Mheshimiwa Zitto,
kwanza hongera sana kwa kuteuliwa kwako. Hii ni dalili kwamba kazi zako kama mbunge zinathaminiwa na watu wengi hata nje ya nchi yetu.
Ila tu mimi pia nina ushauri, pamoja na kushiriki kwenye tume mbalimbali, weka juhudi zako kubwa kwenye kuendeleza jimbo lako la Kigoma. Mafanikio yako kama mbunge yatakuwa judged na juhudi zako za kuwakomboa wana jimbo lako kuliko kitu kingine chochote.
Ukianza kushiriki hizi tume na kamati mbalimbali ni rahisi mno kujisahau na kukuta jimbo linabaki pale pale.
Mafanikio mema katika shughuli zako.