Zitto Kabwe: Hatuwezi Kushinda Vita Hii Kwa Kutishana Na Kuogopa Kushitakiwa Na Wawekezaji

yani hiyo comment ni ya kipopo kabisa,haeleweki yuko upande gani!bora lisu anasema anachokiamini bila woga wa lawama
 
Mtachonga Sana lakini ukweli ni kwamba JPM anachoangalia siyo chama bali watu wenye uzalendo na utayari wa kulitumikia taifa
Unamaanisha watu wote wanataka waonwe na JPM? Hivi maana ya uzalendo ni nini, maana inawezekana hili neno lina tafsiri nyingi?
 
Hivi walichokuchua na kilichopo katika sekta ya madini wingi wake ukoje kama kikichobaki ni wingi vipi tukiachie tu waendelee na kama ndivo hivyo walichochukua kingi waendelee tu kuchua hivyo hivyo kiudanganyifu!! Wasomi lindeni rasilimali hii
 
Nadhani wengi hamjaelewa hali na ukweli uliyopo. Ukweli ni kwamba wawekezaji wa madini wamekuwa wakituibia matrilioni kwa kutorosha dhahabu safi kupitia viwanja vya ndege walivyojenga karibu na migodi yao. Dhahabu iliyoko kwenye makinikia ni ndogo sana ukilinganisha na ile ambayo tayari imeibiwa. Mkataba serikali iliouingia na ACACIA unasema hata hiyo makinikia ni mali yao. Namna mchanga ulivyopimwa ndio shida. Shida sio kule kuukamata. Wakipeleka kesi mahakamani sasa hivi watatushinda tu. Hawakushirikishwa kwenye kuchukua sampuli wala hawakulazimishwa kuweka saini kuthibitisha kwamba waliona sampuli zikitolewa kwenye mchanga huo na wakaona kwamba kilichopimwa ni ile sampuli iliyochukuliwa na sio ingine. Mahakamani wakisema sisi tulifungua makontena yao tukaongeza mchanga wenye dhahabu ndani ili tutoe majibu ya uongo tuna cha kujitetea? Tukiulizwa kwa nini hatuwashirikisha kwenye vipimo wakati mchanga ni mali yao kisheria tutajiteteaje?
 
Zitti ni opportunist..anataka kiki za kilofa.
Botswana wanafaidi sana na rasilimali zao..jee wanachimba wenyewe? Jee wanakimbizana na wawekezaji ?
Jee wakitaka kubadilisha vifungu vya mkataba wanaifunga migodi..
Sote tuna penda sana tufaidi rasilimali zetu.
Sote tunajua ccm imetukosea watanzania.
Cha kwanza ni ccm kutuomba radhi..ikubali kuwa imetudanganya...kuwa wao na serikali zao zilisimamia vyema rasilimali zetu...
Pili njia nzuri sio kuingia vitani na wawekezaji.
kinachotakiwa ni kuwa na mazungzo nao kuona kama mikataba haina tija basi..kukaa na kuibadilisha kila kitu hufanywa kwa mazungumzo.
Kikwete aliikuta hii hali na Mkapa alikubali na kutetea kwa nguvu kupewa loyalty ya 3%...
Kikwete aliingia nao mazungumzo kuongeza hio % na tuka kubaliana ikaongezwa to 4%
Ni mazungumzo sio ubabe..haya anayo sapoti zitto ni sawa na yale alofanya Idd Amin alipo wafukuza Wahindi wote na kuchukua viwanda vyao vyote vya sukari chakula ujenzi na vingine. Kilichotokea ni history...
Hata hapa Mwalimu alituaminisha kuwa kuna mabepari wana tunyonya...hivyo tukashabikia na kumshanhiria..Mwalimu akaona amepata uungwaji mkono...akaingia kazini kutaifisha
Kuanzia Banks..Baroda
City bank
Standard chtrd bank
Bank of india na nyengine
Tukata ifisha na kuyaunganisha makampuni ya bima...tukafanya NIc
Mashamba
Viwanda kubao
Majumba yote kwenye miji ya Tanzania
Hata bakery ya mkate tukatifisha...
Miaka 20 baadae nchi ikabaki muflisi..tumefulia....athari zile bado zina tuandama..uchumi wa kuunga unga..elimu bomu .afya tume fail
siasa zile zimepitwa...zime fail na hazina nafasi kwa uchumi wa sasa....
elimu elimu pia ni tatizo kubwa ...upendeleo kufoji imetufikisha hapa..sote tunashuhudia vyeti feki ilivo tufikisha....yote haya matunda ya upendeleo....
 
nafikiri watu hatujasoma vizuri post ya Zitto mie nadhani kaponda ulaghai na uongo ambao ni kamati ya Mruma
 
Ukifuatilia comments/ posts za Zitto, hasa ile inayohusu msimamo wa kutokuogopa kushtakiwa na Accacia kwenye sakata la mchanga, utagundua kwamba Zitto huenda ameahidiwa kupewa Wizara ya Nishati na madini. Huu utakuwa mwendelezo wa Viongozi na wanachama wa ACT kuwa sehemu ya serikali ya CCM. Alianza Mkumbo, Mgwira na huenda akawa Zitto trotting!

Ni tetesi, mapovu hapana.
 
Zitto ni msaka tonge, m/kiti wake kapewa ukuu wa mkoa, mkuu wa chama anasubiri uwaziri wa nishati na madini, maana kabaki peke yake, na wasaliti wenzake wa mkoa ule.
 
Kwich kwich..... Sijaelewa anasimama wapi hapo....
kukaa katikati kama popo kumeua chama chake.

not so soon, chama kitabaki historia kama cha kina Mrema...

Hivi mbona hawa jamaa hawajifunzi?
Hawana cha kujifunza. Kazi waliyotumwa wamemaliza sasa ni malipo
 
Back
Top Bottom