Zitto Kabwe aomba Bunge lisimamishe shughuli zote juu ya Jairo!

Mbunge Shelukindo hawezi kuomba radhi kwa sababu ushahidi anao ( BARUA ILIYOSOMWA BUNGENI ) kama ni hivyo Luhanjo akane kama kweli barua iliyosomwa Bungeni siyo halali!. Tumewazoea IKULU kusafishana pale panapohitajika watu kuwajibishana. Tunaomba CAG afanye uchunguzi kama kweli Wanyama Hai -twiga walisafirishwa nje ya nchi, kisha Luhanjo atoe ripoti kwa Wananchi.
 
Bajeti imeshapitishwa!!
Tatizo sio kumwadabisha Jairo,aliwaona komedi kwa sababu kila kilichotokea hakikuwa sahihi kwake,sasa afanye nini? hana hatia.Pinda alizungumza bila ushahidi wowote,alitumia maneno ya wanasiasa kumhukumu jairo.

Kama hana kosa hakuna maamuzi magumu Ya nini? kwa manufaa ya Nani?...CCM inabaki chama bora chenye misingi imara na kinachosimamia tararibu na kanuni.
 
Zitto katoa hoja ya bungeni taarifa ya CAG ipelekwe bungeni mara moja..wabunge wengi wameunga mkono hoja ya zitto, ndugai kaenda kwenye faragha maana hali ni tete amemomba simbachawene avae joho kwa mda mfupi
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Sijui kama Speaker na uongozi mzima wa Bunge kama mhimili mmojawapo wa dola wanaona jinsi hiki chombo kinavyovunjiwa heshma. Wametukanwa sana kupita kipindi kingine chochote katika historia ya nchi hii, kwanza Mayor wa DSM, na sasa Jairo.

Wabunge wote wanatakiwa wakomae ili hatua madhubuti zichukuliwe vinginevyo hiki chombo kinaelekea kuzimu.
 
Zitto kaomba shughuli za serikali bungeni ziharishwe, mpaka taharifa ya CAG iletwe bungeni.Ndugai kashindwa kutoa maamuzi, kaamuru kamati ya uongoz ikae na itatoa maamuz baada ya nusu saa.
 
Kimeshawaka huko hali tete zitto kawasilisha hoja,kuwa shughuli za bunge zisimame ili ripoti ya CAG ijadiliwe,na hoja imeungwa mkono na wabunge takribani wote.
 
Wabunge wamejidhalilisha wenyewe kwa kuleta tuhuma bila kujipanga vizuri, ukitaka kumshikisha adabu mtu yeyote ambaye ni swahiba wa Kikwete inabidi ujipange usiende kichwa kichwa.

Hamuoni akina mwakyembe walivyojipanga kwenye Ishu ya lowassa? Wangeenda kichwa kichwa mpaka leo Lowassa angeendelea kuwa disisheni meka katika nchi hii. Japo kumpeleka mahakamani imekuwa ngumu
 
Zitto na wabunge wote komaeni, vinginevyo reputation ya bunge is at stake! Serikali haiko serious so the only option left ni kwa bunge kushika hatamu. Komaeni.
 
I second you Technician.

This lady was being dramatic and emotional instead of rational. Angekuwa rational na kupanga facts zake vizuri angeweza kufanikiwa. She is now coming across as a vengeful woman instead of mtu mwenye uchungu wa kweli na nchi yake.

Mie naomba aombe radhi na kwa kumchafua CS kama asipoleta hard facts to back up her accusation.
 
Hapa kweli kuna moto mkubwa kuaka!
Je ni sahihi Katibu Mkuu kuchukua maamuzi mazito bila kumshirikisha yule alieagiza kazi ya uchunguzi. PM na Bunge kujulishwa kwanza?
Ni dalili za kufunika kombe wanaharamu wapite?
 
Kweli Tanzania ni zaidi ya Tanzania. Ile ilikuwa inasound kama kuna kitu nyuma ya pazia.
 
Waziri mkuu pia anapaswa aliombe bunge msamaha kwa kurupuka na kupayuka bungeni.
Aidha waziri mkuu amuombe Jairo msamaha kwa kauli aliyoitoa bungeni zidi yake(kwani alishamtia hatiani).

