Zitto, Arfi, Shibuda kujadiliwa Kamati Kuu...

KAMA ilivyotarajiwa na wengi, mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe amevuliwa wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, lakini chama hicho 'kikapigwa jeki' baada ya mfanyabiashara maarufu, Mustafa Sabodo kukipa Sh150 milioni kwa ajili ya kujenga chuo cha maadili ya uongozi.
Matukio hayo mawili pia yaliambatana na kuugua ghafla kwa Zitto na makamu mwenyekiti wa Chadema, Said Amur Arfi ambao wamelazwa Hospitali ya Aga Khan kwa matatizo tofauti.

Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zinasema kuwa Zitto, ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chadema, alipigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na wabunge wa chama hicho kwenye mkutano wao uliofanyika juzi mjini Bagamoyo.
Hadi jana, hakuna kiongozi yeyote wa Chadema aliyepatikana kuzungumzia hatua hiyo, lakini wabunge waliohudhuria semina mjini Bagamoyo na ambao hawakutaka majina yao yatajwe, walisema kura hiyo ilipigwa baada ya kujadili kitendo chachake cha kupinga uamuzi wake wa wenzake kumsusia Rais Jakaya Kikwete wakati akitoa hotuba ya kuzindua Bunge la Kumi.

Pia wabunge hao walimtaka Zitto ajieleze kutokana na kitendo chake cha kupinga uamuzi wa pamoja wa kumsusia Rais Kikwete.
Uamuzi wa wabunge hao kumvua uongozi ulikuwa ukitarajiwa na wengi baada ya Zitto kupinga hadharani kitendo cha wenzake cha kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kuhutubia kuonyesha kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais na kushinikiza kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.

Uamuzi wa kumsusia Kikwete ulifikiwa na wabunge hao baada ya mjadala mrefu ulioisha kwa kupiga kura. Zitto na wenzake tisa hawakuingia ndani ya ukumbi wa Bunge siku Kikwete alipokuwa akihutubia na baadaye kuitisha mkutano na waandishi wa habari kueleza kupinga kitendo cha wenzake.

Baada ya Zitto na wenzake kutoingia kwenye ukumbi wa Bunge ili watekeleze uamuzi wa kutoka nje wakati Rais Kikwete akianza kuhutubia, katibu mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema waliosusia uamuzi hao wangechukuliwa hatua na kamati ya wabunge.

Baadaye mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu alitangaza kumwandikia barua Zitto na wabunge wengine tisa ambao hawakuingia kwenye ukumbi wa Bunge siku ya uzinduzi, kuwataka wajieleze kwa kuwa walichofanya ni utovu wa nidhamu.
Wakati taarifa hizo za kuvuliwa uongozi wa Zitto zikibainika, mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alilazwa tangu juzi saa 3:00 usiku kwenye Hospitali ya Aga Khan katika kipindi ambacho gazeti moja la kila siku limeripoti kuwepo kwa mpango wa kumuua.

Taarifa zinasema Zitto amelzwa wodi namba 57 iliyo ghorofa ya tatu na tayari amechukuliwa vipimo vyote ingawa madaktari wamesema hawakuona tatizo na kwamba wanasubiri kipimo kikubwa.
Akizungumza na gazeti hili akiwa hospitalini, Zitto aliwataka Watanzania kutokuwa na hofu na kuugua kwake kwa kuwa ni ugonjwa wa kawaida akiwataka wamuombee apone haraka.
"Watanzania wasiwe na wasiwasi na kuugua kwangu. Hii ni kawaida tu, madaktari wananipa matibabu niombeeni nipone haraka," alisema Zitto.

