Elections 2010 Zitto kabwe kawasaliti CHADEMA kigoma?

kwanini iwe ni Zitto tu kuulizwa hili swali? viongozi wengine wa Chadema waliwezesha majimbo mengi kuchukuliwa huko waliko?
 
Naona watu wanajaribu kuleta wa Lazima, yaani Kumgombanisha Zitto na Viongozi wenzake ili kuacha kutuwakilisha Bungeni

Walianza kuwapambanisha Zitto na Mbowe kwenye Uongozi wa Upinzani Bungeni lengo ni Kuonesha kuna Msuguano Mkubwa katika Nafasi hiyo kati ya Zitto na Mbowe, Sasa wanataka ionekane Zitto hakufanya Kampeni wakati Zitto alienda Musoma, Kibaha, kusini na Hata Sumbawanga Mjini.

Hizi ni hila za SHETANI ambazo CHADEMA wanabidi kuwa makini nazo
 
Blah Blah, sidhani kama zitajenga upinzani wa kweli. Kwanini tusiangalie tulipo anguka na kujifunza, kuliko kuangalia nani alisababisha au hakusababisha tuanguke? Tujifunze kwa makosa na sio kwa kulaumu. Zao la lawama ni kujitoa kwenye majukumu na kuwanyooshea watu vidole. Ufinyu wa uzito wa hoja husika ungeonyoshwa kwa uchangiaji mdogo na si kwa kauli za chuki na kubeza. Tutakuwa hatujengi ila tunabomoa.
NATOA HOJA
 
Ukweli utabaki pale pale ya kuwa Zitto Kabwe aliwasaliti wana Chadema wa Kigoma? Je ni lini Zitto alienda Muhambwe kupiga kampeni? Ni sababu ngapi alitoa kuhahirisha safari yake ya Muhambwe? Alivyoombwa na Dr. Slaa kurudi, je alirudi? Walivyoenda Muhambwe na Dr. Slaa je hata walisalimiana na kukaa na Mzee Ntagazwa kunenea jinsi ya kukomboa jimbo. Yeye alikuwa ameshawaanda vijana wake Mkosamali na Kafulila na ndio aliokuwa anawapigia debe...tunashukuru majimbo yameenda upinzani ila yeye ni chama gani? Au ana mpango gani na watu wa Kigoma? :nono:
 
Kitu cha kushangilia ni kuwa upinzani umetawala Kigoma na ccm imepunguza umaarufu! NCCR na Chadema wote ni wapinzani hivyo tushangilie hilo na kuachana na chokchoko zilizoanzishwa za kugombanisha wapinzani
 
Jamani najiuliza maswali sipati jibu.hivi umaarufu wa zitto kigoma,ameshindwa kuisaidia CHADEMA kunyakua majimbo zaidi?kwa nini imekuwa NCCR MAGEUZI kinara huko?ina maana Zitto hakufanya jitihada zozote??mnijuze wana JF!

Zitto Kabwe ni bora zaidi ya 10000 kama wewe anajua alifanyalo au kwa sababu sio Mchaga??
Mbowe ndio ana mchanganya mpiganaji
 
Hivi dogo si tulishuhudia kwenye TV Zitto alienda kumpiga tafu mgombea wa Chadema? sasa kama alikampenia mpaka kibaha nina hakika hata kigoma alifanya ila kwa Chadema kutochaguliwa sidhani kama ni kosa lake maana hakuwa mkurugenzi wa halmashauri za majimbo yaliyoenda NCCR.

Na kikubwa zaidi na faraja kwa sote majombo yameenda mikononi mwa...................................... na sio ......................................... TIA AKILI na siku nyingine usirudie kuleta utumbo wako wa kuku hapa JF.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom