahamu mimi hajui umuhimu kununuliwa hizo ndege na kulifufua shirika la ndege la taifa?

Hivi Zitto huyu ninayemjua mimi ndio wa kuwadanyanganya watanzania kuhusu kuwekwa kwa tozo ya simu katika bajeti ya mwaka 2016/2017?

Anawadanganya watanzania kuwa mtu akituma shilingi 1,000/= atakatwa shilingi 280/= wakati anajua kuwa kinachokatwa ni asilimia 10 ya kodi ya mapato na asilimia 18 ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya faida ya makampuni ya simu inayotokana na kiwango cha miamala inayotozwa na kampuni za simu na benki.

Yapo mengi mno ambayo Zitto ananishangaza kwa sasa, na nimejikuta kila kukicha nasubiri kushangazwa na mwanasiasa niliyemuamini na kumpenda, sijui lini nitaishia kushangazwa na haya ya Zitto.

Hata hivyo naomba nimwambie Zitto kuwa akumbuke kuwa kwa kiwango chake, nilimtarajia aendelee kuyatazama mabadiliko yanayofanywa na serikali ya Rais Magufuli na kuyafafanua ama kushauri namna bora ya kuyatekeleza badala ya kuponda na kutaka kuwaaminisha wananchi kuwa serikali ya awamu ya tano ni mbaya.

Afanya kama ambavyo mara chache nimemsoma kwenye mitandao ya kijamii akimuunga mkono Rais Magufuli kwa hatua anazochukua na ambazo yeye mwenyewe Zitto Kabwe aliwahi kunukuliwa akisema Tanzania inastahili kiongozi wa aina ya Rais Magufuli.

Zitto Zuberi Kabwe akumbuke kuwa hii ni awamu ya tano, awamu ya “Hapa Kazi Tu” na watanzania wameamua kuungana na Rais wao kufanya kazi badala ya kuleta porojo na mambo ya kudhohofisha mabadiliko. Acheze muziki huo, asifanye tofauti.

Mwanasiasa huyu Mkongwe ajielekeze kujenga chama chake kwa kuunga mkono mambo ya maana ili wafuasi wake wamuamini. Vinginevyo akae kimya kama alivyokaa kimya mwanasiasa mwenzake kijana na Mbunge wa jimbo la Kibamba John Mnyika.

Asipofanya hivyo anahatarisha siasa yake, atapotea akiwa bado kijana, hatutamwamini tena na tusipomwamini sisi tusiokuwa wapiga kura wake wa Kigoma Kaskazini ajue kuwa hata wapiga kura wake hawatamuamini.

Ni muhimu atambue kuwa wapiga kura wa Kigoma Kaskazini walipata imani ya kumchagua kutoka kwenye chama kipya kabisa kwa sababu waliona watanzania waliowengi wanamuamini.

Nionavyo mimi haya ndio mambo muhimu kwake kuliko siasa ya vurugu anayotaka kuanzisha.

Mimi sifahamu Serikali hii na Rais wake wamejipangaje. Lakini kwa jinsi ninavyomsikia Rais Magufuli katika kauli zake anazozitoa katika matukio mbalimbali sina mashaka kuwa ni mtu asiyependa longolongo na asiyekuwa tayari kumvumia mtu ambaye kazi yake ni kuvuruga mambo mazuri.

Zitto Kabwe ndugu yangu ulizoea kufanya upinzani mkali tena wakati mwingine wa kichonganishi na baadaye watawala walikusikiliza na wakakuheshimu. Ndio maana hukuwahi kukong’otwa kama akina Profesa Lipumba, Godbless Lema, Mchungaji Msigwa na wengine wengi katika nchi hii.

Kwa staili unayokwenda nayo sasa nakuona kabisa unataka kuanza siasa za kukabiliana na polisi, unataka kupigwa, unataka kuturudishwa nyuma enzi za kuhamasisha watu wafuate unayoyasema ili wakumbane na polisi na wapigwe.

Unataka kujijenga juu ya damu za watu, unataka kuendeleza umaarufu kupitia mabomu na virungu vya vyombo vya dola.

Ndugu yangu Zitto nakusihi achana na hiyo staili, rudi kwenye staili yako ya siasa za kistaarabu, tutakuelewa tu kama ambavyo tumekuelewa huko tulikotoka na tukakuunga mkono.

Nionavyo mimi hiyo ndio njia ya maana zaidi ya hii unayokwenda nayo sasa.
Serikali hii naiona kabisa inavyokwenda haitakupa huo mwanya wa kuiyumbisha, utaumia bure.

Hujiulizi kelele za kutaka matangazo ya bunge yarushwe live jinsi zinavyopewa kisogo?

Hujiulizi malalamiko ya kupigwa marufuku mikutano ya siasa yalivyopigwa nyundo na hakuna anayebabaika?