Alipoulizwa kuhusu mkutano huo, Zitto alisema hawezi kueleza lolote kwa kuwa alipata nafasi ya kuhudhuria siku moja kati ya mbili za mkutano huo.
Wabunge wengine wa Chadema, Lucy Owenya na John Shibuda walifika hospitalini hapo jana kumjulia hali Zitto ambaye alijijengea umaarufu katika Bunge la Tisa kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja.
Zitto amekuwa akionekana kuwa na mwenendo tofauti na mwenyekiti wake Freeman Mbowe. Wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho mwaka jana, Zitto alitangaza kugombea uenyekiti, uamuzi ambao ungempambanisha na Mbowe, lakini wazee wa chama hicho walimwita na kumshauri aondoe jina lake.

Chaguzi za umoja wa vijana wa chama hicho na baraza la wanawake pia ziliibua makundi yaliyoripotiwa kuwa ni ya wafuasi wa Zitto na Mbowe na chaguzi hizo zilivurugika na kuahirishwa.
Mara baada ya Chadema kuingiza wabunge wengi na hivyo kunyakua haki ya kuunda kambi ya upinzani, Zitto alitangaza kugombea uongozi wa kambi hiyo bungeni, lakini baadaye Mbowe alipewa nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine, makamu mwenyekiti wa Chadema, Said Amur Arfi naye amelazwa wodi namba 29 iliyo ghorofa ya pili kwenye hospitali hiyo na habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Arfi anasumbuliwa na matatizo ya kibofu cha mkojo.
Hata hivyo, jitihada za Mwananchi kutaka kuonana na kuzungumza na Arfi hazikufanikiwa jana.
Hata hivyo, Chadema ilipata ahueni baada ya Sabodo kuamua kuipa Sh150 milioni ili ifanikishe azma yake ya kujenga chuo cha maadili ya uongozi kitakachoitwa “Mustafa Sabodo Accademy” na mfanyabiashara huyo, ambaye ni kada wa CCM, akasema ataendelea kukisaidia kwa karibu zaidi chama hicho.

Msaada huo wa Sabodo kwa Chadema ni wa tatu katika kipindi kisichozidi miezi minne baada ya muumini huyo wa siasa za Mwalimu Julius Nyerere kukipatia jumla ya Sh200 milioni kabla na wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Akitoa msaada huo jana kwa viongozi wa Chadema na wabunge, Sabodo alisema kuwa huo ni mwanzo na ataendelea kukisadia chama hicho kwa sababu kimeonyesha nia ya kuleta maendeleo nchini.

Alisema malengo ya elimu ni kufanya vitendo na sio kula pesa kama inavyofahamika kwa wengine, hivyo mchango wake wa elimu ameshautoa kwa chama fulani lakini hakuna maendeleo yoyote zaidi ya kupoteza pesa bure na badala yake yanabaki majengo tu badala.
“Hii si mara ya kwanza kutoa mchango kwa kuwa nimeshatoa kwa chama lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika ila kwa hiki chama kimeonyesha kina malengo mazuri," alisema.

Alisema yeye ni Mtanzania na amezaliwa mkoa wa Lindi hivyo anaamua kuchangia chama chochote chenye kuonyesha lengo la kufanya maendeleo nchini na sio ubabaishaji na kwamba chama bora kinajulikana kwa vitendo si maongezi yasiyokuwa na msingi.
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema chuo hicho kitakuwa ni cha kwanza nchini chenye lengo la kuwapatia mafunzo viongozi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali ili wawe na uwezo wa kusaidia jamii.

“Tuna lengo la kuanzisha chuo cha kuwasaidia viongozi wawe bora na sio bora viongozi hivyo leo hii tunatangaza rasmi ujenzi wa chuo hicho na ndani ya miaka mitano utakuwa umeshakamilika," alisema Mbowe.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo Chadema itaendelea kumuenzi Sabodo kutokana na umuhimu wake katika chama hicho na taifa kwa ujumla, kama wanavyoenziwa viongozi wengine.

Alisema Sabodo huwa haogopi kama walivyo wafanyabiashara wengine ambao huwa wanaogopa kuchangia vyama vya upinzani kwa kuhofia usalama wao kutoka serikalini.

