Zitto Kabwe, John Malya na Uchaguzi wa EALA

Ndio siasa zake hizo hanaga cha washirika..Zitto ndio kawaida yake kung'ata na kupuliza hata chadema wanamjua,,ccm wanaendelea kutuamulia kila kitu inakera sana
 
Katika wanasiasa wanaotaka na wanaopenda kuona CCM ikitawala milele kwa kuwa wa nafaidika na mfumo ni Mbowe, Zitto na Prof Lipumba
 
hilo jina la mbowe hapo umeongeza chumvi
 
Hapo kila mtu anajali maslahi ya chama chake.. Zitto ana chama chake, sio mwanachadema tena!
 
Zitto anasmamia misingi na kuhusu hilo la EALA ametaka utaratibu kurudishwa. Halafu kitu kingine zitto haendi na upepo kama mnavotaka anachojali yy ni anachokiamini. Na huo ndio umadhubuti wa aiasa
 
hilo jina la mbowe hapo umeongeza chumvi
Kuna siku mtakuja kukubali kuwa Mwenyekiti wenu si mwanasisa ila anaendesha chama kama NGO na sifa ya mwanasisa ni kutoka kutawala tu lakini NGO ni kutaka kupata fedha tu kutoka kwa wafadhili
 
Zitto Kabwe, John Malya na Uchaguzi wa EALA

Na Ado Shaibu

Nimesoma tena na tena uchambuzi mfupi wa Ndugu John Malya, Mwanasheria mahiri wa CHADEMA ambaye kwenye andiko la uchambuzi husika anajitambulisha pia kuwa mmoja wa mawakili kwenye kesi ya Antony Kalisti Komu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani).

Ndugu Malya ameandika kumjibu ndugu Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini aliyemwandikia barua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Kwenye Mwongozo wake kwa umma, Spika ameweka mgawanyo wa viti vya wagombea kwa kuzingatia uwakilishi wa vyama Bungeni ambapo CCM imepewa viti 6, CHADEMA 2 na CUF 1.

Kwa maoni ya Ndugu Zitto mwongozo huu wa Spika:

* Ni kinyume na Tangazo la Msimamizi wa Uchaguzi (Katibu wa Bunge) kwenye Gazeti la Serikali Na. 11 la tarehe 17 Machi 2017 kuvialika “Vyama Vyenye Uwakilishi Bungeni” kuwasilisha majina ya wagombea wasiozidi watatu kwa kila kundi.

* Unakiuka Ibara ya 50(1) ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotaja waziwazi kuwa “Vyama Vyenye Uwakilishi Bungeni” ndivyo vyenye haki ya kugombea bila kujali idadi ya wabunge iliyonayo.

* Unakiuka Kanuni za Bunge Juu ya Jambo hili ambazo nazo zinatoa haki kwa vyama vya siasa vyenye uwakilishi kugombea.

Ndugu Malya, kwa kurejea kwenye hukumu mbili za kesi ya Komu (Kwenye Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani) amemjibu Ndugu Zitto kuwa:

* Mwongozo wa Spika kugawa idadi ya viti kwa vyama ni sahihi kwa sababu Divisheni zote mbili za Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ziliamua kuwa (Ninamnukuu) “Kwa kuzingatia complexity ya Tanzania (Being a Union of Tanganyika and Zanzibar and Zanzibar having no categorical representation) basi kuwe na UCHAGUZI wenye UWIANO wa idadi ya wabunge”.

* (Ninamnukuu) “Mwenye kupaswa kubeba mzigo wa makundi ya Zanzibar, Bara na Wanawake (Ukiachilia mbali kundi la vyama vya upinzani) ni chama chenye wabunge wengi (CCM).

Hoja yangu:

* Ni makosa kisheria kwa Ndugu Malya kufanya rejea kwa Kesi ya Antony Komu iliyoamuliwa na Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama ya Afrika Mashariki kwa sababu hukumu hiyo YOTE ilitenguliwa na Divisheni ya Rufani ya Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kwa sababu mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kuamua suala husika.

* Si sahihi kama asemavyo Ndugu Malya kuwa hukumu ya Divisheni ya Rufani ilijishughulisha na masuala ya mchakato wa upatikanaji wa Wabunge wa EALA hapa nchini aliyoyasema. Mahakama, kabla ya kujibidiisha na masuala hayo, ilijishughulisha kwanza kwa kirefu kuhusu kama Mahakama ya Awali ilikuwa na mamlaka (Jurisdiction) kuamua kesi ya Komu. Hitimisho la Divisheni ya Rufani lilikuwa kwamba Mahakama haikuwa na maamuzi kuamua suala ambalo madaraka yake yapo chini ya chombo mahsusi (Bunge) cha Nchi Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nimezisoma aya zote 73 za Hukumu ya Divisheni ya Rufani, sijakiona anachokisema Kaka yangu Wakili Msomi John Malya.

Hitimisho:

* Mchakato wa Uchaguzi wa Afrika Mashariki uzingatie Sheria na taratibu kwa kurejea Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kanuni za Bunge na Tangazo Rasmi la Katibu wa Bunge lililotolewa kwenye Gazeti la Serikali.

* Mchakato wa Uchaguzi uzingatie maslahi mapana ya nchi na si maslahi ya vyama pekee ikiwemo kuhakikisha ushiriki wa makundi mbalimbali ya kimaoni na makundi maalumu katika jamii kama inavyoelezwa na Ibara ya 50(1).

