Zitto atoa siku saba kwa Waziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto atoa siku saba kwa Waziri

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Monday, 27 December 2010
  Anthony Kayanda, Kigoma

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), George Mkuchika, amepewa siku saba kuhakikisha anaitisha uchaguzi wa kumchagua Meya wa Halmashauri ya Manispaa Kigoma-Ujiji aliouahirisha, licha ya Mahakama kuamua ufanyike siku uliopangwa rasmi.


  Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alipokuwa akihutubia Wananchi wa Kigoma mjini kuelezea mambo mbalimbali yanayohusiana na mustakabali wa kisiasa, ambapo alimshutumu Waziri huyo kwa kutumia Mamlaka yake vibaya.

  ‘Chadema tuna idadi kubwa ya madiwani zaidi ya CCM, hivyo juhudi zozote zinazofanywa na Waziri kusaidia Chama chake hazitasaidia kitu, badala yake zitaongeza hasira na chuki kwa Wakazi wa Kigoma mjini na kujikuta wakiichukia zaidi CCM na viongozi wake kwa vile anachangia kukwamisha maendeleo ya mji wetu’ alieleza Zitto.

  ‘Kutokana na hali hiyo, nampa Waziri wa Tamisemi siku saba ahakikishe anaitisha uchaguzi wa kumchagua Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ili tumpate Mwenyekiti wa baraza la madiwani na kamati zake za kudumu waanze kutuhudumia na kusimamia miradi ya maendeleo, kwa sababu kadri Waziri anavyochelewesha uchaguzi ndivyo Watendaji wanavyoweza kutumia vibaya nafasi hiyo kuharibu Halmashauri yetu” aliongeza.

  Alisema baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu, Chadema walishinda nafasi za madiwani katika Kata 10 dhidi ya tisa walizopata CCM, jambo lililofanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa nafasi nne za madiwani wa Viti Maalumu wakati CCM walipewa nafasi tatu za Madiwani wa Viti maalumu.

  Zitto alisema chanzo cha mgogoro huo ni idadi hiyo ya madiwani wa Viti maalumu ambapo alidai kuwa CCM walikwenda Mahakama ya Wilaya Kigoma kulalamikia mgawo huo, lakini Mahakama ilitupilia mbali shauri hilo.

  ‘Waziri Mkuchika anapaswa kujua kwamba siku ile alipoandika barua ya kusimamisha uchaguzi wa Meya (Desemba 17, 2010), Mahakama ya Wilaya Kigoma ilikuwa imetoa maamuzi ya shauri la CCM waliotaka Mahakama isimamishe uchaguzi, lakini Hakimu alilitupilia mbali shauri hilo kwa maelezo kwamba Tume ya Uchaguzi ipo sahihi katika mgawanyo wa madiwani wa viti maalumu” alifafanua Zitto.

  ‘Na hata kama Mahakama ingesema okay, CCM waongeongezewa diwani mmoja ili tulingane nao bado wasingekuwa na uwezo wa kushinda halmashauri, labda ile ndoa ya Mseto tuliyofunga nao mwaka 2005 inaonekana wameridhika nayo ndiyo maana wanataka turudiane nao, sisi tunasema kwa hilo hatupo tayari na kamwe mwaka huu hatuipotezi Manispaa ya Kigoma Ujiji’ alisisitiza.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Hivi Mkuchika anaishi dunia ipi ambayo inapingana na nguvu ya raia waliomweka yeye hapo alipo?
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  These manouvres are a recipe for unnecessary chaos. We should be more sensible and let the will of the people prevail lest we plunge this contrary into chaos or violence.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Zitto, hapo imekaa sawa maana ni suala la kudaihaki ya wananchi / Umma wa Tanzania kupata uwakilishi wao stahiki.

  Kwa nafasi yako hiyo hiyo ya Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, sogeza mkono wako kidogo ukajumuishe na halmashauri zile nyinginezo tata nchini tupate matokeo mapema.