“Kipindi cha uchaguzi nilikuwa nawafuata wafanyabiashara ambao ni rafiki zangu, lakini walikuwa wanashindwa kunipa ushirikiano kwa kuniambia wazi kuwa wanaogopa vitisho vya serikali, lakini nilivyomfuata Mzee Sabodo aisaidie Chadema wakati wa uchaguzi, aliniambia niwaite waandishi wa habari ili umma ufahamu mchango wake kwa jamii,” alisema Mbowe.

Naye katibu mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa alisema leo kamati ya chama itakutana na kujadili gharama hizo na kuziweka wazi kwa vyombo vya habari, ikiwa ni changamoto kwa vyama vingine.

source:mwananchi
 
samahani, wewe ni mh. Pinda? Mbona sasa unakuwa na majibu mafupi tofauti na unavyojielezaga bungeni mh! Hope u are not the 1!

mimi ni babaako kama huamini kamuulize mama yako;nimesema huo upupu hapo juu ni uongo,
 
Kama nimeelewa vizuri ni kwamba zito hakuwepo kwenye hicho kikao so kwa maana hiyo hakujitetea me nadhani angepewa nafasi ya kujitetea kwanza caz chama chetu ni cha kidemocrasia basi apewe hiyo nafasi then tutaamua kutokana na utetezi wake..! this wl be a ridiculous decision if jamaa hatapewa hiyo nafasi...! if and only if this thread is true...!:A S-alert1:
 
chadema hawawezi kumtimua zitto kwa vyovyote,kwa kizazi na wakati tulio nao sasa chadema ni zitto na no zitto no chadema;ukweli ndio huo.

Hicho Ulichokiandika ndicho hata Zitto anachokiamini? Kama ni hivyo basi atakufa kwa Pressure
 
Hakuna kitu kilichoifanya wikendi yangu iwe nzuri kama habari hii..................

Tumekuwa tukimuonya Zitto kwa muda mrefu kuwa asitoe siri za chama hadharani aheshimu demokrasia ya ndani ,lakini hakutusikia sasa he is paying his own price, akubali kuinywa dawa ingawa ni chungu na jifunze uongozi wa pamoja kuwa mnaweza kutofautiana mawazo lakini mnapotoka nje mnatakiwa kuwa kitu kimoja. Kama kiongozi mkuu wa chama huwezi kuongoza chama kwa kutumia FACEBOOK huo ni utoto.

Kuna wana CCM humu na nje ya JF wanaomlilia Zitto nauita ni unafiki ni machozi ya mamba kulia anapoona mwili wa binadamu huku moyoni akichekelea. Kwa tukio hili kuna wana CCM wa aina mbili kwanza wanaofurahia wakidhani tukio hili litazua mgogoro pili kuna wale wanaosikitika kuondoka kwa Zitto kuwa dili lao limefikia mwisho kwa vile walikuwa wanamtumia Zitto kupata habari za ndani za CDM.

Kundi la kwanza ndilo kubwa na wengi wao wanazunguza kishabiki zaidi bila kufikiri kuwa CDM inazidi kujisafisha machoni mwa jamii. Inafuata vikao vya chama, haina kuleana, imedhirisha kuwa CDM si mtu ni system hata akiondoka mmoja haiwezi kuyumba nk.

Kundi la pili ambalo hasa ni la viongozi wakuu wa CCM RA, EL you name it waliokuwa wanamtumia ingawa lengo lao kuu halijatimia lakini karibu watafanikisha lengo jingine la kumuondoa na kumleta kundini mwao waliyekuwa wanadhani wanamuogopa. Na kwa kitendo hicho Zitto atakuwa kwenye himaya yao kama kina Tambwe, Kabouru, Lwamwai, na wengine unaweza kumwongeza Maalim ingawa yeye ni kwa stail nyingine.