Hujiulizi jinsi baadhi ya tuhuma za kutoka mataifa ya nje zinavyopotezewa na mambo

yanakwenda mbele? Hujiulizi ni kwa nini Rais Magufuli anasifiwa karibu dunia nzima kwa hatua anazochukua?

Hujiulizi hizo harakati zako wakizisikia watu wanaoielewa dhamira ya serikali hii watakuchukuliaje?
Serikali hii tunaiona inarekebisha na kuchukua hatua dhidi ya mambo mengi ambayo wewe mwenyewe ulikuwa unayapigia kelele.

Ufisadi, rushwa, matumizi mabaya ya ofisi, uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kuimarisha mashirika ya umma, kudhibiti matumizi ya fedha za umma, kukusanya mapato ipasavyo na kuwawajibisha wazembe.

Sasa ndugu yangu Zitto unapoipinga serikali hii tukuelewe unataka kubeba upande gani wa shilingi?

Mbona hatukuelewi kaka? Unatuchanganya na unatupoteza kabisa tuliokuwa tunakuamini na kukufuatilia.

Haya, mimi naishi hapo. Najua wapo wenzangu wengi ambao wanachukizwa na mwendo wako huu, unawakwaza sana.

Najua nao wataamka kukwambia ukweli.

Kwa heri.

C&P
 
Ukiona kiongozi anatumia nguvu nyingi kupambana na wakosoaji wake basi mtu huyo hafai kuwa kiongozi!
Kama ambavyo chadema na viongozi wake hawataki kukosolewa, mna double standard sana wafuas wa cdm, hv hao kina zitto na mbowe malaika? Hawakosei? Ccm tu ndo kila siku inakosea? Acheni hizo
 
Kama ni baharini anaitwa dome nchi kavu anapaswa kuitwa kinyonga ngozi yake inabadilika,ukawa waliligundua hilo!
 
Godlisen samahan napenda kujua hivi Zito ni mbunge wa Kigoma Kaskazini au Kigoma mjini au mm nimechanganya kwenye Maelezo yako.
 
Uzi unachosha huu,kuscroll peke yake imenichukua saa nzima,kukifikia kibox cha kucomment,duh..!!.

Zito ni mwanasiasa mzuri wala hana tatizo lolote na anajenga groundwork kwa ajili ya 2020 sasa
 
Anawadanganya watanzania kuwa mtu akituma shilingi 1,000/= atakatwa shilingi 280/= wakati anajua kuwa kinachokatwa ni asilimia 10 ya kodi ya mapato na asilimia 18 ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya faida ya makampuni ya simu inayotokana na kiwango cha miamala inayotozwa na kampuni za simu na benki.

Kwani hapa zito kawadanganya nini wananchi? Achana na Zito. Tunaomjua tunajua nini anasema na anachokitetea.
Hivi wewe unajua arithmetic calculations, achilia mbali mathematical calculations kuhusiana na dhana kadhaa za kodi na tozo
 
Zitto Zuberi Kabwe ni miongoni mwa wanasiasa waliochipukia hapa nchini katika kipindi cha miaka takribani kumi iliyopita akipitia mlango wa vyama vya upinzani.
Kwa upande ule wa upinzani haina mashaka kuwa ameonekana kuwa ni mwanasiasa machachali na mleta uhai katika dhana ya siasa za upinzani.

Sio nia yangu kuangalia historia yake ya safari ya kisiasa wala historia ya amefikaje hapa alipofika leo katika maisha yake mengine yanayofunikwa na wadhifa wa Ubunge wa Kigoma Mjini.

Huyu ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge hili la 11 lilizinduliwa tarehe 11 Novemba, 2015.

Ninachojiuliza mimi haya anayoyafanya na kuyasema sasa mwanasiasa huyu kijana ambaye amejivunia sifa nyingi katika miaka takribani kumi iliyopita, ni yeye kweli? Ama naota?
Zitto ni Kiongozi wa chama changu cha ACT- Wazalendo, ndiye mbunge pekee katika chama hiki, tunajua alifikaje kwenye chama hiki kichanga akitokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Baadhi ya tuliokuwa tunamshabikia wakati wa mgogoro wake na viongozi waandamizi wa CHADEMA tulifanya vile kwa kuwa tulikuwa na imani na hoja alizokuwa akijenga na tulichukia mambo kadhaa yaliyofanywa ndani ya CHADEMA ambayo yalituvunja moyo juu ya matumaini ya kujenga upinzani wenye manufaa kwa nchi. Tulitamani siasa za Zitto ambazo zilituaminisha kuwa huyu ndiye mwanasiasa ambaye anavunja maswali na wasiwasi dhidi ya dhamira za wanasiasa wa upinzani Tanzania.

