TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,564
Amani iwe kwenu wana ukumbi:
Mkuu wa chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema hawana mpango wa kujiunga na ukawa kwa kuwa chama chake kina sera tofauti.
Ameyasema hayo leo ndani ya kikao chao cha ndani na kusisitiza kuwa azimio lao la Tabora linamtaka kila mtu kutangaza mali na madeni yake ndo ajiunge naye.
Chanzo ITV taarifa ya habari ya saa 2 usiku.
Hakiongea na wanachama wenzake wa ACT-Wazalendo,kiongozi mkuu wa huyo Bw.ZZK amedai kwamba ACT haiwezi kujiunga na UKAWA kutokana na tofauti za kifalsafa baina ya ACT na UKAWA,pia akinukuu azimio la Tabora ambalo linamtaka mwanachama wa ACT kutamka Mali,Madeni na Maslahi binafsi kitu ambacho amedai UKAWA akipo.
Swali: Hivi ni nani alianza kumkataa mwezake asijiunge naye?ni ACT au UKAWA?
Au ndiyo kale kamsemo ka wahenga kanachosema "SIZITAKI MBICHI HIZI" kanajidhihirisha kwenye kauli hiyo ya ZZK?
Source: ITV Habari!
kila kitu kinamwisho wake...na huu ndo mwisho wa dogo/kaka yetu zitto...tumpe pole.
Sielewi nini hasa mantiki yako mkuu,.siamini kama ni kweli umekaa na kutafakari kwa mda mpaka kufikia kuandika uzi huu au kwa sababu ya chuki zako tu umeamua kuandka. Kaka mimi sio shabiki wa Zitto bali mimi naamini katika umuhimu wa upinzani katika maendeleo ya nchi. Alichosema Zitto juzi ilikua UPINZANI kuwa na nguvu na kuondoa mfumo dhalimu wa chama tawala, UKAWA wamekaa wakasema hawamkaribishi Zitto kwao, ACT bado ni wapinzani, UKAWA bado ni wapinzani, Alichosema Zitto leo ni kuwa pamoja na kutokukaribishwa UKAWA bado chama chake kitaendelea kusimama kama miongoni mwa vyama vya upinzani. Sasa hapo kakosa nini? Jamani MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI, Kuna wakati chuki zetu binafsi zinatufanya kutokuangalia katika ukweli na haki.
Yani huyu jamaa kaishiwa sera kabisa nafsi yake inamsuta. Ninachokifahamu mimi ni kwamba Ukawa hawawezi kumkaribisha Zitto kutokana na uhaini alio ufanya Chadema.
Zitto mpaka anaboa na hilo azimio lake la Tabora. Kila mahali yeye analitaja tu. Kwani mtu akishataja mali na madeni yake automatically anakuwa kabatizwa na kuachana na ufisadi wake!?
Mala chama changu kipo tayari kushirikiana na ukawa mala siwezi kuungana na ukawa,,sasa tumueleweje huyu mtu?? Kwa heri zitto
Hatutajiunga kamwe na wapiga dili hawa wa UKAWA, wameshauza vyama vyao kwa mafisadi kuna nini tena huko, tutabaki na ACT yetu
Huyu si aliandika barua ya kuomba kujiunga na UKAWA
Chama chake kinasubiri wabunge reject ambao si washambuliaji, Chadema wanasajili viungo wakabaji na washambuliaji wa bei mbaya!
Huo ndio ukweli na yeye analijua hilo,eti azimio la tabora
Hawa watu wana chuki kila anachokifanya Zitto kwao ni kibaya. Waache waendelee kumpaisha Zitto. Waache waendelee kujitoa ufahamu!