Zitto chupuchupu kutimuliwa CHADEMA!

Zitto chupuchupu kutimuliwa CHADEMA!

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,613
Reaction score
6,735
*Hoja ya kumng’oa yajadiliwa Baraza Kuu CHADEMA


KWA mara ya pili mfululizo, katika kipindi kisichozidi miezi sita, jitihada za siri za kujaribu kumng’oa kutoka ndani ya CHADEMA, Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe zimegonga mwamba.

Tukio la kukwama kwa mkakati huo lilitokea ndani ya kikao cha Baraza Kuu la Chadema kilichoketi juzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kwamba, hoja ya kutaka Zitto na Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda Magalle wavuliwe uanachama wa Chadema ililetwa na uongozi wa Baraza la Vijana la Taifa la chama hicho (BAVICHA).

Wajumbe watatu tofauti wa kikao hicho, waliozungumza na Mtanzania Jumatano walisema hoja hiyo ambayo haikuwa miongoni mwa ajenda za kikao hicho, iliibuliwa wakati wa kujadili mengineyo.

Kwa mujibu wa Bavicha, Zitto na Shibuda walishitumiwa kwa madai ya kuhatarisha uhai wa chama hicho kutokana na kile kilichodaiwa kuwa na mienendo ya kugawa viongozi na kutoa matamshi yanayohatarisha uhai wake.

Kosa jingine alilotuhumiwa nalo Zitto pamoja na Shibuda ambaye hata hivyo hakuwemo kwenye kikao hicho ni tuhuma kwamba anatumiwa na mahasimu wa chama hicho wenye lengo la kukidhoofisha kisiasa.

Wapasha habari wetu walieleza kuwa hatua ya Mbowe kuruhusu hoja hiyo kuibuka ilisababisha Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe aliyekuwa akiongoza kikao hicho alazimike kuzima kuendelea kwake baada ya mkutano kukumbwa na tafrani.

Tafrani hiyo ilisababishwa na kuibuka kwa mgawanyiko mkubwa wa kimakundi, moja likiunga mkono msimamo wa Bavicha huku jingine likiwatetea Zitto na Shibuda.

Hata hivyo, mpira ulionekana kumgusa zaidi Zitto ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe waliokuwamo ndani ya chuma cha mkutano wakati hoja hiyo ilipoibuliwa.

Taarifa zimeeleza kuwa, wajumbe tisa walichangia mjadala huo huku watatu kati ya hao, wakimtuhumu Zitto kwa kulifadhili genge la vijana wakorofi ndani ya Bavicha ambalo baadhi ya wafuasi wake walitimuliwa katika chama hicho hivi karibuni.

Habari zaidi zinaeleza kwamba, wajumbe wawili walipinga hoja ya kutaka Zitto afukuzwe na badala yake wakakieleza kikao hicho kwamba, shutuma zilizokuwa zikielekezwa kwake hazikuwa za kweli.

Wajumbe hao walieleza mshangao wao wa kuendelea kusakamwa kwa Zitto ambaye ni kiongozi wa juu wa chama hicho wakati kukiwa na kundi la vijana ambao wako katika rekodi za kupata kumtukana wakiachwa wakiendelea kuwa wanachama.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mjumbe kutoka Longido ambaye alionekana kutofurahishwa na mwenendo huo wa mambo, alikieleza kikao hicho kuwa, CCM kimepandikiza ugomvi ndani ya chama hicho ili Zitto aonekane mbaya.

Aliwataka wajumbe wenzake kuwa makini na njama hizo za CCM ambazo alidai iwapo zingechukuliwa juu juu zingeweza kusababisha mpasuko mkubwa wa kisiasa ndani ya Chadema.

Hata hivyo, baada ya hali hiyo kutokea, Mwenyekiti wa kikao hicho, Mbowe, ambaye alikuwa akishinikizwa na wajumbe atoe nafasi kwa Zitto kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, alikataa kufanya hivyo.

Hatua hiyo ya Mbowe ilipingwa na baadhi ya wajumbe waliosikika wakiguna na mmoja wao akasikika akisema kwamba, pengine viongozi wa juu wa chama hicho walikuwa sehemu ya mkakati wa kumng’oa Zitto.

