Zitto awapasua roho wabunge

Zitto awapasua roho wabunge

Hapa ndipo maumivu ya kichwa huanza taratibu. Nashajiuliza mara nyingi bila jibu, hivi JK alitumia vigezo gani kwa aliowavisha nishani? Ni kigezo kipi alichotumia kwa Bi Kiroboto? Huyu bado ana miaka 4, mambo ndio yanamwendea kombo kiasi hiki. Je, akilazimishwa kujiuzulu mbele ya safari, hiyo nishani atamnyanganya? Kama hatamnyanganya, kwanini hakumpa fisadi mtuhumiwa Lowasa?
 
tokea lianze swala la posho kwa wabunge zitto amekuwa mstari wa mbele kulipinga swala hilo.
so namuombea aendelee na swala hilo la kupinga.
duh nchi hiii...................................
 
Gaijin hujui siasa wewe..........ulikuwa unataka wabunge wote wa cdm watoe matamko?

we fanya kazi ulopewa na max bana. achana na siasa, huziwezi, siasa zinataka majibu, sio maswali, and you are full of questions.

Sikuwa nataka matamko, nilikuwa nataka actions. Zikowapi?
 
huyo aliyetoa pesa ambayo haijafuata taratibu ni nani?? unaona namna pesa yetu walipa kodi inavotumika kiholela hakuna nidhamu ya matumizi kila mtu akijisikia anajiongezea pesa ili mradi ameshika kule kwenye makali!!
 
good to him.
Haitoshi kulalama, je wakati wa majadiliano ya kuongeza posho alipinga kwa kiasi gani?
alikuwa matibabuni india....ishitoshe hii posho imeongezwa bila wabunge kushirikishwa....
ni kama mswada wa katiba mpya ambayo wewe hujashirikishwa but baba riz1 kasaini
 
Alisema hapa nchini, mwalimu hulipwa mshahara usiozidi Sh. 150,000 kwa mwezi, lakini katika kikao kimoja cha siku hata kama hatazungumza kitu, mbunge analipwa Sh. 300,000."Kama huoni kitu hapo, lazima unahitaji maombi," alisema Zitto
FJM, nilidhani Mh/ndg Zitto kawa daktari bingwa wa upasuaji "roho" :lol:

On a serious note tho, Zitto is a very smart politician, naona kama anajibu kina EL ambao walianzia misikitini,Zitto naona ameanzia kanisani...

BTW does he have "presidential ambitions"?
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mh. Zitto kwa hili kula TANO za amani kwa watz. Ama kweli nchi hii haina dereva watu wakishakuwa na vimadaraka bas9 wanaamua watakavyo hii ndo iliyomkuta mkubwa Makinda Anne kwa kuamua kuongeza posho na kuwawekea wabunge bila hata mjadala wao na bila idhini ya mwenye mamlaka husika tayari kashazitupia kwenye akaunt za wabunge hapa ujue kuna zengwe wanajaribu kulifunika sio bure. Imefika wakati viongozi wetu waone aibu kwa uwajibikaji wao mbovu na wachukue uamuzi mgumu kwa misingi ya uwajibikaji kama anavyowaambia Mh. Lowasa.
 
naomba JK saini ili wabunge waendelee kula nchi! Shida na ukosefu wa huduma kwa wananchi vikiongezeka ndipo ukombozi wa pili unakuja! Zito mbona unawazindua? hakuna ukombozi usio na kafara!
 
Huyo bibi kiroboto ni kilaza sana,anatakiwa ajiuzulu kwani kazi imemshinda na ameonyesha udhaifu mkubwa sana kua ni mkurupukaji na hato weza fikia kiwango cha samwel sita.hivi kanuni anazijua kweli kweli au ndio kubweteka na hiyo nafasi aliyozawadiwa?ZITO KABWE ni sayari nyingine very criative na huwa anasimamia upande wenye ukweli.big up ZITO.
 
Waheshimiwa miungu watu wemepiga posho ambayo haijaidhinishwa wamenyamaza kimyaaaa kama hawapo vile!Kifupu ni kwamba wamekula haramu.Hofu yangu ni kwa JK.Kama hajasaini basi na asisaini kabisa.Isije ikawa anasubiri watu tusahau kidogo halafu asaini.
 
............Alisema hapa nchini, mwalimu hulipwa mshahara usiozidi Sh. 150,000 kwa mwezi, lakini katika kikao kimoja cha siku hata kama hatazungumza kitu, mbunge analipwa Sh. 300,000."Kama huoni kitu hapo, lazima unahitaji maombi,"

Zitto big up endelea .
Pa kukukosoa tutakusoa lakini kwa hili la posho ni wewe pekeee ndio umekuwa sauti ya wa wananchi .
 
ni vizuri tukamsuport zitto katika hili,huku ni kujihalalishia ufujaji wa mali ya umma
 
Upinzani dhidi ya nyongeza ya posho za vikao vya wabunge, umechukua sura mpya, baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, kuibuka na madai mapya akiitaka serikali kuwaamuru wabunge wote waliolipwa nyongeza hiyo, kuzirejesha mara moja kwa vile bado hazijaidhinishwa na Rais.

Zitto aliibua madai hayo mapya alipokuwa akihutubia katika Harambee ya Sikukuu ya Mavuno-2011 iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Nikolao na Mashahidi wa Afrika-Ilala, la Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam. “Nadhani Mheshimiwa Rais amesikia kilio cha wananchi wake, asiidhinishe nyongeza hiyo ya posho na wale waliolipwa bila kuidhinishwa, waamrishwe kuzirejesha,” alisema Zitto.

Kwa mujibu wa Spika Makinda, posho za wabunge zilipanda mwishoni mwa Mkutano wa Nne wa Bunge, ambapo wabunge walilipwa posho hizo mpya katika vikao vya Novemba 8, 9 na 11, mwaka huu. Hata hivyo, Zitto alisema sababu ya kuongeza posho inayotolewa na serikali haina msingi. “Kwani hali gani ya Mtanzania ni nzuri,” alihoji Zitto na kushangiliwa na umati mkubwa wa waumini waliofurika katika harambee hiyo.

Alisema hapa nchini, mwalimu hulipwa mshahara usiozidi Sh. 150,000 kwa mwezi, lakini katika kikao kimoja cha siku hata kama hatazungumza kitu, mbunge analipwa Sh. 300,000.“Kama huoni kitu hapo, lazima unahitaji maombi,” alisema Zitto, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Harambee hiyo ililenga kukusanya Sh. milioni 40 kwa ajili ya kuchangia gharama za kuezeka madarasa mawili ya shule ya awali ya Mwidu, iliyoko Chalinze, wilaya ya Bagamoyo, mkoni Pwani, ukarabati wa kanisa hilo, nyumba za watumishi na mazingira yanayolizunguka. Zitto aliahidi kuchangia Sh. milioni 13, mifuko 250 ya saruji na mabati 200 kupitia marafiki zake.

Source:IPPMedia.

Hapo kwenye red: nafurahi kwamba Zitto kawa muwazi na naamini atakubaliana na mimi nikisema wakati umefika sasa kwa bunge kuweka sheria itakayomlazimisha kiongozi yoyote wa umma including mbunge kuweka wazi kila donation wanayopata/kutoa ili kuondoa mianya ya rushwa! Pia hii itapunguza nguvu ya ma-lobbyists wanaochochea upindashaji wa sheria.

Zitto anajua sana kufanya siasa.....

 
Back
Top Bottom