Zitto: CAG hajasema pesa zimeibwa bali zimetumika (kuliwa) hazionekani zimetumikaje, zimekwenda wapi ila zimetumika

Hii clip inanikumbusha ile ya pesa za Uma mwingine si zauma..Tena kuna za uma na zingine sio
Baadaye Rumpango
 
Zito kama hujaelewa muulize CAG mwenyewe ueleweshwe, yani mpaka aliyeandika hiyo report unamuona hajui alichoandika kuhusu report yake.
Nachoona Zito kachoka na siasa anataka kujifungisha magerezani, nadhani ana stress fulani
Akili za KLF COMBINATION.
 
Swali fikirishi. Kwann spika haundi kamati ya bunge kuchunguza hii pesa ilipo??? Lengo kumsaidia mh.Raisi ktk kubambana na ufisadi
 
Hili jambo wanavyozidi kuliziba linafukua makaburi mengine tuliyajua hayo ya billion 252? Bora kukaa kimya tu huyu kakamatika
Mbona hili lilikuwepo na tumekuwa tukilisema humu toka enzi hizo!!! Magufuli ni jizi kubwa. Ni JAMBAZI LA KUTISHA. Ni masikitiko kwamba watanzania wengi ni 0 brain!! Vinginevyo, Magufuli alipaswa kuwa jela na siyo Ikulu. Hili jiwe kila lilipopita lilifanya ujambazi: ujenzi, uvuvi na sasa Ikulu.
 
Zito anakuja na version mpya kila baada ya siku; asituchoshe;

Mara ya kwanza alisema zimepotea;

Leo anasema zimeliwa:

Kesho atatuambia Zimejila;

Anafikiri yeye pekee ndiye mwenye masikio ya kusikia alichosema CAG?? Ili atutafsirie??

Atuache.
Acheni kutema Omo onyesheni zililipo
BIL 1,500
 
Mbona hili lilikuwepo na tumekuwa tukilisema humu toka enzi hizo!!! Magufuli ni jizi kubwa. Ni JAMBAZI LA KUTISHA. Ni masikitiko kwamba watanzania wengi ni 0 brain!! Vinginevyo, Magufuli alipaswa kuwa jela na siyo Ikulu. Hili jiwe kila lilipopita lilifanya ujambazi: ujenzi, uvuvi na sasa Ikulu.
Da sikuipata mkuu aisee huyu mtu ni janga kwa kweli
 
View attachment 751093
Watanzania wenzangu,

Kwenye ripoti yake, CAG hajasema popote kuwa TZS 1.5trn zimeibiwa. Alichosema leo Ikulu ndio msimamo wake uliopo kwenye Taarifa yake ukurasa wa 34. Fedha hizo HAZIONEKANI kwenye matumizi ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Ndio maana tunahoji zipo wapi. Tunataka Ukaguzi Maalumu ili kuhakiki majibu ya Serikali na kujua hela zetu zipo wapi. Hilo tu, hakuna lingine.

Vitisho vya hatua za kisheria ni tambo tu za watawala, hazina maana yeyote. Kumsimamisha CAG Ikulu na kumhoji mbele ya Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni kumtisha CAG, ni kinyume na misingi ya Katiba yetu. Ripoti ya CAG ikishakuwa mbele ya Bunge sio Ripoti ya Executive tena. Ni mali ya Bunge. Kama Rais ana majibu aende akayaseme Bungeni mbele ya PAC.

Rais sio wa kumchekea chekea anapovunja misingi ya nchi yetu. Ni lazima ADHIBITIWE na Taasisi za Kikatiba ikiwemo Bunge. Rais leo amekosea. CAG naye amekosea kwenda Ikulu.

Watanzania sikilizeni, mimi nimekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC miaka 8, ninajua kusoma, kuchambua na kutafsiri Taarifa ya CAG. TZS 1.5trn hazina maelezo, hazipo Benki Kuu na Maelezo ya Naibu Waziri Fedha leo ni kujikosha tu.

Nikiwa Mwenyekiti wa PAC, Mwaka 2013 Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli alikutwa na Hoja ya ukaguzi ya TZS 252 bilioni ya ujenzi wa barabara hewa ambayo mpaka sasa haijajibiwa na utaikuta kwenye Hoja za CAG za mwaka 2016/17. Hivyo ni Kawaida yake kutoheshimu sheria za Fedha na kutojibu Hoja za Ukaguzi.

Kama Serikali ina uhakika kabisa hii hoja ya TZS 1.5trn haipo inipeleke mahakamani hata leo. Nitawashinda hata Jaji akiwa mmoja wa majaji wapya walioapishwa leo.

Mimi siogopi. Nitasema UKWELI daima fitina kwangu mwiko.

Zipo wapi TZS 1.5trn?


Soma: Kuapishwa kwa majaji Ikulu: CAG mbele ya Rais Magufuli, akanusha Shilingi trilioni 1.5 kuibwa/kupotea

Tamko la Serikali: Hakuna fedha tasilimu ya shilingi trilioni 1.51 iliyopotea, ni madai ya wasiolitakia mema taifa letu
Zitto hajielewi anahama katika kile anacholenga. Alianza na hoja ya Serikali kutumia pesa bila kupitishwa na Bunge. Hoja hiyo ni dhaifu ameshindwa kusoma sheria ya bajeti inasemaje. Akaja na pesa kuibiwa nayo anaipinga na kusema matumizi. ameshindwa kudadavua vizuri matumizi na mapato ya serikali ikilinganishwa na bajeti iliyopitishwa na Bunge 2016/2017
 
Inavyo onekana huna tofauti na mtu anayeshangilia mbio za mwenge na huwepo wa mwenge.

Zitto anahoji matumizi ya pesa yasiyo rasmi yaliyofanywa na serikali, wewe unaona hana maana!

Watz wengi hatujitambui.
Zitto hajielewi anahama katika kile anacholenga. Alianza na hoja ya Serikali kutumia pesa bila kupitishwa na Bunge. Hoja hiyo ni dhaifu ameshindwa kusoma sheria ya bajeti inasemaje. Akaja na pesa kuibiwa nayo anaipinga na kusema matumizi. ameshindwa kudadavua vizuri matumizi na mapato ya serikali ikilinganishwa na bajeti iliyopitishwa na Bunge 2016/2017
 
Walishindwaje kumpatia CAG hayo maelezo before mpaka akaandika "pesa hizo hazina maelezo"

UKIKUBALIANA NA WANACHOSEMA SERIKALI (CCM) UTAKUWA EMPTY HEADED.
kweli full headed anyway, tusubiri maelezo mnayotaka wawatosheleze...
 
Back
Top Bottom