Niyaache hayo, baada ya kuanza kwa Bunge la 11 Zitto alikaririwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambayo kwa sasa haina mashaka kwamba ndio sehemu anayoitumia zaidi kuwasiliana na wananchi, alidai ameomba kuungano na kambi rasmi ya upinzani bungeni lakini hakukubaliwa.

Hata hivyo baadaye tukaona ushirika mkubwa wa Zitto Kabwe na wabunge kambi rasmi ya upinzani bungeni ambao wanaundwa na mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Nionavyo mimi hii ni karata nyingine nzuri kwa Zitto Kabwe ambaye hakuwa na ujanja mwingine isipokuwa kuungana na UKAWA ili awe na nguvu ya umoja.

Nilianza kumuelewa siku Rais Magufuli alipokwenda kuzindua Bunge la 11 pale nilipomuona kabaki bungeni kusikiliza hotuba ya uzinduzi tofauti na wabunge wa UKAWA ambao waliamua kutoka nje kwa madai ya kutomtambua Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein ambaye alihudhuria uzinduzi huo akiwa Rais Zanzibar anayeendelea kuwa madarakani baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi ya tarehe 25 Oktoba, 2015 kule Zanzibar kutokana na dosari kubwa zilizojitokeza. Kwa wakati ule nilimuona Zitto ninayemfahamu.

Sasa baada ya hapo nikaanza kumuona Zitto anayekuja na kutoka kama homa za vipindi, anaongea hoja ambazo sizielewi, anatetea mambo ambayo hayafanani nae, anashabikia hoja nyepesi nyepesi ambazo sio saizi yake, najiingiza katika migogoro isiyo na mashiko, anatoa takwimu za uongo na uchochezi, anataka kupingana na kupambana na vyombo vya dola bila sababu na analeta janja ya nyani kama vile bado yupo shule ya sekondari.

Hili alilolifanya mwisho wa wiki hii ndio limenifuruga kabisa. Najiuliza hivi Zitto ameshindwa kujua kuwa nchi hii ina vyombo vya dola na serikali inayotambua kuwa baada ya kupigwa marufuku kwa mikutano ya hadhara wapo watakaothubutu kujifanya wanaendesha makongamano?

Ameshindwa kutambua kuwa baada ya mkutano alioufanya Mwembeyanga na kuporomosha shutuma nyingi kwa serikali atakuwa ametibua nyuki waliokuwa wametulia? Hajui kuwa hawezi kupata tena fursa nyingine?

Hivi Zitto huyu ninayemfahamu mimi hajui ubora wa bajeti hii ya kwanza ya Rais Magufuli mpaka atake kupanga mbinu za kuibeza na kuwaaminisha wananchi kuwa ni bajeti mbovu kabisa?

Kwenye mitandao ya kijamii anakokutumia mara kwa mara na pia akichangia bungeni kuna siku nilimsikia akiponda uamuzi wa kutenga Shilingi Bilioni 5 za ununuzi wa ndege 3 za ATCL, nikajiuliza hivi Zitto ninayemfahamu mimi hajui umuhimu kununuliwa hizo ndege na kulifufua shirika la ndege la taifa?

Hivi Zitto huyu ninayemjua mimi ndio wa kuwadanyanganya watanzania kuhusu kuwekwa kwa tozo ya simu katika bajeti ya mwaka 2016/2017?

Anawadanganya watanzania kuwa mtu akituma shilingi 1,000/= atakatwa shilingi 280/= wakati anajua kuwa kinachokatwa ni asilimia 10 ya kodi ya mapato na asilimia 18 ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya faida ya makampuni ya simu inayotokana na kiwango cha miamala inayotozwa na kampuni za simu na benki.

Yapo mengi mno ambayo Zitto ananishangaza kwa sasa, na nimejikuta kila kukicha nasubiri kushangazwa na mwanasiasa niliyemuamini na kumpenda, sijui lini nitaishia kushangazwa na haya ya Zitto.

Hata hivyo naomba nimwambie Zitto kuwa akumbuke kuwa kwa kiwango chake, nilimtarajia aendelee kuyatazama mabadiliko yanayofanywa na serikali ya Rais Magufuli na kuyafafanua ama kushauri namna bora ya kuyatekeleza badala ya kuponda na kutaka kuwaaminisha wananchi kuwa serikali ya awamu ya tano ni mbaya.

Afanya kama ambavyo mara chache nimemsoma kwenye mitandao ya kijamii akimuunga mkono Rais Magufuli kwa hatua anazochukua na ambazo yeye mwenyewe Zitto Kabwe aliwahi kunukuliwa akisema Tanzania inastahili kiongozi wa aina ya Rais Magufuli.