Hongera CDM kwa kuliona hili mapema kabla madhara makumbwa hayajajitokeza na hili litakuwa fundisho kwa wengine walioingia CDM kwa nia hiyo.

Tuko pamoja............
 
Chadema wanawaogopa wengi wakiwamo Zitto! Zito ni threat kwa slaa na Mbowe,Slaa amesikika sana akijitapa kuwa Zito hamuwezi yeye kapigiwa kura million 2!!!! The man you hoped to be a president, ikifika wakati wake tutayafunua na Slaa, personally ni archtect wa hii move!

'Hawana Imani Naye' is a political statement it has nothing to do with reality,Zito angekuwa mbaya angekaa kimya kabisa kwa tuhuma zote zilizoelekezwa kwa chadema, alipigania umoja na kusema kila kitu kiko sawa tu kuwaweka wananchi wazidi kuwa na imani na CDM, ambayo ingeporomoka (kama bado) wakikumbuka kifo cha Wangwe.
Waberoya

Kwa wasiokufahamu watafikiri unamwonea huruma Zitto kumbe ni nafiki la kutupwa unauna na kupuliza..... Eti Slaa yuko kwenye move hii umekalia umbea mbea tu kuchonganisha watu. Soma post yako hapa chini haijapita hata mwezi ulituambia Zitto ni hatari kwa demokrasia ndani ya upinzani leo unatuambia eti Zitto hana tatizo, sipendi unafiki wako utawadanganya wengine ambao hawakujui lakini si mimi.

quote_icon.png
Originally Posted by Waberoya

However, we all know JK ni mdini, maana alianza harakati za udini tangu akiwa UDSM miaka hiyo….na hili fuatilieni

Nani anayejua Zitto ana mtambo wa kusaga kokoto na alipata tender ya barabara ku-supply kokoto? Is he defending his interest indirectly?

I mean we should be careful na watu kama Zitto yes they are bright, mmh! But they might be dangerous for the opposition existence. But we should examine him carefully and not judge him. Nimegusia tu swala la uislam maana mpaka leo kuna baadhi ya waislamu wanaofikiri kuwa wanaiweza kuigawa nchi hii kidini, na kuna wakristo wanaofikiri wanaweza kuigawa nchi hii kidini.
 
Hakuna kitu kilichoifanya wikendi yangu iwe nzuri kama habari hii..................

Tumekuwa tukimuonya Zitto kwa muda mrefu kuwa asitoe siri za chama hadharani aheshimu demokrasia ya ndani ,lakini hakutusikia sasa he is paying his own price, akubali kuinywa dawa ingawa ni chungu na jifunze uongozi wa pamoja kuwa mnaweza kutofautiana mawazo lakini mnapotoka nje mnatakiwa kuwa kitu kimoja. Kama kiongozi mkuu wa chama huwezi kuongoza chama kwa kutumia FACEBOOK huo ni utoto.

Kuna wana CCM humu na nje ya JF wanaomlilia Zitto nauita ni unafiki ni machozi ya mamba kulia anapoona mwili wa binadamu huku moyoni akichekelea. Kwa tukio hili kuna wana CCM wa aina mbili kwanza wanaofurahia wakidhani tukio hili litazua mgogoro pili kuna wale wanaosikitika kuondoka kwa Zitto kuwa dili lao limefikia mwisho kwa vile walikuwa wanamtumia Zitto kupata habari za ndani za CDM.

Kundi la kwanza ndilo kubwa na wengi wao wanazunguza kishabiki zaidi bila kufikiri kuwa CDM inazidi kujisafisha machoni mwa jamii. Inafuata vikao vya chama, haina kuleana, imedhirisha kuwa CDM si mtu ni system hata akiondoka mmoja haiwezi kuyumba nk.