Zitto mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alijibu kwa kifupi, “I have no comment” akimaanisha kwamba hakuwa na cha kusema kabla ya kukata simu.

Kama ilivyokuwa kwa Zitto, ndivyo ilivyokuwa pia kwa Mkurugenzi wa Habari wa chama hicho, John Mnyika ambaye hata baada ya kupigiwa simu kwa zaidi ya mara moja, hakuwa tayari kueleza lolote.

“Pengine katika hayo uliyouliza, miye binafsi sina majibu nashauri ungewasiliana na huyo aliyekupatia taarifa hizo kwa ajili ya kukupa maelezo sahihi,” alieleza Mnyika.

Kwa muda sasa kumekuwepo na taarifa za kuwapo kwa mikakati ya chini chini inayoratibiwa na wanasiasa walio ndani ya Chadema ya kutaka Zitto avuliwe uanachama au anyang’anywe nyadhfa zake zote ndani ya chama kwa kile kinachodaiwa kuwa amekuwa akitofautiana kimsimamo na baadhi ya viongozi wake wakuu.

Makada wa Chadema ambao wamekuwa wakihusishwa kushiriki mpango huo ni pamoja na wabunge wa chama hicho na maofisa wa makao makuu ambao hivi karibuni waliripotiwa kuanza kufuatalia kile walichoeleza kuwa ni mali za Zitto kwa lengo la kuzitangaza.


Chanzo: Mtanzania
 
ikifika december bado Zitto Kabwe hajafukuzwa ndani ya CHADEMA ntarudisha kadi yangu kwa hiari...nikiwa kama mwanachama wa kawaida sana, nasikitiswa sana na jinsi kijana huyu anavyohujumu mipango na mikakati ya chama, zito ni mbinafsi, msiri, mchochezi, mpika majungu na M-CCM pia...anamatukio ya ajabu ajabu sana..SHAME ON ZITTO ZUBERI KABWE.
 
CHADEMA ni chama makini wanafanya maamuzi muhimu hawakurupuki, kama ZZK anafanya hila za kuisambaratisha CHADEMA atafuatiliwa na kuchukuliwa hatua, hakuna superstar.
 
ikifika december bado zito kabwe hajafukuzwa ndani ya chadema ntarudisha kadi yangu kwa hiari...nikiwa kama mwanachama wa kawaida sana, nasikitiswa sana na jinsi kijana huyu anavyohujumu mipango na mikakati ya chama, zito ni mbinafsi, msiri, mchochezi, mpika majungu na M-CCM pia...anamatukio ya ajabu ajabu sana..SHAME ON ZITO ZUBERI KABWE.

we unafata matendo ya mtu!au matendo ya chama!
 
CHADEMA ni Chama makini unatakiwa uanze kujifunza,mlishazoweya kusambaratisha vyama vyaupinzani lakini hapo mmegonga mwamba,kama mlitega mtego huo kajipangeni tena.

Mnajua habari za Makamba kununua tawi la Urusi Kigoma? mil 15 tulikula na baada ya hapo tukahamisha tawi pembeni!
 
ikifika december bado zito kabwe hajafukuzwa ndani ya chadema ntarudisha kadi yangu kwa hiari...nikiwa kama mwanachama wa kawaida sana, nasikitiswa sana na jinsi kijana huyu anavyohujumu mipango na mikakati ya chama, zito ni mbinafsi, msiri, mchochezi, mpika majungu na M-CCM pia...anamatukio ya ajabu ajabu sana..SHAME ON ZITO ZUBERI KABWE.
Hoja hovyo kabisa, vijana kama zitto wana dammu yao ndani ya CDM. Kinacohitajika ni hekima, busara, uvumilivu, na hasa kuelewa hawa bado ni vijana. Na perception za binadamu zinatofautiana. Zitto atakomaa tu, kwanza ngoja aoe utaona.
 
THE GUY LOOKED AS COOL AS A LION IN A ZOO THROUGHOUT THE MEETING....
attachment.php

IN FACT HE SAT ON THE HIGH TABLE ITSELF! HOW DO YOU CHASE SOMEBODY FROM THE HIGHTABLE BEATS ME.....
attachment.php

THERE WERE NO SIGNS OF YOUR ALLEGATIONS...I WAS THERE MR INFORMER!



