Elections 2010 Zitto atoa siku saba kwa Waziri

Huyo ndo mh.zitto! Msimamo unao ila sijui unachemka nini mpaka wananchi wanakuwa na wasiwasi. Zitto tetea haki ya wananchi mpaka kieleweke,usikubali ccm waongeze madiwani mamluki kama kule Arusha. Cdm ni imara,jenga chama,utaheshiwa!
 
Zitoa wembe ni ule ule usikubali kamwe kuburuzwa na hao wasioendeleza taifa kwa miaka hamsini na bado wangangania kuiongoza taifa sijui kwa maslahi ya nani?
 
Lakini hayo maneno yanatoka moyoni kwa zito ambaye alianza kupoteza umaarufu sa anayaka kuurudisha kwa nguvu? Cjui ngoja tuone hiyo hatua atakayochukua baada ya cku saba.
 
Monday, 27 December 2010
Anthony Kayanda, Kigoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), George Mkuchika, amepewa siku saba kuhakikisha anaitisha uchaguzi wa kumchagua Meya wa Halmashauri ya Manispaa Kigoma-Ujiji aliouahirisha, licha ya Mahakama kuamua ufanyike siku uliopangwa rasmi.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alipokuwa akihutubia Wananchi wa Kigoma mjini kuelezea mambo mbalimbali yanayohusiana na mustakabali wa kisiasa, ambapo alimshutumu Waziri huyo kwa kutumia Mamlaka yake vibaya.

‘Chadema tuna idadi kubwa ya madiwani zaidi ya CCM, hivyo juhudi zozote zinazofanywa na Waziri kusaidia Chama chake hazitasaidia kitu, badala yake zitaongeza hasira na chuki kwa Wakazi wa Kigoma mjini na kujikuta wakiichukia zaidi CCM na viongozi wake kwa vile anachangia kukwamisha maendeleo ya mji wetu' alieleza Zitto.

‘Kutokana na hali hiyo, nampa Waziri wa Tamisemi siku saba ahakikishe anaitisha uchaguzi wa kumchagua Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ili tumpate Mwenyekiti wa baraza la madiwani na kamati zake za kudumu waanze kutuhudumia na kusimamia miradi ya maendeleo, kwa sababu kadri Waziri anavyochelewesha uchaguzi ndivyo Watendaji wanavyoweza kutumia vibaya nafasi hiyo kuharibu Halmashauri yetu" aliongeza.

Alisema baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu, Chadema walishinda nafasi za madiwani katika Kata 10 dhidi ya tisa walizopata CCM, jambo lililofanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa nafasi nne za madiwani wa Viti Maalumu wakati CCM walipewa nafasi tatu za Madiwani wa Viti maalumu.

Zitto alisema chanzo cha mgogoro huo ni idadi hiyo ya madiwani wa Viti maalumu ambapo alidai kuwa CCM walikwenda Mahakama ya Wilaya Kigoma kulalamikia mgawo huo, lakini Mahakama ilitupilia mbali shauri hilo.

‘Waziri Mkuchika anapaswa kujua kwamba siku ile alipoandika barua ya kusimamisha uchaguzi wa Meya (Desemba 17, 2010), Mahakama ya Wilaya Kigoma ilikuwa imetoa maamuzi ya shauri la CCM waliotaka Mahakama isimamishe uchaguzi, lakini Hakimu alilitupilia mbali shauri hilo kwa maelezo kwamba Tume ya Uchaguzi ipo sahihi katika mgawanyo wa madiwani wa viti maalumu" alifafanua Zitto.

‘Na hata kama Mahakama ingesema okay, CCM waongeongezewa diwani mmoja ili tulingane nao bado wasingekuwa na uwezo wa kushinda halmashauri, labda ile ndoa ya Mseto tuliyofunga nao mwaka 2005 inaonekana wameridhika nayo ndiyo maana wanataka turudiane nao, sisi tunasema kwa hilo hatupo tayari na kamwe mwaka huu hatuipotezi Manispaa ya Kigoma Ujiji' alisisitiza.


ZItto NI NANI MPAKA AMUAMURU WAZIRI?AMEPATA WAPI HAYO MAMLAKA? NANI ANAEMSIKILIZA HUYU?

KWAKO DOGO ZITTO LINDA MDOMO WAKO,SIO SAWA KUMKARIPIA NA KUMPA AMRI WAZIRI WEWE NI MBUNGE TUU TENA WA UPINZANI NA USIEAMINIKA HATA KWENYE CHAMA CHAKO

TAFADHALI KAA KIMYA NENDA ARUSHA JIUNGE NA NDUGU ZETU HUKO KUANDAA MAZISHI YA MASHUJAA WETU ,

KWA KWELI KWA SASA HATUKUAMINI TENA ZITTO TUNATAKA HELA ZAKO LAKINI HATUTAKI USHIRIKIANO NA WEWE TENA USIDHUBUTU KUTOA MATAMKO YA CHAMA TAFADHALI KAA MBALI NA CHAMA CHETU TUKUFU CHADEMA
 
Back
Top Bottom