Kundi la pili ambalo hasa ni la viongozi wakuu wa CCM RA, EL you name it waliokuwa wanamtumia ingawa lengo lao kuu halijatimia lakini karibu watafanikisha lengo jingine la kumuondoa na kumleta kundini mwao waliyekuwa wanadhani wanamuogopa. Na kwa kitendo hicho Zitto atakuwa kwenye himaya yao kama kina Tambwe, Kabouru, Lwamwai, na wengine unaweza kumwongeza Maalim ingawa yeye ni kwa stail nyingine.

Hongera CDM kwa kuliona hili mapema kabla madhara makumbwa hayajajitokeza na hili litakuwa fundisho kwa wengine walioingia CDM kwa nia hiyo.

Tuko pamoja............

Mkuu,
Chadema inasonga mbele hatua kwa hatua, vikiambatana na umakini mkubwa.
Tuko pamoja mkuu, ni suala la muda pamoja na uvumulivu..magugu yote yatang'olewa na tutabakia na ngano safi.
 
safi safi sana CDM , kwa kutoficha UNAFIKI, SAFI sana , nasema CDM hakitakufa na wala hakitatikisika milele, hongereni CDM kwa uamuzi wa busara
 
Vijana tunamchukia Zitto, kijana aliyefanya kazi na kuvuta vijana wengi Chadema ni John Mnyika, Rais wa tnzania 2025

Hakika unautafuta kwa kasi sana huo ubunge wa viti maalumu mwaka 2015, good job!!
 
Kawaida historia hua inajirudia. Staili ile ile yakumwondosha CHACHA, njia zile zile namna ile ile , bado hatujajifunza. Duuuuu watanzania wenzangu ninani aliyetuloga? KWELI MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO.

WABEROYA
Ulisema kwamba waafrika tuko nyuma sababu ya mazingira, je hii nayo unaichukulia je? yani namna ileile CHACHA walimuondoa wakasema anatumiwa na fisadi RA wamekutana kwenye hoteli fulani nk. baada ya kufariki hawa hawa wakasema Chacha alikuwa jemedali wa demokrasia. Kinachoshangaza zaidi yaliyomsibu Chacha ndo hayohayo yanamwandama Zito.

Mie kwa kweli nashekerea kwa CCM kuchakachua matokeo ya uchaguzi. Amini nakuambiani watanzania mngeteseka sanaaaaaa

Kaka I am speechless!! Haiingii akilini kuwa hamna imani naye kwenye kambi ya upinzani bungeni at the same time ni naibu katibu mkuu wa chadema! logically hata unaibu katibu mkuu wa chadema hawana Imani naye, upo kaka?? Zitto amevuliwa vyeo vyote!

Kama ultimate solution ya chadema ni kufanya hivyo,then what about those 9?? Huoni kuna kamchezo hapo kama ka yule nabii alipouliza wako wapi wale tisa? sikuponya kumi?

Waberoya

Kwa wasiokufahamu watafikiri unamwonea huruma Zitto kumbe ni nafiki la kutupwa unauna na kupuliza..... Eti Slaa yuko kwenye move hii umekalia umbea mbea tu kuchonganisha watu. Soma post yako hapa chini haijapita hata mwezi ulituambia Zitto ni hatari kwa demokrasia ndani ya upinzani leo unatuambia eti Zitto hana tatizo, sipendi unafiki wako utawadanganya wengine ambao hawakujui lakini si mimi.

Quinine,umejaribu kuturnish image yangu humu ndani kwa hiyo article!

Nilikujibu na ninajibu tena, Mimi nampenda Zito na kwangu mimi nimejifunza vitu vingi kwake, nilichoandika ningeandika hata kwa mtuyeyote yule kwani statement zake sikuzielewa na nilispeculate hicho nilichoandika hapa!

