Zitto Kabwe ajisalimisha polisi

Mkuu huyu ndo Magu uliyempigania,
Sasa tulia tuliii dawa iingie sindano isijevunjikia kwenye tako
He is far much better compared to Lowassa...

Hatujazoea uhuru kuminywa namna hii.....even freedom of expression inakuwa tabu
 
Kweli ngoja tusubiri tuone nini kinatokea; tena naomba wadau tuwe kimya na wavumilivu ili tuanze kuthibitisha hofu yetu kuwa, kile kinachoitwa "chaguo la Mungu" kinabadilika na kuwa zimwi lisilotujua. Kweli Tanzania inafikia hapa; viongozi wa kisiasa kukamatwa, kudhalilishwa na kuzuiwa wasifanye siasa? Kweli tumefikia mahala ambapo sasa hatupaswi tena kujadili mambo yanayohusu taifa hili kwa uwazi na eti tukithubutu tunaweza kukamatwa. Hii ni aibu ya kutisha!

Natoa wito kwa wanaharakati na wazee/viongozi wastaafu; wasomi na wanasheria kuunganisha nguvu na kuzuia (kisheria na kwa maridhiano) muendelezo wa udhalimu unaowezekana kukita mizizi yake katika taifa hili. Mikakati hii ya kukaba/kubaka democrasia haiwezi kuachwa kuendelea, kwa sababu mwisho wa siku Mungu atawahukumu wadhalimu lakini sisi tutakaoendelea kuuona udhalimu ukiendelea bila kufanya chochote kuusitisha, hukumu yetu itakuwa ni kali zaidi.

Na tumuombe Mungu alete uvuvio na hekima kwa viongozi wa kisiasa; wadau wa utawala bora ili watawala wafanye mageuzi chanya ili waiongoze nchi hii katika misingi sahihi ya kujenga nidhamu ya hiari na upendo badala ya vitisho na chuki.

MUNGU ibariki Tanzania
 


Vipi wamempiga mbata? Itakuwa kazi bure kama Askari wetu hawajamtia mbata!
 
Hana kosa lolote ni uharamia tu unaofanywa na Magufuli kupitia polisi ili kuwatisha Viongozi wa upinzani na wanachama wa upinzani.

Zitto kakosa nini? nimepitwa wandugu!
 
Tuendelee kusali na kumwomba mungu ataonyesha haki ya kura zetu siku moja
 
Maumivu ya kichwa huwanza polepole!![emoji86] [emoji86] [emoji86]
 
Kwa hii nchi yetu ilivyo huitaji kutumia nguvu kubwa kuwazuia wapinzani, waletee watanzania maendeleo uone kama utapata upinzani mkubwa, pamoja ukosefu wa elimu tulionao watanzania ila wengi ni wenye busara na hekima.

JPM alivyoanza utawala wake wachache sana walimpinga, wengi tulimsapoti na hata wapinzani tulikosa hoja, hata harakati zilipungua, ila sasa kwa kitendo cha kuminya demokrasia na kubana uhuru wa vyama vya upinzani kufanya harakati zao kisiasa, zinaondoa umoja wa kitaifa.

Serikali inatakiwa ijue upinzani sio kina Mbowe peke yao, hata kwenye maofisi ya umma kuna wapinzani wengi tu.
 
Ina maana zitto ametafutwa na polisi kwa siku mbili bado hawajampata,sasa amewezaje kuongea na waandishi wa habari?Yaani polisi wameshindwa kumpata zitto? Naanza kuhisi zitto ni beyond sirro kinetwork ndani ya jeshi la polisi au hakuna wakujitoa kafara direct kumtia nguvuni ? mwisho wa siku polisi kama hakuna report yoyote ya uvunjifu mbona wanampa coverage ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…