Zitto Kabwe aumbuka idadi ya vifo 100 Uvinza, RPC asema waliofariki ni wanne

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Zitto Kabwe aumbuka idadi ya vifo 100 Uvinza, RPC asema waliofariki ni wanne

SIKU moja baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), kuibua tuhuma za mauaji ya wananchi zaidi 100 katika Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno, amesema taarifa hizo hazina ukweli.

Kamanda Ottieno alisema Zitto amezungumza upotoshaji na anatafuta umaarufu kupitia tukio hilo hivyo apuuzwe.

Kamanda Ottieno alisema ukweli uliopo ni kwamba askari wawili na wananchi wawili ndiyo waliopoteza maisha katika mapigano ya jamii ya wafugaji.

Pia soma
>Kigoma: Askari Polisi watatu wauawa kwa mishale - JamiiForums
>Kigoma: Zaidi ya wananchi 100 wa Jamii ya Wanyantuzu, wadaiwa kupigwa risasi na Polisi - JamiiForums
>Kigoma: Siri ya vurugu zilizosababisha mauaji ya askari wawili yavuja - JamiiForums

------
SIKU moja baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), kuibua tuhuma za mauaji ya wananchi zaidi 100 katika Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno, amesema taarifa hizo hazina ukweli.

Kamanda Ottieno alisema ukweli uliopo ni kwamba askari wawili na wananchi wawili ndiyo waliopoteza maisha katika mapigano ya jamii ya wafugaji.

Juzi, Zitto aliwaambia waandishi wa habari kuwa mauaji hayo yalitokea kwenye mapigano kati ya polisi na Wanyantuzu wilayani Uvinza, takribani siku 11 zilizopita.

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, alidai kuwa katika tukio hilo mbali na wananchi 100 kupoteza maisha pia askari wawili waliuawa.

RPC KIGOMA

Akizungumza na MTANZANIA jana kwa njia ya simu, Kamanda Ottieno alisema Zitto amezungumza upotoshaji na anatafuta umaarufu kupitia tukio hilo hivyo apuuzwe.

“Zitto anazungumza upotoshaji, ni mwongo anatafuta kiki ambazo hazina maana, wananchi wapuuze taarifa yake,”alisema Kamanda Ottieno.

Alipoulizwa endapo hakuna hata mwananchi mmoja aliyefariki katika mapigano hayo, alisema ni wananchi wawili na askari wawili tu waliopoteza maisha.

“Ni kweli askari wawili waliuliwa na jamii hiyo ya wafugaji katika mapigano hayo na ni wananchi wawili tu ndiyo waliofariki na sio 100 kama anavyopotosha Zitto,”alisema kamanda huyo.

Juzi gazeti hili lilizugumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ambapo alisema taarifa za wananchi 100 kuuawa si za kweli na kwamba kwa sasa anasubiri taarifa kutoka kwa Inspekta Generali wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro.

“Sina taarifa za aina hiyo, lakini kuna askari wetu wawili walipoteza maisha na IGP yuko kule tunasubiri atuletee taarifa,”alisema Lugola.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi, Zitto alisema wiki iliyopita yalitokea mauaji ya askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mto Malangarasi, Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza ambapo Mkuu wa Kituo cha Polisi Nguruka aliuawa na wanaodaiwa kuwa ni wananchi wenye hasira.

“Tumekuwa tukifuatilia kwa kina yote yanayojiri huko Uvinza tangu kuuawa kwa askari polisi wetu. Tunasikitika kusema kuwa taarifa tunazozipata kutoka Uvinza zinaogofya mno.

“Kwani tunaambiwa kuwa wananchi zaidi ya 100 wa kabila la Wanyantuzu wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na polisi, wengine wakisema kuuawa hata wakiwa kwenye matibabu hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye purukushani na Jeshi la Polisi.