 
Ndio maana huwa namkubali sana MBOWE...palipo na MBOWE hapaharibiki jambo...safi sana...ZITTO is there to stay...magamba tafuteni kwingine kwa kutokea.......
 
we unafata matendo ya mtu!au matendo ya chama!

chama makini ni kile kinachowachukulia watu hatua bila kujali wadhifa, rangi au tabaka, na CHADEMA imekua makini katika kutekeleza hayo ispokua tu inapofika kwa Zitto. Je ni kweli kuwa hufahamu ni jinsi gani Zitto amekua akifanya mambo yake kinyume kabisa na misingi ya chama. Sasa kama chama kikianza kuwa na matabaka hasa katika kuchukua maamuzi hatutakua tofauti na CCM waliowafunga kima Farijala Hussein na kuwaacha KAGODA, au wanaposhinwa kuwashughulikia magamba aka mapacha watatu. Huoni kuwa misingi ya chama hapo itaanza kuwa ya kiupendeleo? hasa pale viongozi wa chini wanapowajibiswa kwa adhabu kali kali ikiwemo kufukuzwa uanachama, lakini huyu bwana haguswi? yeye ni nani?

kwa misingi hii ntarudisha kadi
 
Mpango mwingine wa kuisambaratisha CDM wakwama tena.walitegemea watumie
suala la ZZK kuisambaratisha CHADEMA.Hiki ni chama makini hakiyumbishwi kirahisi
hivyo,hayo yote bado yako under control"
 
Kichwa cha habari kingekaa hivi:

Zitto na shibuda chupuchupu kutimuliwa CHADEMA!

mpango wa kumtimua JOHN SHIBUDA haujaelezwa ni nini kilichojiri kwa upande wake, Baraza lilijadili au halikumjadili Shibuda?
 
Dunia haina siri ipo siku ukweli utagundulika tu, na naomba Mungu igundulike angali CHADEMA ikiwa hai na mpinzani mkuu
 
Hoja hovyo kabisa, vijana kama zitto wana dammu yao ndani ya CDM. Kinacohitajika ni hekima, busara, uvumilivu, na hasa kuelewa hawa bado ni vijana. Na perception za binadamu zinatofautiana. Zitto atakomaa tu, kwanza ngoja aoe utaona.

Acha ushabiki mkuu....Kama ni busara na uvumilivu basi vitumike kwa usawa na haki na kwa kila mwanachama..kwani hao waliofukuzwa hawakustahili huo uvumilivu??nina sababu lukuki zinazonifanya nishangae haya maamuzi ya kiupendeleo yaliyoanza kutawala vikao vya chama.Je ni nani ambaye hana damu ya chama ndani yake?? tutajie kama unawajua??Kimsingi sikubaliani na jinsi chama kinavyobeza hoja ya zito kuchukuliwa hatua...huu ni muda wa kujiandaa kuchukua nchi na si muda wa kuwavumilia wasaliti na waleta utata
 
ikifika december bado zito kabwe hajafukuzwa ndani ya chadema ntarudisha kadi yangu kwa hiari...nikiwa kama mwanachama wa kawaida sana, nasikitiswa sana na jinsi kijana huyu anavyohujumu mipango na mikakati ya chama, zito ni mbinafsi, msiri, mchochezi, mpika majungu na M-CCM pia...anamatukio ya ajabu ajabu sana..SHAME ON ZITO ZUBERI KABWE.

Mie nilidhan ungehoji Busara ya Mbowe kukataa pendekezo la mjumbe mmoja alotaka Zitto apewe fursa ya kusomewa mashtaka then nae ajitee!
 
Adui mkuu wa CHADEMA ni wezi wa rasilimali, CCM ... ngoja waanze na hawa mchwa wa maisha bora kwa Mtanganyika then mamluki watamalizana nao taratibu!
 
Kwa nini MBOWE hakutoa fursa kwa ZITTO kujitetea kuhusu kashfa hizo???? alikuwa anamlinda ZITTO au Chama?
 
Back
Top Bottom