Zitto Kabwe aiponda bajeti, asema Tanzania itaanguka vibaya sana kiuchumi haijawahi tokea

Sikuona sawasawa ,hivi kodi ya majengo walikusanya trilion 15 au ni trilion 1.5.

Maana hata kama ni trilion 1.5 bado ni pesa ndefu inaweza kuleta mabadiliko makubwa
 
Bajeti hii ni nzuri sana, ila kazi ya kwanza ya mpinzani ni kupinga kitu kizuri kinachotokana na serikali iliyoko madarakani.
 
Namwona ZK akirudia akili zake za awali na polepole anajijenga na waasisi wa uasi ule ambao yeye aliingia kichwakichwa bila Kujua wenzake Mkumbo nk walikuwa kazini wakimtumikia bwana tumbo aka ccm
 
Mara baada ya bajeti ya mwaka jana Zitto alitoa kauli kama hii. Mwaka juu ameirudia tena. Nani anashangaa?
 
Kama wabunge walifuraia kushikwa kwa mchanga,na kusahau kuwa dhahabu bado inasafirishwa,wataacha kufuraia kufutwa kwa kodi ya roadlicens,na kuongeza kodi kwenye mafuta kweli?
Mkuu hili liko tu sawa na issue ya ripoti ya Mruma juu ya makinikia. Wengi tulikimbilia kupongeza kazi "nzuri" ya tume kabla ya kuitafakari kisomi na kitaaluma. Tulipofanya uchambuzi ndio tukaja kugeuka na kuiita rubbish...kwa maana haikuwa na uhalisia. Huwezi kuwa na kiwango kikubwa kiasi hicho kwenye mchanga wa Buzwagi na Bulyanhulu.
Sasa na hili la eti road licence imefutwa badala yake eti imehamishiwa kwenye mafuta ni upuuzi mwingine. Kifupi ni kuwa road licence sasa inalipwa kwa tafsiri sahihi waliyoitaka kina Msigwa...once pale ununuapo gari. Sasa kusema eti unaongeza shs 40 kwenye mafuta iwe ndio road licence ni upuuzi mwingine. Hivi kwani mafuta yanatumika kwenye magari tu? Hivi yule atumiaye mafuta ya taa yeye road licence inamhusu nini? Vipi mimi ninayetumia mafuta kwa ajili ya kajenereta kangu?
Nikupe mfano: mimi ninapofanya kazi hakuna umeme wa grid. Tunatembeza majenereta makubwa ya diesel at least matatu kwa mwaka mzima nonstop. Matumizi yetu ya mafuta ya diesel ni lita laki 7 kwa mwezi. Kati ya hizo lita laki 4 huishia kwenye majenereta. Ina maana ongezeko hilo la shs 40 litatuathiri zaidi kwenye gharama za ufuaji umeme kuliko sehemu nyingine yoyote.
Kati ya lita laki tatu zilizobaki lita laki 2 na nusu ni kwa ajili ya mashine zingine na magari makubwa ya uzalishaji/uchimbaji ambayo hata hayajawaji kugusa barabara za umma.
Hapa najaribu tu kuonesha kuwa ni makosa kuliita ongezeko hilo la shs 40 kuwa ni la road licence wakati linagusa kila mtumiaji mafuta hata asiye na gari. Kiufupi linaenda tu kuongeza bei ya mafuta na athari zake zitacut across kila nyanja...usafirishaji, uzalishaji, matumizi ya kawaida ya mlalahoi anayetegemea mafuta ya taa,nk.
 
Hoja hapa sio kodi mbalimbali kupunguzwa, isipokuwa Zitto anajua kuwa bajeti hii ya pili ktk utawala wa JPM imetisha,imekithi viwango haijawahi kutokea.
 
Hujui hata unachoandika ni kitu gani. Eti unasema, inaweza kuwa worse or vice versa. Hapo tu, mbobezi wa masuala ya uchumi atang'amua kwa sababu hulipi kodi kwa kupost hapa JF, ndiyo maana umeamua kuandika huo utumbo. Umesoma vizuri bajeti iliyowasilishwa jana? umesoma financial indicators katika mabenki yetu? mfumuko wa bei upo kiasi gani sasa? single digit. Siyo? Hivi unajua nchi hii mfumuko wa bei uliwahi kufika 30% mwanzoni mwa miaka ya 90s. Leo upo chini ya aslimia 6% wewe unaandika utumbo wako hapa. Jaribu kutumia hekma na busara. Acha kuleta stori za vijiweni, kwenye migahawa na wanywa viroba.
Mngese wewe
 
Back
Top Bottom