Zitto Kabwe achunguzwa kuvuna PAP

Zitto Kabwe achunguzwa kuvuna PAP

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,868
Reaction score
5,753
Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) ameanza kuchunguzwa na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa kwa kutuhuma za kutumia rafiki zake wakiwamo mawakili Beatus Malima na Albert Msondo , kupokea fedha kutoka Kampuni ya Pan Africa Power Solutions(T)Limited. Habari zilizolifikia Gazeri la Jamhuri zinaonesha kuwa April 3 na 8, 2014 kwa nyakati tofauti marafiki zake hao walipokea Sh. Milioni 10 na dola 5,000 kutoka Kampuni hiyo kwa niaba ya ZITTO.Pia kupitia Kampuni yake ya Gombe Advisors and Leka Dutigite Ltd iliyosajiliwa BRELA kwa namba 92959 Agosti 13 , 2012 na kipindi cha miezi minne tu tangu iliposajiliwa ilianza kupata fedha kutoka Mashirika ya Umma tofauti na Kampuni za Watu wengine ambao hawana wadhifa kama alio nao.

Kampuni ya Leka Dutigite Ltd imepata zaidi ya sh. Mil. 12.2 kutoka Hifadhi ya Taifa ya Sadani na mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) , zaidi ya Sh. Milioni 80. Kitendo cha kupokea hizo na zile za IPTL ndivyo vinavyochunguzwa iwapo hakutumia nafasi ya PAC kwa manufaa binafsi.

Hapo chini ni baadhi ya nyaraka zinazofanya Mbunge wa Kigoma Kaskazini , Zitto Kabwe achunguzwe kutokana na madai ya kuchukua fedha Kampuni ya PAP
attachment.php

Chanzo: Gazeti la Jamhuri
 
Attachments

  • zitto.jpg
    zitto.jpg
    35.3 KB · Views: 10,669
Kwenye orodha ya watu waliokua wakimtetea zzk kwamba kaonewa na CDM, jina lako pia lipo! Hatimae umeanza kuelewa sasa.
 
Kwa adabu tu zitto angejiuzuru wadhifa wake sawa na ngeleja na chenge, huu ndo uwajibikaji wa kiungwana. nasikia upo ushahidi wa cctv, ndo maana siku zote nasema jk vunja hili bunge tuunde serikali ya mpito tuanze moja haya yote mapiga dili. juzi hapa hawa wabunge wa cdm walikuwa watoto wa shule na wengine wanauza grocery leo wanautajiri wa kutisha wamefanya biashara gani ndani ya miaka mitano hii tu?
 
Wakati wa mjadala wa sakata la ESCROW bungeni hili swala liliibuliwa na Nchambi pamoja na Lusinde, wakadai wana nyaraka. Lakini wakati Zitto akijibu hoja nakumbuka aliweka commitment yake swala lipelekwe kamati ya maadili ya bunge na yeye yupo tayari kuwajibika ikiwamo kujiuzuru ubunge wake ikiwa itathibitika ni kweli.

Kwangu nilijua kwa kuwa jambo lile liliibukia bungeni tena baina ya wabunge kutuhumiana nikajua commitment ya Zitto ni suluhu mujarabu ili ukweli ufahamike. Sasa kama wale ndugu Nchambi na Lusinde waliibua hili na kudai wana nyaraka kwa nini wasingekubaliana na Zitto na kuweka commitment zao kama mwenzao? Na kwa nini Spika alilikalia kimya pasipo ufafanuzi wowote? maana hizi zilikuwa ni tuhuma dhidi ya mwenyekiti ambaye kamati yake imeshiriki uchunguzi uliokuwa unajadiliwa.
 
Wakati wa uchunguzi, zitto kabwe ashinikizwe kuachia ngazi ndani ya kamati ya PAC kupisha ucbunguzi
 
Mkuu, kwa mazingira ya siku ile unafikiri kuna kitu kingefanyika? Zitto alilia lia kuomba huruma ya wabunge eti kutokana na kubusishwa kwa kashfa yake na ugonjwa wa mama yake
 
Kwenye orodha ya watu waliokua wakimtetea zzk kwamba kaonewa na CDM, jina lako pia lipo! Hatimae umeanza kuelewa sasa.