Ndugu Ado Shaibu
Dar es salaam
29 Machi 2017
Tatizo usiloliona ni kuwa Bunge limegawa nafasi sita kwa CCM kwa kuzingatia uwiano wa wabunge sasa kwa cdm na CUF kwanini wabaguliwe?

Hata kwa mtu wa kawaida inaonyesha dhahiri kuna ubaguzi. CCM inapendelewa na cdm na CUF wanaonewa.

Tatu, kwa kuvipa upendeleo vyama ambavyo wapigakura walivikataa ni dhahiri hatua hiyo ni kubeza demokrasia.

Kwa mahakama ya rufani ya EA Court of Justice kudai haina mamlaka juu ya ubishi wa tafsiri ya Treaty ni aibu kwao sidhani Kama hata walijikanganya hivyo
 
Zitto Kabwe, John Malya na Uchaguzi wa EALA

Na Ado Shaibu

Nimesoma tena na tena uchambuzi mfupi wa Ndugu John Malya, Mwanasheria mahiri wa CHADEMA ambaye kwenye andiko la uchambuzi husika anajitambulisha pia kuwa mmoja wa mawakili kwenye kesi ya Antony Kalisti Komu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani).

Ndugu Malya ameandika kumjibu ndugu Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini aliyemwandikia barua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Kwenye Mwongozo wake kwa umma, Spika ameweka mgawanyo wa viti vya wagombea kwa kuzingatia uwakilishi wa vyama Bungeni ambapo CCM imepewa viti 6, CHADEMA 2 na CUF 1.

Kwa maoni ya Ndugu Zitto mwongozo huu wa Spika:

* Ni kinyume na Tangazo la Msimamizi wa Uchaguzi (Katibu wa Bunge) kwenye Gazeti la Serikali Na. 11 la tarehe 17 Machi 2017 kuvialika “Vyama Vyenye Uwakilishi Bungeni” kuwasilisha majina ya wagombea wasiozidi watatu kwa kila kundi.

* Unakiuka Ibara ya 50(1) ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotaja waziwazi kuwa “Vyama Vyenye Uwakilishi Bungeni” ndivyo vyenye haki ya kugombea bila kujali idadi ya wabunge iliyonayo.

* Unakiuka Kanuni za Bunge Juu ya Jambo hili ambazo nazo zinatoa haki kwa vyama vya siasa vyenye uwakilishi kugombea.

Ndugu Malya, kwa kurejea kwenye hukumu mbili za kesi ya Komu (Kwenye Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani) amemjibu Ndugu Zitto kuwa:

* Mwongozo wa Spika kugawa idadi ya viti kwa vyama ni sahihi kwa sababu Divisheni zote mbili za Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ziliamua kuwa (Ninamnukuu) “Kwa kuzingatia complexity ya Tanzania (Being a Union of Tanganyika and Zanzibar and Zanzibar having no categorical representation) basi kuwe na UCHAGUZI wenye UWIANO wa idadi ya wabunge”.

* (Ninamnukuu) “Mwenye kupaswa kubeba mzigo wa makundi ya Zanzibar, Bara na Wanawake (Ukiachilia mbali kundi la vyama vya upinzani) ni chama chenye wabunge wengi (CCM).

Hoja yangu:

* Ni makosa kisheria kwa Ndugu Malya kufanya rejea kwa Kesi ya Antony Komu iliyoamuliwa na Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama ya Afrika Mashariki kwa sababu hukumu hiyo YOTE ilitenguliwa na Divisheni ya Rufani ya Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kwa sababu mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kuamua suala husika.

* Si sahihi kama asemavyo Ndugu Malya kuwa hukumu ya Divisheni ya Rufani ilijishughulisha na masuala ya mchakato wa upatikanaji wa Wabunge wa EALA hapa nchini aliyoyasema. Mahakama, kabla ya kujibidiisha na masuala hayo, ilijishughulisha kwanza kwa kirefu kuhusu kama Mahakama ya Awali ilikuwa na mamlaka (Jurisdiction) kuamua kesi ya Komu. Hitimisho la Divisheni ya Rufani lilikuwa kwamba Mahakama haikuwa na maamuzi kuamua suala ambalo madaraka yake yapo chini ya chombo mahsusi (Bunge) cha Nchi Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nimezisoma aya zote 73 za Hukumu ya Divisheni ya Rufani, sijakiona anachokisema Kaka yangu Wakili Msomi John Malya.

Hitimisho:

* Mchakato wa Uchaguzi wa Afrika Mashariki uzingatie Sheria na taratibu kwa kurejea Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kanuni za Bunge na Tangazo Rasmi la Katibu wa Bunge lililotolewa kwenye Gazeti la Serikali.

* Mchakato wa Uchaguzi uzingatie maslahi mapana ya nchi na si maslahi ya vyama pekee ikiwemo kuhakikisha ushiriki wa makundi mbalimbali ya kimaoni na makundi maalumu katika jamii kama inavyoelezwa na Ibara ya 50(1).

Ndugu Ado Shaibu
Dar es salaam
29 Machi 2017
 
wasomi wa kitanzania ni wadadisi wa mambo tatizo ni mgongano wa kimaslahi
 
Naona mmeanza tena kumuita Zito msaliti kwasababu tu amepeleka mgombea lakini ni haki yake yeye kufanya hivyo tatizo tunaweka uchama mbele bila kuangalia maslahi mapana ya Taifa kiukweli kati ya wagombea kutoka upande wa upinzani hakuna anaemfikia Prof.kitila na ndo hofu yenu....
 
Back
Top Bottom