Zitto Kabwe aiponda bajeti, asema Tanzania itaanguka vibaya sana kiuchumi haijawahi tokea

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Zitto anasema watu wamepotezwa na hatua za kupunguza kodi tu ambazo hazimaanishi chochote na seriakali ya awamu ya tano itapata anguko kubwa la kiuchumi ambalo halijawahi kutokea Tanzania

WhatsApp Image 2017-06-08 at 21.10.18.jpeg


Kitila Mkumbo anaifagilia bajeti na pia anajivunia kuwa kati ya watu walioiandaa
WhatsApp Image 2017-06-08 at 21.10.17.jpeg
 
Kitila nae, yaani kuwa ndani ya serikali leo ndio anapongeza bajeti miaka yote alikuwa analia, hii ya maji haikidhi hata mikoa 10, lakini yeye kama katibu anapongeza, ngoja tuweke kumbukumbu mwakani kusiwe na kijiji hakinamaji safi salama na yanayopatikana kwa uhakika, asije singizia bajeti.
 
Kazi ya upinzani ni kupinga. Wakianza kukubali mambo ya serikali watakua wamesahau wajibu wao wa kupinga kila kitu. Upinzani inabidi wapinge lolote lile la serikali either zuri au baya ila waendelee kuwa wapinzani
 
Kitila nae, yaani kuwa ndani ya serikali leo ndio anapongeza bajeti miaka yote alikuwa analia, hii ya maji haikidhi hata mikoa 10, lakini yeye kama katibu anapongeza, ngoja tuweke kumbukumbu mwakani kusiwe na kijiji hakinamaji safi salama na yanayopatikana kwa uhakika, asije singizia bajeti.
Ndio asili ya wanasiasa wetu wa afrika, yuko radhi asaliti mamilion ya watu, kwa faida ya ukoo wake wenye watu 30
 
Records si zipo lakini

Sikuelewi. Mimi namkatalia zitto anaposema kwamba uchumi utaporomoka, kiasi kwamba haijawahi kutokea. Hilo nakataa, na haliwezi kutokea. Lilishatokea miaka ya 80 baada ya vita ya uganda. Maduka hayakuwa na bidhaa, watanzania walikuwa wanakula unga wa yanga (mahindi ya njano), mabetri dukani ilikuwa ni adimu, sabuni, etc etc. Sasa wewe kwa akili yako unadhani huko ndiko tunakolekea? Jaribuni kufikiri kabla ya kuandika pumba hapa JF.
 
Kama wabunge walifuraia kushikwa kwa mchanga,na kusahau kuwa dhahabu bado inasafirishwa,wataacha kufuraia kufutwa kwa kodi ya roadlicens,na kuongeza kodi kwenye mafuta kweli?
 
Back
Top Bottom