Unaweza kumtetea mtu kwa kosa moja lakini usimtetee kwa kosa jingine. Kwa hili hata mie nashinikiza Zitto achukuliwe hatua kali. Kwa nini yeye na si DeoFilikunjombe?
 
Wakati wa uchunguzi, zitto kabwe ashinikizwe kuachia ngazi ndani ya kamati ya PAC kupisha ucbunguzi

asipoachia ngazi tutaenda kumtoa kwa nguzu bungeni, tumeshaanza kuhamasishana na kufikia jmosi haja ng'oka tutaanza kupanda mabasi kuelekea dodoma tayari kwa kazi ya kumng'oa asijifanye kotapini. tundu lissu lema na sugu kama mtamshindwa basi tegemeeni mshikemshike wiki ijayo, hakianani dodoma haitakalika.
 
Mie namwunga mkono Zitto katika mengi. Ila katika hili, awajibike.
 
Zitto hajawahi kuacha ufisadi hata siku moja kaanza ufisadi kitambo rushwa kwake ndiyo kama ada siku hizi kaungana na mengi na mafisadi mengine ni shida.
 
Serikali hii utafikiri kichwa cha mwendawazimu.
Hawa PCCB wanaojianya wanachunguza wanashindwaje kuchunguza na kubaini wakina nani walichuka ela Mabilioni ya pesa kwenye Lumbesa pale Stanbic bak.?Ni uchizi husio na kifani. Unaacha kuchunguza watu waliokwapua a lot of billions through Stanbic unaanza kukimbizana na hawa watu waliochukua sijui vimilioni kumi sijui tano.Hii ni akili au matope.
 
asipoachia ngazi tutaenda kumtoa kwa nguzu bungeni, tumeshaanza kuhamasishana na kufikia jmosi haja ng'oka tutaanza kupanda mabasi kuelekea dodoma tayari kwa kazi ya kumng'oa asijifanye kotapini. tundu lissu lema na sugu kama mtamshindwa basi tegemeeni mshikemshike wiki ijayo, hakianani dodoma haitakalika.
Kwa nchi za watu zitto kama china zitto anasifa zote za kunyongwa kwa kufisadi taifa halafu anakimbilia kujikosha kwa watu kumbe yeye ndiyo mwizi.
 
nilijua tu hili suala litafika hapa lilipo..PCCB watakuja na mambo ya kustua nina uhakika Zitto kapokea zaidi ya shilingi hizo zilizotajwa
 
Kumbe cdm walikua sahìhi kabisa kumfukuza huyu jamaa.
 
Serikali hii utafikiri kichwa cha mwendawazimu.
Hawa PCCB wanaojianya wanachunguza wanashindwaje kuchunguza na kubaini wakina nani walichuka ela Mabilioni ya pesa kwenye Lumbesa pale Stanbic bak.?Ni uchizi husio na kifani. Unaacha kuchunguza watu waliokwapua a lot of billions through Stanbic unaanza kukimbizana na hawa watu waliochukua sijui vimilioni kumi sijui tano.Hii ni akili au matope.

mbona muhongo hajachukua hata senti tano katimliwa iweje yeye aliyekomba milioni kumi aachwe? tutaandamana kwenda dodoma labda awe analala bungeni
 
Zitto mwizi sana halafu akibanwa kujibu maswali anakimbilia kulia kama mtoto mdogo ili ahurumiwe jamaa kafisadi kweli.
 
Ni kweli Lizaboni kulikuwa na hot debate siku ile na hata maelezo ya Zitto yaweza kuwa ilikuwa ni kutafuta huruma ya wabunge na jamii kwa ujumla lakini still haiwezi kuwa excuse ya bunge lenye dhamana kubwa ya kusimamia uwajibikaji kwa mihimili mingine lishindwe kuwajibika lenyewe.

Binafsi bado naona bunge lilipotoka sana kuachia tuhuma zile zipite bila uchunguzi wowote.
 
Last edited by a moderator:
nilijua tu hili suala litafika hapa lilipo..PCCB watakuja na mambo ya kustua nina uhakika Zitto kapokea zaidi ya shilingi hizo zilizotajwa
Hii tabia ya kuchukua pesa kwa zitto hajaanza leo hata mbinu yake anayotumia ni hii wala haijabadilika kwa yeye kutumia watu kuchukua pesa zake halafu ndiyo wa kwanza kujikosha.
 
Back
Top Bottom