Upinzani dhidi ya nyongeza ya posho za vikao vya wabunge, umechukua sura mpya, baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, kuibuka na madai mapya akiitaka serikali kuwaamuru wabunge wote waliolipwa nyongeza hiyo, kuzirejesha mara moja kwa vile bado hazijaidhinishwa na Rais.
Zitto aliibua madai hayo mapya alipokuwa akihutubia katika Harambee ya Sikukuu ya Mavuno-2011 iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Nikolao na Mashahidi wa Afrika-Ilala, la Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam. Nadhani Mheshimiwa Rais amesikia kilio cha wananchi wake, asiidhinishe nyongeza hiyo ya posho na wale waliolipwa bila kuidhinishwa, waamrishwe kuzirejesha, alisema Zitto.
Kwa mujibu wa Spika Makinda, posho za wabunge zilipanda mwishoni mwa Mkutano wa Nne wa Bunge, ambapo wabunge walilipwa posho hizo mpya katika vikao vya Novemba 8, 9 na 11, mwaka huu. Hata hivyo, Zitto alisema sababu ya kuongeza posho inayotolewa na serikali haina msingi. Kwani hali gani ya Mtanzania ni nzuri, alihoji Zitto na kushangiliwa na umati mkubwa wa waumini waliofurika katika harambee hiyo.
Alisema hapa nchini, mwalimu hulipwa mshahara usiozidi Sh. 150,000 kwa mwezi, lakini katika kikao kimoja cha siku hata kama hatazungumza kitu, mbunge analipwa Sh. 300,000.Kama huoni kitu hapo, lazima unahitaji maombi, alisema Zitto, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
Harambee hiyo ililenga kukusanya Sh. milioni 40 kwa ajili ya kuchangia gharama za kuezeka madarasa mawili ya shule ya awali ya Mwidu, iliyoko Chalinze, wilaya ya Bagamoyo, mkoni Pwani, ukarabati wa kanisa hilo, nyumba za watumishi na mazingira yanayolizunguka. Zitto aliahidi kuchangia Sh. milioni 13, mifuko 250 ya saruji na mabati 200 kupitia marafiki zake.
Source:IPPMedia.
Hapo kwenye red: nafurahi kwamba Zitto kawa muwazi na naamini atakubaliana na mimi nikisema wakati umefika sasa kwa bunge kuweka sheria itakayomlazimisha kiongozi yoyote wa umma including mbunge kuweka wazi kila donation wanayopata/kutoa ili kuondoa mianya ya rushwa! Pia hii itapunguza nguvu ya ma-lobbyists wanaochochea upindashaji wa sheria.