Zito alizijibu hizo tuhuma zote. I mean Zote, na moyo wangu ukatulia, lengo la kuweka hiyo article hapa ni kuona mawazo ya wengine ambao wana concrete evidence, lakini sikuona zaidi ya statement za 'I hate you' 'fisadi' Na ulishtuka na unazidi kushtuka unapoona ninampa shavu, ninaangalia GLOBALLY kama mwanamageuzi nchi hii, siangalii chadema.Yes I want CCM to move out but I need qualified people to take over which now we are all proving (me and you) beyond reasonable doubt that CDM is not capable is still far far away to be called chama mbadala, wanaweza kuwa mbadala ila kwa kulingana na CCM!

Una uhuru wa kuniita majina yote, na ujiridhishe nafsi, una uhuru wa kuchafua jina langu la mtu usiyemfahamu physically! what a clever boy!!!

FYI(1) your in my ignored list! najua na wengine wamefanya hivyo, bado haujaijua JF, angalia thread hii nieleze ni JF wangapi waliopinga issue ya Zito kuondolewa uongozini? huwa unawajua?? , unasoma mawazo yao kila siku?? ulikaa at least six month utaijua kuwa kuna great thinkers humu na sio great haters

FYI(2) Akina waberoya wako wengi humu, ila sijaona akina quinine wengi humu!!!! nimeona watu wenye mawazo huru (wengi sio chadema), wenye kukosoa, kutafakari na kuendelea, nilikuwa na hofu-kama fan wa Zito nikaandika, Zito akajibu what else?, issue zote za EPA zilianza kama speculation na watu wakatoa evidence!!

Mwisho, simuoonei huruma Zito kwa kuondolewa uongozini! nawahurumia chadema ambayo wamehehuka na kile wanachokiita mafanikio! ambayo hajayashangaza kwa sasa ,KAMA ANALYST WALIVYOSEMA WHAT MADE CHADEMA TO HAVE MANY MPs is not because they are strong, no no...no....is because CCM had conflicts in particular areas and Slaa was not their choice, ndio maana unakuta mbunge wa chadema na rais wa CCM!!! Ndiyo maana wenye akili wote hawakuamini kuwa chadema wameshinda!

sasa na hii mikikimikiki ndio inawarudisha nyuma na watu(wapiga kura) wanasema 'NDIVYO WALIVYO' FYI(3) tuliwaonya CUF-bara pia!!


Hata wewe leo nitakupinga kwa lile ninaloona tunatofautiana na siku ukitoa point (sijawahi ona) nitakusupport kwa nguvu zote na nitakuondoa kwenye ignore list yangu! at least niheshimu kwa wingi wa post na thanks! ebo! unarudia kitu kilekile for what?
 
Zitto anapaswa aendelee kuifanya kazi yake kwa umakini bila kuyumbishwa na move hii ya watu waoga;

Mwisho wa siku watanzania watawatambua wabunge makini kwa hoja zao na kwa namna walivyotekeleza majukumu yao majimboni na kwa taifa kwa ujumla na kisha hukumu ya haki itafanywa kwa wote mwaka 2015,ila kwa uamuzi huu naanza kupata shaka kuwa tuna wabunge wengi wa term moja ndani ya Chadema.
 
Mkuu,
Chadema inasonga mbele hatua kwa hatua, vikiambatana na umakini mkubwa.
Tuko pamoja mkuu, ni suala la muda pamoja na uvumulivu..magugu yote yatang'olewa na tutabakia na ngano safi.


Chacha wangwe alikuwa gugu? Kafulila alikuwa gugu? Leticia alikuwa gugu? Zito unataka kusemani gugu? kesho yule nanihii ni gugu? mapenzi yenu kwa chama kilichokufa kinawapofua hamuoni ukweli wala kuunusa! haiwezekani wanaume na wanawake wazima wasem hawana imani naye wakati hajafanya kazi yoyote ile! hawakupiga kura kumuweka! na bado same person anaongoza chama kama naibu katibu mkuu. chama gani hakina intelijinsia, hakithibitishi maneno kinato aushauri wote humu JF! nadhani wanshtuka kuona watu wengi wamepinga huo uamuzi in the very same JF!!!
 
chadema hawawezi kumtimua zitto kwa vyovyote,kwa kizazi na wakati tulio nao sasa chadema ni zitto na no zitto no chadema;ukweli ndio huo.

