Zitto Kabwe: Hatuwezi Kushinda Vita Hii Kwa Kutishana Na Kuogopa Kushitakiwa Na Wawekezaji

Zitto wakati mwingine anauvaa uzalendo sana. Kwa kwa kauli hii nakupongeza
Ingawa ni kigeugeu sana. Ni huyu huyu aliyesema kuwa Rais anapoteza zaidi ya billion 1.8 kwa kwa kuzuia mchanga. Lakini leo anaipongeza serikali
 
Team Lissu ni vigumu sana kuwaelewa wazalendo kama Zitto
Zito alikuwa ni mjumbe katika ile kamati iliyoundwa kupitia mikataba yote ya madini, wewe unayemuita mzalendo unaweza kutuambia ile kamati ilikuja na hoja gani juu ya kufanya haya tunayoyaona leo yasitokee? zaidi ninachokiona ndani ya kamati ile ndipo hasa Zito utajiri wake ulipatikana.
 
The simple way to describe Politician:

"The hungry politician is dangerous than a lion, whereas a greedy politician is a threat than hyena and a hypocrite politician changes his stance depending on his own interest the way a chameleon changes its colour according to its surroundings".
 
Hivi hawa wawekezaji walivamia tu migodi na kuanza kujichimbia madini au ni sisi tuliowakaribisha?
Takwimu zinaonyesha kuwa shughuli za uchimbaji mkubwa wa madini zimeongezeka kwa kuanzishwa migodi mikubwa sita mipya ya dhahabu kati ya mwaka 1997 na 2007.

MIKATABA YA MADINI

Kati ya mwaka 1994 na 2007, mikataba ya migodi mikubwa sita ya dhahabu ilisainiwa

  1. Bulyanhulu Agosti 5, 1994
  2. Golden Pride ulioko Nzega – Juni 25, 1997
  3. Geita Gold Mine uliopo Geita – Juni 24, 1999
  4. North Mara uliopo Tarime – Juni 24, 1999
  5. Tulawaka uliopo Biharamulo – Desemba 29, 2003
  6. Buzwagi uliopo Kahama – Februari 17, 2007
MAPENDEKEZO YA RIPOTI YA BOMANI 2008 KATIKA MIKATABA YA MADINI
  • Kuwapo mfumo imara wa sheria utakaofanya uwekezaji katika shughuli za madini ufanyike kufuatana na sheria za nchi zinazosimamia uwekezaji kwa ujumla badala ya mikataba maalumu na mwekezaji mmoja mmoja
  • Mikataba binafsi iruhusiwe pale tu ambapo uwekezaji ni wa kiwango cha dola za Marekani milioni 200 au zaidi
  • Mikataba itakayoingiwa ni lazima ipelekwe bungeni kwa taarifa; Sheria ya madini ifanyiwe marekebisho ili iweke vipengele vyote muhimu vinavyohusu uwekezaji katika sekta ya madini ili kuwa na sheria inayojitosheleza
  • Mikataba iwe wazi kwa wananchi na ipatikane katika ofisi za mikoa, wilaya na halmashauri ambako migodi ipo
  • Mikataba yote haifanani. Mikataba yote ifanane na kuwe na model agreement ambayo itakuwa sehemu ya sheria ya madini
  • Msamaha wa ushuru wa mafuta isipokuwa kwa mafuta yatakayotumika kwa uzalishaji wa umeme unaotumika migodini tu; Gavana aachiwe nafasi ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria
  • Asilimia 60 ya fedha inayotokana na mauzo ya madini irejeshwe nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani
Utozaji wa mrabaha; Mapendekezo:

Kamati inapendekeza kuwa tozo la mrabaha lizingatie ukokotoaji kwa kigezo cha gross value badala ya net back value.

Mgawanyo wa mapato yatokanayo na madini:

Kamati imebaini kuwa hakuna utaratibu wa kufanya mgawanyo maalumu kwa mapato yatokanayo na madini. Jambo hili linaleta wasiwasi na hisia tofauti kuhusu matumizi halisi ya mapato haya na manufaa yake kwa taifa na wananchi kwa ujumla.

Mapendekezo:
Katika mgawo wa mrabaha, 60% iende katika mfuko wa maendeleo ya madini kwa ajili ya miradi endelevu; 20% ya mrabaha iende kwenye mamlaka ya madini inayopendekezwa kuundwa katika taarifa hii; 10% iende wilaya yenye mgodi; 7% iende wilaya yenye mgodi; 7% iende kwenye halmashauri nyingine katika mkoa wenye mgodi; 3% iende kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi.

Biashara ya madini;

Mapendekezo:
Kwa kuwa hakuna utaratibu maalumu wa kuuza na kununua madini, Serikali iweke utaratibu wa biashara ya madini na kusimamia ili kuepusha utoroshwaji wa madini na kupoteza mapato yake; Kwa kuwa madini yaliyokatwa yana thamani kubwa kuliko yasiyokatwa, kuna umuhimu wa Serikali kuhamasisha na kuwezesha wafanyabiashara wafanye shughuli za ukataji wa madini; Serikali iwe na utaratibu wa kuandaa maonyesho ya vito na kuanzisha kituo cha minada ya vito; Kuwe na udhibiti mzuri wa madini ya vito yanayozalishwa nchini ili kuweza kuwavutia wawekezaji katika usanifu wa vito; Kuwe na kitengo maalumu katika mamlaka itakayoundwa kusimamia biashara ya madini ya vito na almasi.

UCHUNGUZI MCHANGA WA DHAHABU, WAIBUA RIPOTI YA JAJI BOMANI
 
Lissu nadhani ujumbe wa Zitto umeupata
mie nadhani lissu anatoa maoni yake, maamuzi yameshafanyika, lissu aonge ah asiongee bado action imeshafanyika, sioni kwa nini watu wana wasiwasi sana na comment za.lissu
 
Amezungumzia takwimu za uongo hazitatusaidia
Takwimu za Mruma kuwa hayo mashobo anayoita Makanikia kuwa container mia mbili na ushee zina tani kumi na tano za dhahabu SI za kuaminika
Using'ang'anie sentensi moja kwenye aya nzima ili uelewe maana
 
Back
Top Bottom