kama jana mliangalia bunge jioni kuhusu viongoz wa nchi yetu walioficha pesa nje ya nchi,kuna mbunge alisema imefika wakati watanzania washtuke wanapoona mbunge kila siku anatoa mamamillion kwenye kuchangia mambo mbalimbali,alidiriki kusema kwamba hiyo ni pesa chafu ambayo inatumika kujisaficha na skendo za richmond na epa.
alisema kwamba angekua yeye anawajua angewataja live pia akasema yeye ni mtaalamu wa kudetect pesa zilipofichwa na anacho kifaa maalumu hivo kama wamechimbia ndani ya nyumba kuficha pesa atawaumbua.
aliwaambia wabunge wenzake kwamba majimbo yao hayana maji,umeme,barabara,na maisha mabovu ni kwa sababu ya pesa ambazo zimefichwa uswisi na nchi nyingine za ulaya,uarabuni na america.
ninachokiona mimi ni kuwa viongozi wengi walioiba pesa wanajipendekeza sana kwa watu wa dini sababu wameshajua udhaifu wa viongozi wetu wa dini wa kupenda pesa na udanganywa sana na pesa wanazopewa na kusahau kuoji mambo ya msingi na tuhuma wanazousika nazo
jaman pesa ambazo zimefichwa ni pesa nyingi sana asa ukizingatia nchi yetu ni maskini sana,hivo usiwe upepo wa kupita,tunatozwa kodi nyingi sana na uwa zikipanda kila mwaka,na pesa ambazo zinafichwa zinavunja raia moyo wa kulipa kodi.
naomba wananchi wote bila kujali chama tukomae tuwajue walioficha na pesa zirejeshwe tanzania kwa maendeleo ya vizazi vijavyo