“Jeshi la Polisi limekalia kimya suala hili, pamoja na IGP kutembelea eneo hilo la maafa. Haiwezekani kamwe tukio kubwa namna hii kutokea halafu Serikali ibaki kimya bila kutoa maelezo yoyote kwa wananchi. Uchunguzi wa kina unapaswa kufanywa ili kutambua nini kimetokea pale Mpeta,”alisema Zitto.

Kutokana na hilo, alisema chama chao kinaendelea kukusanya majina na taarifa za wote wanaodaiwa kuuawa na kitaweka wazi taarifa hizo.

Chanzo: Mtanzania
 
Kuamimi taarifa zinazotolewa na polisi wakati mwingine ni ujinga tu

Polisi hawajawahi kuwa na taarifa za kuaminika kwa umma toka awamu hii iingie madarakani, wao kila siku ni uongo uongo tu kama vile wanatuona Watanzania wote wajinga
Tuamini za zito si ndiyo?
 
Kuamimi taarifa zinazotolewa na jeshi la Polisi wakati mwingine ni ujinga tu

Polisi hawajawahi kuwa na taarifa za kuaminika kwa umma toka awamu hii iingie madarakani, wao kila siku ni uongo uongo tu kama vile wanatuona Watanzania wote wajinga

Correction: kuamini taarifa zinazotolewa na policcm ni ujinga wakati wote.
Ikitokea wakatoa taarifa ya ukweli basi ama ni kwa bahati mbaya au ni ile inayowapendeza wao
 
Kama sio Zitto kuliamusha, wangeendelea kukaa kimya kuhusu vifo vya raia kana kwamba uhai wa raia hauna thamani. Wakati mwingine kuweka chumvi ni mbinu mujarabu ya kuwatoa nyoka pangoni. Takwimu ya Zitto angaa imewafanya waanze kuongelea uhai uliopotezwa wa raia kama walivyokwishaongelea uhai wa askari. Wahanga wote (askari na raia) wapumzike kwa amani.
 
Bado nilkuq nawaza maiti hizo zilipo hadi isijulikane

Damu za hao watu mahala hapo hadi isifahamike

Vyombo vya habari kuanzia vya ndani hadi vya nje

Zitto umejidhalilisha
Shirikisha akili yako kidogo kuhusu hili the njoo uandike tena. Unasema vyombo vya habari!? Hivi umeisha jiuliza ni kwanini vyombo vya habari makini karibu vyote hua havipeleki waandishi wake kwenye press za maana hasa wana siasa wa upinzani!? Halfu wananchi waue askari 2, nature ya police wakionaga wenzao wameuawa hua wanaacha tu hali ipite hivyo hivyo!? We labda sio wa nchi hi, unaandika ukiwa mbali na bongo! Well, labda ujiulize why Azori hadi sasa hivi haonekani wakati alikua ameenda kuandika habari za Mkiru. Police hawana historia ya kusema ukweli mkuu!
 
Zitto aliwahi pia kusema Tanzania ina njaa, Mbowe akasema kama serikali itashndwa kununua chakula basi CDM watamnunulia kila mtanzania chakula,muda kidogo ukapita Lissu akspigwa risasi,Chadema na wabunge wrote walishindwa kumlipia mwenzao nauli aende Nairobi, Mungu mkubwa mbunge ccm akaingia mfukoni akaokoa maisha ya Lissu, sijui walidhani kulisha watanzsnia mil 50 ni sh laki 7,Magu alisema hamna mtu atakayekufa kwa njaa na kweli hamna hata mtu mmoja aliyekufa.Hawa ndio wapinzani wetu
 
Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu aliyeamini zile ngonjera za ZZK. Anaona hakuna njia nyingine yoyote ya kujipatia umaarufu ila ni kutunga uongo na upuuzi wa kuonyesha kuwa serikali inaharibu kila kitu ili usionekane uzuri wowote wa serikali hii. Inawezekana kuna wanaoamini ila watakuwa ni wale wasiopenda kutafakari wanachoambiwa.
 
Back
Top Bottom