He! tuliona chadema ilivyoanza kushika kasi! ni kipindi kile ambacho misimamo ya zito udsm ikawafanya watu wakitafute chama kiko wapi!!!

ulichosema ni sentensi ndogo sana, Zito angekuwa mroho wa madaraka au vyeo angekuwa mbali kupitia hata CCM!!
 
Ama kweli kila mtu akipata umaarufu kidogo huvimba kichwa. Ningependa kusema ile mesali ya masikini akipata ma...,.,.............
Zitto aliyeaminika na watanzania kwa 100% leo hii anakengeuka au anaonewa?. Zitto unatuangusha na ukae ujiulize unataka kutoka pale ambapo watz wote tunakimbilia sijiu anamawazo ya kwenda sehemu ambayo imekosa mvuto. Zitto nakushauri ujirudi na ulete imani na wanaCDM Kwako maana kiburi si maungwana
 
Kwa sababu umeshatuambia kwamba the reason mlisimamisha ni kwa sababu alitaka kuwapiga, na aliwatukana.

Umetuambia kwamba mlipoenda kwenye mkutano haikuwa kwenye agenda kumtimua Wangwe, mpaka alipoanza ku act up ndani ya mkutano. Vinginevyo angekuwepo leo hii huyo loose cannon madarakani. Na mngemnadi tena Tarime 2010.

Au sio?

Kama sio basi futa maneno yako kwamba agenda siku ile haikuwa kumfukuza!



Kwa nini unam cherry pick Zitto? Mimi nauliza viongozi wengine wa juu kabisa waliomkumbatia, kina Tundu, na Mbowe kabla ya honey moon kuisha na reality ku sink in. Sasa mambo yameharibika mnashindwa kudili nae.

Zitto anadiriki mpaka kusema chama kilikuwa hatarini. Kwa ajili ya loose cannon mmoja ambae mmemlea wenyewe? Mkamuuza kwa wananchi?

Halafu mnadiriki kusema - Tundu Lissu anadiriki kutuambia - kwamba anaenda mahakamani kumtetea huyu mtu ambae yeye Tundu mwenyewe anasema ni mwongo. Mnakuja tena kum-nadi kwa wananchi, na kumdanganya Jaji kuhusu huyu mtu wenu ambae mnatuambia hana integrity? Nyinyi mnaweza ku run Chama kweli nyinyi au ni wazugaji mnaogombanishwa na viruzuku vya laki mbili hapa laki nne pale?



Na kina Tundu Lissu na Mbowe na viongozi wengine nao basi wanafiki manake walimnadi, mlimpromote kiongo ongo, Wamarekani wanasema mlim pimp huyu Wangwe kwetu! Nyote ndumila kuwili. Nyote ma pimp nyinyi!



Sio Chacha kawekwa hadharani.

CHACHA-DEMA nzima imewekwa hadharani!

Mnagombea ruzuku, mnasingiziana eti pesa zilienda hazikwenda mikoani, nilikupa hujanipa, kwani hakuna daftari tuone ankra?

Au ma accountant wenu wana doctor madaftari ya hela? Ni mafisadi? Kuna ufisadi ndani ya CHACHA-DEMA?

Au hamna daftari nyinyi watu?

Kama lipo kwanini kuwe na 'he say she say' ya pesa nilikupa hukunipa?



Siungi wala sipingi mtu. Mimi si shabiki shabiki tu la Chama. Chochote kile.