  Nasikitika kwamba mwaka huu nilikua nalazimika kutofautiana na wewe katika maswala mengi sana sana, ila bila chuki. Na hata kesho mienendo isipokua ni ya kupigania umma na kujenga teamwork katika chama nako bado utarajie kwamba mimi na wewe bado tutakwaruzana tu licha ya urafiki wetu wa siku nyingi.

  Hata hivyo, mwakani jitahidi sana ku-Reclaim the Ziitto that we had always known to be standing out steadfast in you full stop.

  Vile vile anza kuiwekea mikakati murua ule mswada wa Mhe Mnyika kuhusu KATIBA MPYA kule bungeni Dodoma.
   
 5. Abraham

  Abraham Senior Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapo umeongea sasa ...achana na migogoro ya chama badilika na anza kujenga chama upya usisikilize waandishi wa habari sana watakupoteza
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yeye ametumwa tu, ni kama andengenye na chitanda arusha, kila sehemu wapo.... wanatekeleza amri ya mkuu wao na wao kama wanajeshi nadhani unaelewa huwa wanatekeleza then kuhoji badae
   
 7. n

  niweze JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Zitto Amerudi Sehemu Yake au ni Vipi?
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Zitto unaona aina ya maswali ambayo vijana wenzako huwa tunajiuliza huku vijiweni. Mimi binafsi sihitaji ukaninunulie hata chupa ya fanta lakini uwe tu mtu wa kuaminika mbele ya jamii yako basi!!!!
   
 9. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mbona wabunge wengine wana zuiwa kuongea na wananchi lakini zito kila mara anaruhusiwa bila tatizo?
   
 10. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Zitto, Ztto, Zitto...
   
 11. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu huyu Mkuchika ndie aliyekuwa waziri wa habari na michezo serikali ilopita. Huyu jamaa ni mtata saana, siku zote yupo katika kulinda maslahi ya CCM. Kumbuka aliwahi kususiwa na waandishi wa habari hasa baada ya kuzua bifu nao, na waandishi wakaamua kumweka kolokoloni (kwa kutandika habari zake ) Sijui kama adhabu ile iliisha, mimi naamini huyu jamaa BADO anastahiri ile adhabu
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hongera sana Zitto kawa sasa unanifurahisha sana,ni lazima uwe mwanasiasa mwenye msimamo.Naona CCM wanataka vurugu zisizokuwa za lazima!!!
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu mbona umeongea kitu kipya kabisa?ni mbunge yupi aliyekatazwa kuongea na wananchi!!
   
 14. GWeLa 2003

  GWeLa 2003 Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  viongozi wetu hawa (product ya CCM) kama alivyowahi kunukuliwa chenge kipindi cha Uspika.. inatakiwa kulinda maslahi ya chama na siyo ya wananchi..na ndio maana si shangai kuona mkuchikaakisindwa kutatua ssuala la Umeya kigoma...na kingine selikeli ilishaona ya kuwa raia wake hawana akilindio maana inafanya maamuzi tata..tukisema tz ni nchi ya kiimla nani atapinga? ... ni kigezo gani kilichotumika kuwapa madiwani wa3 ccm wa viti maalum kati ya nafasi hizo nne..yote kwa yote hali hii itaisha, tunachotaka ni katiba mpya
   
 15. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160

  Hauna taarifa ni Naibu Katibu Mkuu
   
 16. n

  nyantella JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Crap!!
  Asipoitisha atafanya nini? asitishie watu nyau!!!
   
 17. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #17
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  lakini nawewe mkuchikaaaaaaa soma alama za nyakati waziri,huu wakati tulionao ni tofauti sana na enzi zenu,watu wamebadilika na wana hasila kweli,wape haki yao,kwa hilo hatuko nawe juu ya hilo kwani tunahitaji maendeleo na wala sio longolongo


  mapinduziiiii daimaaaaaaa
   
 18. P

  Penguine JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Mkuchika unataka KUKUCHIKA kila kitu eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee katika siasa?
   
 19. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili
   
 20. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  ????????
   
Loading...