Pia mh.Godbless Lema aombe muongozo ikiwa mtu mkubwa kama waziri mkuu atakurupuka na kulielezea bunge kwa kujiamini mambo ambayo hayana ukweli na yanayolenga kuvunjiana heshima bunge linapaswa kufanya nini.

Mwisho rais apime mwenyewe uzito wa tatizo ikiwa watendaji wake wakuu wanatofautiana kiasi hiki afanye nini.
 
Namuona Mbangwa kwa mbali akija kwa kasi sana kurudi ofisini kuenedelea na kazi kama kawaida. very sad when will this culture of impunity among our leaders end?
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Zitto Kabwe ametoa hati ya dharura za kulitaka Bunge kusimamisha mambo yote ya serikali kuzungumziwa Bungeni kwa sababu aliyetuhumiwa ni Mtumishi wa Serikali na aliyemchunguza ni Mtumishi wa Serikali. Na isitoshe Luhanjo amemwambia Jairo anaweza kwenda Mahakamani kuwashitaki Wabunge waliomtuhumu kwa Defarmation. Kwa kuwa Bunge ndilo linalotuhumiwa, basi wasiendelee kujadili mambo ya Serikali mpaka Riport ya CAG ifikishwe na kujadiliwa na Wabunge.

Waziri mmoja wa Ofisi ya Waziri Mkuu akatoa kifungu kupinga akidai kwamba kifungu alichotumia Zitto hakiwezi kukubalika kwa sababu aliitaji kutoa taarifa kwa Spika kabla ya kuleta hoja yake

Ndugai akasema, Mh. Zitto alimpa Ki-note kabla hajaingia bungeni kumtaarifu kwamba ataleta hoja hiyo.

Hoja imeungwa mkono na wabunge wengi. Lakini kwa kuwa hoja ni Nzito, Naibu spika ameomba kwanza akae na wenyeviti wa Bunge ili walijadili kwanza na kumtaka Simbachawene akavae kama kiongozi wa bunge ili walijadili
 
Natamani kuamini kuwa maamuzi magumu yanaweza kufikiwa, lakini nikiangalia historia roho yangu inanikatalia kabisa, hebu na tusubiri. Swali langu kwa mawizara juu ya maandalizi ya kusomwa kwa bajeti hizi, kwa nini hawaweki vipengele vya maandalizi haya kwenye bajeti mama ambayo itakuwa inasomwa bungeni kuwa..."kifungu cha maandalizi na usomwaji wa bajeti - bilioni moja!'. Leo hii wala tusingemshika uchawi bwana Jairo na waraka wake kwa idara zake....
 
Waziri mkuu pia anapaswa aliombe bunge msamaha kwa kurupuka na kupayuka bungeni.
Aidha waziri mkuu amuombe Jairo msamaha kwa kauli aliyoitoa bungeni zidi yake(kwani alishamtia hatiani).
Pia mh.Godbless Lema aombe muongozo ikiwa mtu mkubwa kama waziri mkuu atakurupuka na kulielezea bunge kwa kujiamini mambo ambayo hayana ukweli na yanayolenga kuvunjiana heshima bunge linapaswa kufanya nini.
Mwisho rais apime mwenyewe uzito wa tatizo ikiwa watendaji wake wakuu wanatofautiana kiasi hiki afanye nini.

Sidhani kama Pinda ni waziri mkuu. Hivi anajisikiaje pale inapodhihirika yeye na bosi wake hawafikirii kwenye the same track, inakuwaje? Jamaa kamwagwa hadharani. Sijui kama tutafika kwa usanii huu.
 
Mh! Mimi ninakijisafari kidogo napita tu nawaageni tutaonana baadae inshallah? Mpeni hongera zake Blaza Jairo.
 
Pinda asipounga hoja hii basi kuanzia leo, Pinda na Shelukindo watuambie kuwa Jairo anapewa mamlaka au nguvu kiasi hicho na nani???? Basi Pinda ajiuzulu maana jairo ana nguvu kumshinda yeye...
 
Back
Top Bottom