Zitto Kabwe kuburuzwa mahakamani?

Zitto Kabwe kuburuzwa mahakamani?

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,628
Reaction score
6,818
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameingia matatani, baada ya kutakiwa kukanusha tuhuma alizozitoa bungeni katika Mkutano wa Tisa wa Bunge, kwamba mfanyabiashara wa kigeni, Moto Mabanga, alipewa vitalu vya mafuta kinyume na taratibu.

Mfanyabiashara huyo amesema kuwa iwapo Zitto atashindwa kukanusha tuhuma hizo, atafikishwa mahakamani.

Barua iliyoandikwa kwenda kwa mbunge huyo iliyosainiwa na Mwanasheria wa Mabanga, Lawley Shein wa Kampuni ya Uwakili ya Lawley Shein Attorneys, ambayo Mwananchi Jumapili limeiona, inaeleza kuwa hoja binafsi aliyoitoa Zitto, haikuwa na ukweli wowote.

Barua hiyo ya tarehe 28 Novemba, 2012 ilisema kuwa hoja hiyo ya Zitto ni ya uongo, imemkashifu mteja wao na kumshushia hadhi yake binafsi na biashara zake.

“Katika kuthibitisha kuwa tuhuma zako siyo za kweli katika hoja uliyotoa, umemtaja mteja wetu kama raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mteja wetu ni raia wa Afrika Kusini, lakini, umeamua kumtaja kama raia wa Kongo bila kuangalia ukweli,” alisema Shein.

Katika barua hiyo, Shein pia amesema kuwa Zitto amemtuhumu mteja wake Mabanga kuwa aliwahonga baadhi ya vigogo serikalini na kuwapa rushwa wanasiasa katika mchakato wa kufanikisha upatikanaji wa vitalu hivyo.

“Tuhuma hizo siyo za kweli, mteja wetu alifuata taratibu zote kwa uwazi na mamlaka husika nchini na hakuwahi kutoa rushwa kwa mtu yeyote,” alisema mwanasheria huyo.

“Tuhuma hizi ni za uongo, zimemharibia jina mteja wetu na kumsababishia madhara. Kama hutazifuta kauli hizo, uongo huo utamsababishia mteja wetu madhara makubwa zaidi na tutalazimika kudai fidia,” Shein alionya kupitia barua hiyo.

Shein aliongeza kuwa pamoja na Zitto kuongea hoja hiyo akiwa bungeni hivyo kuwa na kinga ya kibunge, lakini kwa mazingira aliyotolea hoja hiyo alitumia vibaya kinga ya kibunge, anayopata mbunge yeyote anapotoa hoja akiwa bungeni.

Kupitia barua hiyo, Shein alimtaka Zitto kufuta kauli yake dhidi ya mteja wao na kwamba mteja wao ana haki zote za kushtaki dhidi ya hoja hiyo.

Zitto azungumza
Alipotakiwa kuzungumzia hoja hiyo na hatua atakazochukua, Zitto alisema kuwa amemwandikia barua Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, kumjulisha hatua hiyo ya kutaka kushtakiwa.

“Nimemwandikia Katibu wa Bunge kumjulisha kwamba nimeletewa kusudio la kushtakiwa, maana hili ni suala la Kinga ya Bunge,” alisema Zitto na kuongeza:

“Mbunge ana kinga kwa masuala aliyozungumza ndani ya Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 100 ya Katiba. Kwa hiyo Katibu (Dk Kashililah), atawajibu hao wanasheria.”


MY TAKE:
Mkuu Zitto, ina maana kweli uliteleza? Kwanini usimwombe radhi basi? Kama ni kweli, unaweza kutusaidia wananchi tukajua nini kinaendelea?
 
Tusubiri labda mheshimiwa Zitto ana ushahidi wa kutosha kuhusiana na jambo hili,vinginevyo itakuwa aibu ya mwaka kama alilopoka bila kuwa na ushahidi!
 
Huyu Mwanasheria anataka tu kula pesa za Mteja wake ina maana hajui Mbunge ana kinga kwa jambo lolote alilozungumza ndani ya Bunge? Kama mteja wake amekashifiwa Bungeni anatakiwa apeleke malalamiko yako Bungeni? (arejee malalamiko ya Reginald Mengi vs Wilson Masilingi kama sikosei)

TUMBIRI (PhD, HULL City - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Ninavyomjua Zitto hatakubali kushindwa hata kama kweli alifamya kosa, atabingirita na kuvingirika nao mpaka basi, Leka dutigite
 
Tusubiri labda mheshimiwa Zitto ana ushahidi wa kutosha kuhusiana na jambo hili,vinginevyo itakuwa aibu ya mwaka kama alilopoka bila kuwa na ushahidi!

Zitto anataka alindwe na bunge labda na yeye hana uhakika.
 
kama ni kweli zitto katoa kashfa za uongo kuna hatua za kuchukua na sio kwenda mahakamani, uyo mwanasheria ni kilaza na mteja wake ana pesa za kuchezea.
 
mahakamani kufanya nini? ujinga mwingine huo
 
Zito si anapenda ligi!hivi kufukuzwa kwake CDM kutafanyika lini?au wanamvumilia hadi muda waliouweka ufike?
 
Inawezekana zitto alisema uongo kwa nia ya kutafuta sifa maake wabunge wa chadema ni kawaida yao hivyo sheria uchukue mkono wake tumechoka kudanganywa.
 
-Huku ni kukurupuka sasa.Hivi hawajui kuna Kinga ya kisheria kwa jambo lisemwalo Bungeni?Wanasheria wengine nao!
 
Inawezekana zitto alisema uongo kwa nia ya kutafuta sifa maake wabunge wa chadema ni kawaida yao hivyo sheria uchukue mkono wake tumechoka kudanganywa.

Kwa kushabikia mambo tu hamjambo, eti sheria ichukue MKONO wa nani!!?? unazijua taratibu za bunge wewe? afu eti umechoka kudanganywa, kwani umedanganywa mara ngapi na raisi wako!?
 
Inawezekana zitto alisema uongo kwa nia ya kutafuta sifa maake wabunge wa chadema ni kawaida yao hivyo sheria uchukue mkono wake tumechoka kudanganywa.

unatumia makalio kufikiri?
hujaelewa hata mada unapost upuuzi tu
 
peleka lupango wakome uzushi, wamezoea sana kujitengenezea umaarufu kwa njia za kuzushia watu ulongo
 
Jamaa anataka kutafuna hela za uwakili kama kawa ,hakuna kesi hapo. Mbona mambo yapo wazi kuhusu kinga ya Mbunge
 
Unakumbuka wabunge wako kuhusu kamati ya nishati na madini wamepokea rushwa je ili kweli? Pia zitto amekuwa ni mbunge anaye leta hoja kwa mbwembwe nyingi mwisho wake huishia hewani kumbuka munyika kuhusu kumshitaki nape kuhusu pesa chafu za chadema alifikia wapi? Chadema bwana kwa uongo mko sawa!
 
Kwani alipataje hivyo hitalu, Hakuna watanzania wanaovihitaji?
 
Back
Top Bottom