Zitto Kabwe, haya yote wewe hayakuhusu? Naona umeamua kunyamaza; hutaki kumshika mkono kipofu?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,470
11,640
Kwenye siasa Zitto anaendeshwa na mambo makuu mawili.

1. Pesa (Je, atafaidikaje kwa jambo fulani).

2. Position (Je, anaweza pata nafasi gani ya kumpatia kipato au deals )

3. Imani (aliyeko madarakani ni Dini gani?)

Hayo ndiyo humwendesha Zitto Kabwe. Kama Dini yako ni tofauti na yake lakini unampatia pesa hana shida. Atakuwa anakushtua shtua kidogo ili uone umuhimu wa kuendelea kumpa pesa.

Kama ni Dini moja na hujambana kwenye issues zake basi hawezi kukukosoa sababu wote mna imani moja. We ni wa kwetu. Si vizuri kukukosoa.

Kama anajua kuna nafasi unaweza mteua anakuwa makini asikukwaze..mpaka apate uhakika kabisa kuwa hatopata kitu hapo ndo anakuwa na uchungu sana.

1. Kuna suala la Mafuta kuongezwa kodi. Zitto amenyamaza. Anaona ni sawa tu yeye hajaguswa, yeye hajajua hatma yake.

2. Katiba mpya takwa la Watanzania kupitia tume ya Warioba. Zitto kimya. Halimhusu.

3. Kodi ya tozo ya miamala na kulipia line za simu. Zitto kimya sababu yeye alishatulizwa asionekane anamchafua Rais wa kwetu.

Tunamfahamu zitto ni mnafiki ,mjanja mjanja kisiasa kujipatika kipato. Hana mapenzi na Watanzania.
 
Unamchafua ndugu yetu we all know Kwa kiasi gan Zitto Kabwe ni critical thinker ko ulitaka aungane na chadema wapate nguvu.
 
Ila mnahitaji nguvu yake mpate nguvu ( Right from wrong) kukaa kimya kakosea ila mna sababu nje ya hili
Zitto ni muigizaji. Wpinzani wa kweli tuliwajua miaka ya Jiwe. Katika kumbukumbu zako, lini umeona Zitto akipata tabu katika siasa zake kama wenzake walivyopata. Just think about it.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Zitto kwanza ndie mkuu wa wilaya ya Handeni. Maana mke wake ndio mkuu wa wilaya so by default yeye pia ni mkuu wa wilaya.

Jambo la pili, Zitto hataki kumkosoa muislamu mvaa ushungi(sijui kama nitaeleweka). Maana Zitto alionyesha kupendezwa zaidi na mwanamke wa kiislamu kua rais kuliko kitu kingine chochote.

Zitto kwa sasa hatasema lolote.
 
Zitto ni muigizaji.... wapinzani wa kweli tuliwajua miaka ya Jiwe. Katika kumbukumbu zako, lini umeona Zitto akipata tabu katika siasa zake kama wenzake walivyopata. Just think about it.
Zitto aligombea ubunge swali linakuja je alipata huo ubunge kama ni kibaraka c angepewa hujuma kama walifanyiwa ni wote sio wanambowe peke yao
 
Back
Top Bottom