Nataka ukija na narration of what happened kuhusu aliyetaka kupigwa basi hizo accounts should be substantiated na watu ambao sio hao hao wanaosema walitaka kupigwa!

moja kati ya vitu vigumu kuvitetea duniani ni ukabila,udini au ubaguzi wa aina yeyote ile.japo ubaguzi wa rangi wakati mwingine ni aibu kubwa kuutetea ila hizi aina nyingine za ubaguzi ni ngumu sana.unaweza kujikuta upo tayari hata kujilipua ili kuutetea ukabila au udini...
...UHURU wa YESU ni wa milele

hii nimecopy humu jf...

"CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-
Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.
Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?
Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.
Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?
Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?
Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?
Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.
Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.
Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.
Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha.


Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA?"


kuna kila dalili ya moto kuwaka ndani ya chadema...kama hazitafanyika juhudi za makusudi za kuumaliza mgogoro huu yatakuwa yaleyale ya akina NCCR-Mageuzi na TLP.Cha msingi hapa wanachama wa chadema mliomo humu JF muwashauri viongozi wenu watafute suluhu ya mgogoro huu na dhambi mbaya hapa ni ukabila kuliko hata ufisadi...kama mtaendelea kupigana jihadi ya kutetea hali hali hii kana kwamba hakuna mgogoro ndani ya chadema basi mnakiua hichi chama kilichoanza kujipatia umaarufu nchini hasa tanzania bara.tunajua kule visiwani CUF wapo imara kwa upande wao kule.

Na kina Tundu Lissu na viongozi wengine waliokuwa wana m-promote miaka yote hiyo hawakujua Wangwe ana mdomo mchafu, na mchochea ukabila na mtunga uongo?

Amegeuka ghafla au mlijua siku zote si mwema na mkamnadi anyway?

Mlikuwa mna m-pimp kwa Wananchi?

I miss those days! Kuhani where are you?

Nataka kusema kitu naona mikono inanizuia nisiandike
 
Jamani tuacheni ubishi. Zitto hafai tena CHADEMA! Matendo yake ni ya kisaliti! Kupeleka umbea usalama wa Taifa, kutaka urais, kununuliwa na kina EL & RA, kutoa siri za vikao, kupinga maamuzi ya vikao n.k. Jamani haiitaji even a simple common sense kujua Zitto hafai, yote mazuri aliyofanya haya justify atende mabaya, na mabaya aliyotenda yana erase mazuri yote aliyofanya!

Embu fanya mazuri mengi leo halafu ufanye baya moja ufe leo uone kama utaingia Mbinguni! Zitto kwa upupu aliofanya alistahili aondolewe CHADEMA! Kama angeomba msamaha ndo alitakiwa avuliwe vyeo.
 
Chacha wangwe alikuwa gugu? Kafulila alikuwa gugu? Leticia alikuwa gugu? Zito unataka kusemani gugu? kesho yule nanihii ni gugu? mapenzi yenu kwa chama kilichokufa kinawapofua hamuoni ukweli wala kuunusa! haiwezekani wanaume na wanawake wazima wasem hawana imani naye wakati hajafanya kazi yoyote ile! hawakupiga kura kumuweka! na bado same person anaongoza chama kama naibu katibu mkuu. chama gani hakina intelijinsia, hakithibitishi maneno kinato aushauri wote humu JF! nadhani wanshtuka kuona watu wengi wamepinga huo uamuzi in the very same JF!!!
Eti wengi wamepinga ni wapi hao kina Mwanamageuko sema wewe umepinga, halafu tangu lini ukawa na mawazo hayo kwa Zitto???????? Umebadilika lini au wewe ni kupinga kila move yeyote ya CDM, umesahau juzi uliposema Zitto ni hatari leo kavuliwa cheo unasema CDM wamekosea, nitazidi kukumbusha maneno yako haya hadi utakapoyakana, usiwe ndumila kuwili.

quote_icon.png
Originally Posted by Waberoya

I mean we should be careful na watu kama Zitto yes they are bright, mmh! But they might be dangerous for the opposition existence.
 
Back
Top Bottom