Zitto Zuberi Kabwe akumbuke kuwa hii ni awamu ya tano, awamu ya “Hapa Kazi Tu” na watanzania wameamua kuungana na Rais wao kufanya kazi badala ya kuleta porojo na mambo ya kudhohofisha mabadiliko. Acheze muziki huo, asifanye tofauti.

Mwanasiasa huyu Mkongwe ajielekeze kujenga chama chake kwa kuunga mkono mambo ya maana ili wafuasi wake wamuamini. Vinginevyo akae kimya kama alivyokaa kimya mwanasiasa mwenzake kijana na Mbunge wa jimbo la Kibamba John Mnyika.

Asipofanya hivyo anahatarisha siasa yake, atapotea akiwa bado kijana, hatutamwamini tena na tusipomwamini sisi tusiokuwa wapiga kura wake wa Kigoma Kaskazini ajue kuwa hata wapiga kura wake hawatamuamini.

Ni muhimu atambue kuwa wapiga kura wa Kigoma Kaskazini walipata imani ya kumchagua kutoka kwenye chama kipya kabisa kwa sababu waliona watanzania waliowengi wanamuamini.

Nionavyo mimi haya ndio mambo muhimu kwake kuliko siasa ya vurugu anayotaka kuanzisha.

Mimi sifahamu Serikali hii na Rais wake wamejipangaje. Lakini kwa jinsi ninavyomsikia Rais Magufuli katika kauli zake anazozitoa katika matukio mbalimbali sina mashaka kuwa ni mtu asiyependa longolongo na asiyekuwa tayari kumvumia mtu ambaye kazi yake ni kuvuruga mambo mazuri.

Zitto Kabwe ndugu yangu ulizoea kufanya upinzani mkali tena wakati mwingine wa kichonganishi na baadaye watawala walikusikiliza na wakakuheshimu. Ndio maana hukuwahi kukong’otwa kama akina Profesa Lipumba, Godbless Lema, Mchungaji Msigwa na wengine wengi katika nchi hii.

Kwa staili unayokwenda nayo sasa nakuona kabisa unataka kuanza siasa za kukabiliana na polisi, unataka kupigwa, unataka kuturudishwa nyuma enzi za kuhamasisha watu wafuate unayoyasema ili wakumbane na polisi na wapigwe.

Unataka kujijenga juu ya damu za watu, unataka kuendeleza umaarufu kupitia mabomu na virungu vya vyombo vya dola.

Ndugu yangu Zitto nakusihi achana na hiyo staili, rudi kwenye staili yako ya siasa za kistaarabu, tutakuelewa tu kama ambavyo tumekuelewa huko tulikotoka na tukakuunga mkono.

Nionavyo mimi hiyo ndio njia ya maana zaidi ya hii unayokwenda nayo sasa.
Serikali hii naiona kabisa inavyokwenda haitakupa huo mwanya wa kuiyumbisha, utaumia bure.

Hujiulizi kelele za kutaka matangazo ya bunge yarushwe live jinsi zinavyopewa kisogo?

Hujiulizi malalamiko ya kupigwa marufuku mikutano ya siasa yalivyopigwa nyundo na hakuna anayebabaika?

Hujiulizi jinsi baadhi ya tuhuma za kutoka mataifa ya nje zinavyopotezewa na mambo

yanakwenda mbele? Hujiulizi ni kwa nini Rais Magufuli anasifiwa karibu dunia nzima kwa hatua anazochukua?

Hujiulizi hizo harakati zako wakizisikia watu wanaoielewa dhamira ya serikali hii watakuchukuliaje?
Serikali hii tunaiona inarekebisha na kuchukua hatua dhidi ya mambo mengi ambayo wewe mwenyewe ulikuwa unayapigia kelele.

Ufisadi, rushwa, matumizi mabaya ya ofisi, uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kuimarisha mashirika ya umma, kudhibiti matumizi ya fedha za umma, kukusanya mapato ipasavyo na kuwawajibisha wazembe.

Sasa ndugu yangu Zitto unapoipinga serikali hii tukuelewe unataka kubeba upande gani wa shilingi?

Mbona hatukuelewi kaka? Unatuchanganya na unatupoteza kabisa tuliokuwa tunakuamini na kukufuatilia.

Haya, mimi naishi hapo. Najua wapo wenzangu wengi ambao wanachukizwa na mwendo wako huu, unawakwaza sana.

Najua nao wataamka kukwambia ukweli.

Kwa heri.

C&P
Sasa umeandika pumba gani hii uchafu?
 
Ingefaa zaidi itungwe sheria mbunge akitaka kufanya mkutano maandamano awe anaenda kufanyia jimboni kwake kwa wapiga kura sio kila kitu dar unatatua kero za wanadar es salaam jimboni kwako umezisahau
 
Back
Top Bottom