ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Zitto Kabwe, John Malya na Uchaguzi wa EALA
Na Ado Shaibu
Nimesoma tena na tena uchambuzi mfupi wa Ndugu John Malya, Mwanasheria mahiri wa CHADEMA ambaye kwenye andiko la uchambuzi husika anajitambulisha pia kuwa mmoja wa mawakili kwenye kesi ya Antony Kalisti Komu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani).
Ndugu Malya ameandika kumjibu ndugu Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini aliyemwandikia barua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Kwenye Mwongozo wake kwa umma, Spika ameweka mgawanyo wa viti vya wagombea kwa kuzingatia uwakilishi wa vyama Bungeni ambapo CCM imepewa viti 6, CHADEMA 2 na CUF 1.
Kwa maoni ya Ndugu Zitto mwongozo huu wa Spika:
* Ni kinyume na Tangazo la Msimamizi wa Uchaguzi (Katibu wa Bunge) kwenye Gazeti la Serikali Na. 11 la tarehe 17 Machi 2017 kuvialika “Vyama Vyenye Uwakilishi Bungeni” kuwasilisha majina ya wagombea wasiozidi watatu kwa kila kundi.
* Unakiuka Ibara ya 50(1) ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotaja waziwazi kuwa “Vyama Vyenye Uwakilishi Bungeni” ndivyo vyenye haki ya kugombea bila kujali idadi ya wabunge iliyonayo.
* Unakiuka Kanuni za Bunge Juu ya Jambo hili ambazo nazo zinatoa haki kwa vyama vya siasa vyenye uwakilishi kugombea.
Ndugu Malya, kwa kurejea kwenye hukumu mbili za kesi ya Komu (Kwenye Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani) amemjibu Ndugu Zitto kuwa:
* Mwongozo wa Spika kugawa idadi ya viti kwa vyama ni sahihi kwa sababu Divisheni zote mbili za Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ziliamua kuwa (Ninamnukuu) “Kwa kuzingatia complexity ya Tanzania (Being a Union of Tanganyika and Zanzibar and Zanzibar having no categorical representation) basi kuwe na UCHAGUZI wenye UWIANO wa idadi ya wabunge”.
* (Ninamnukuu) “Mwenye kupaswa kubeba mzigo wa makundi ya Zanzibar, Bara na Wanawake (Ukiachilia mbali kundi la vyama vya upinzani) ni chama chenye wabunge wengi (CCM).
Hoja yangu:
* Ni makosa kisheria kwa Ndugu Malya kufanya rejea kwa Kesi ya Antony Komu iliyoamuliwa na Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama ya Afrika Mashariki kwa sababu hukumu hiyo YOTE ilitenguliwa na Divisheni ya Rufani ya Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kwa sababu mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kuamua suala husika.
* Si sahihi kama asemavyo Ndugu Malya kuwa hukumu ya Divisheni ya Rufani ilijishughulisha na masuala ya mchakato wa upatikanaji wa Wabunge wa EALA hapa nchini aliyoyasema. Mahakama, kabla ya kujibidiisha na masuala hayo, ilijishughulisha kwanza kwa kirefu kuhusu kama Mahakama ya Awali ilikuwa na mamlaka (Jurisdiction) kuamua kesi ya Komu. Hitimisho la Divisheni ya Rufani lilikuwa kwamba Mahakama haikuwa na maamuzi kuamua suala ambalo madaraka yake yapo chini ya chombo mahsusi (Bunge) cha Nchi Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nimezisoma aya zote 73 za Hukumu ya Divisheni ya Rufani, sijakiona anachokisema Kaka yangu Wakili Msomi John Malya.
Hitimisho:
* Mchakato wa Uchaguzi wa Afrika Mashariki uzingatie Sheria na taratibu kwa kurejea Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kanuni za Bunge na Tangazo Rasmi la Katibu wa Bunge lililotolewa kwenye Gazeti la Serikali.
* Mchakato wa Uchaguzi uzingatie maslahi mapana ya nchi na si maslahi ya vyama pekee ikiwemo kuhakikisha ushiriki wa makundi mbalimbali ya kimaoni na makundi maalumu katika jamii kama inavyoelezwa na Ibara ya 50(1).
Ndugu Ado Shaibu
Dar es salaam
29 Machi 2017