Zitto azomewa Bukoba

Zitto azomewa Bukoba

Lakuchumpa123

Senior Member
Joined
May 26, 2015
Posts
138
Reaction score
74
Nikiwa hapa Bukoba leo nimehudhuria mkutano wa ACT-Wazalendo katika uwanja wa Mashujaa. Kiongozi mkuu wa chama hicho,niko Zitto Kabwe alikuwa akihutubia.

Awali alianza kueleza sababu za kuondoka CHADEMA, akisema sio kosa kubadilisha jukwaa la siasa. watu walikuwa wakimpigia makofi tu.

Lakini hali ya mkutano ilibadilika na kuwa mbaya pale alipoanza kujisifu kuwa yeye ndiye aliyeagiza hesabu za CHADEMA zikaguliwe na CAG, kisha akaitwa msaliti na kamati kuu ya CHADEMA.

Hapo wananchi waliokuwa uwanjani hapo wakaanza kupiga kelele wakisema 'sio kweli, sio kweli, sio kweli".

Ilibidi Zitto abadilishe mahubiri na kuanza kueleza msimamo wa chama chake. Lakini watu wakawa hawamsikilizi tena. Wengine walisikika wakisema, "kama umekuja hapa eleza ya chama chako, ya CHADEMA uyaache,".

Kama hiyo haitoshi, Zitto akaanza tena majigambo akisema eti alipokuwa bungeni aliiangusha serikali mara tatu, "Hao wanaokuja kunitukana waseme wamefanya nini bungeni" alisema Zitto.

Watu waliendelea kuzomea hadi Zitto akasema, "Kama hamtaki kunisikiliza naondoka zangu,". Watu wakajibu,waliendelea kuzomea " Nendaaa...!

Hata hivyo mkutano umeisha salama.

Kwa kweli Zitto ana kazi ngumu kuijenga ACT-Wazalendo?
 
Kiwanda cha kutengeneza uongo.

"Alikuwa akielezea kuhusu CAG,:mara watu wakasema usiseme kuhusu CDM!!! " CAG siku hizi kawa wa CDM?
 
Aiseee Masikini Zitto inasikitisha zitto leo anazomewa??
 
Last edited by a moderator:
Hebu acha uongo mweupe wewe unadhan kwenye mkutano ulikuwepo wewe tu? mbona hutaj idadi ya waliorudisha kad zenu hizo ?

Mbona husem maandamano aliyofanyiwa??

Nimeamin kwel unafiki mbaya!! ulijua hakuna tunaofatilia eti?
 
Kuzomea ni tabia ya watu waliokosa hoja, chakufanya ni kumuambia awape nafasi ya kumuuliza maswali yanayowachanganya
 
Namshauri Zitto kama anataka kukipaisha chama chake aongee sera za Chama, vinginevyo Watamchinjia mbali, aje huku mwanjelwa tunamsubiri
 
ACT Itapatikana Mwandiga tu soon! Wazalendo huwa hawajitangazi kwani hizi nyimbo zimetukifu! Walikuwepo wale "mitume" wa kupambana na ufisadi wakiongozwa na Mwakyembe & Mzee wa Viwango! Ile vita imekwisha baada ya wale mitume 12 kupewa vyeo i.e Anna lango, Samwel 6, Kyembe, ONdeka na wengine wengi!

Walipanda jukwaa moja hadi jingine wakituambia kuwa wenzao ni mafisadi! Leo Agizo la Chama Tawala Wanakuja kwa mlango wa nyuma na wimbo ule ule uliotuchosha wenye lengo lile lile!

Kiongozi Mkuu ajue kabisa hakuna mtu anayetutuma isipokuwa tumechoshwa na ulaghai wa kutuambia wewe ni msafi, kama ni msafi sisi wenyewe tutakuona siyo hadi utuambie!

Mara nyingine tutawashusha jukwaani kwa mvua ya mawe! Msifikiri Hatuna Akili!
 
Niliona watu wanapiga makelele ckujua kwanin,nilipokaribia niliona kama kuna kuzomewa lakini sikutaka kufuatlia ni kwanini maana nilkuwa napita na nilikuwa na haraka. Hata hivyo kwa zitto kazomewa sehemu nyingi.
 
Namshauri Zitto kama anataka kukipaisha chama chake aongee sera za Chama, vinginevyo Watamchinjia mbali, aje huku mwanjelwa tunamsubiri

Je kwenye wasifu wake ana tabia ya kupokea ushauri au yake ndio anaona yako sahihi?...Hayo yote amejitakia mwenyew
 
watu mnavyo viwanda vya uongo balaa. nawewe unatofauti gani na mafisadi. mimi nilikuwepo mbona hilo sikuliona? wewe tu ndio ulikuwa kwenye huo mkutano?. ukweli ni kwamba mkutano wa zitto leo ulifana na haijawahi pata tokea. kijana anakipawa kikubwa cha kupendwa.
 
Safi sana anafikiri watu wa bukoba ni kama wa mwandiga wala migebuka watu wa bukoba wamesoma wanahtaji fact indeed siyo porojo na majigambo ya kitoto big like.
 
Mbona wanamsikiliza kwa makini....
 

Attachments

  • 1434387635581.jpg
    1434387635581.jpg
    74.2 KB · Views: 1,422
Back
Top Bottom