MKUU WA WAKUU
Member
- Oct 23, 2010
- 18
- 1
kabwe alionesha hali ya masikitiko alipogigwa mabomu na wachakachuaji, alipona madhara baada ya mdogo wake kujitoa mhanga. Kwa nini unadhani ukomavu wa kisiasa ni kuiunga mkono ccm tu? Je mafisadi ni wakomavu wa kisiasa? Wewe ni taahira miongoni mwa mataahira wachache wenye uwezo wa kusoma na kuandika lakini hawana uwezo wa kutathminini wanachokiandika.
utumbo huu unatia aibu na kinyaazitoo ni nani katika chama mpaka apingane na wakuu wake hakuna demokrasia katika hili huyu ni msaliti na chama kichukue hatua dhidi yake faster au wananchi tuchukue hatua???????msaliti na auawe uchi na aibu imrudie mamaake.;;;
Zitto Kabwe ameeleza kuwa ni kweli walipiga kura na kukubaliana watoke wakati Rais akizungumza, lakini wao walipinga na ndiyo maana aliamua bora asiingie ndani ya Bunge, amesema kuwa yeye kama Zitto na wenzake aliona ni bora kutoingia kuliko kuingia na kutoka wakati Rais ambaye ndiye alama ya Bunge na Amiri jeshi mkuu akiongeaa. kwa vile kutoka ulikuwa msimamo wa chama, basi yeye na wenzake wamekosea na hilo ni swala la Chama kwani wanaweza kuadhibiwa na chama kwa vile kura za kukubaliana kutoka ilishinda.
Zitto alisema kuwa wanasubiria hatma yake katika chama na kusema kuwa hiyo ndiyo gharama ya Demokrasia. Ila amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.
Source: TBC 1 News Bulletin
Huna sababu ya kuwachukia. Kuna watu vichwa vinafanya kazi. Wanamptisha waziri mkuu na wanaomba serikali inayoongozwa na mtu wasiyemtambua asikilize madai yao!!!!! Kuna haja ya kufikiria upya strategies za namna hii. Zitto anatambua wazi kuwa strategy hii ni fake maana February watakuwa bungeni na wanahitaji kujadili hotuba ya Rais. Wakisusa kwa CCM ni mteremko tu maana hata utendaji wa serikali hawataujadili na kwa kifupi CCM watapeta zaidi. Nadhani aliyeshauri strategy hii alisahau kuangalia mbeleni. Mnakumbuka kura za maruhani Zenji? CHADEMA wanayaweza haya?
Zitto Kabwe ameeleza kuwa ni kweli walipiga kura na kukubaliana watoke wakati Rais akizungumza, lakini wao walipinga na ndiyo maana aliamua bora asiingie ndani ya Bunge, amesema kuwa yeye kama Zitto na wenzake aliona ni bora kutoingia kuliko kuingia na kutoka wakati Rais ambaye ndiye alama ya Bunge na Amiri jeshi mkuu akiongeaa. kwa vile kutoka ulikuwa msimamo wa chama, basi yeye na wenzake wamekosea na hilo ni swala la Chama kwani wanaweza kuadhibiwa na chama kwa vile kura za kukubaliana kutoka ilishinda.
Zitto alisema kuwa wanasubiria hatma yake katika chama na kusema kuwa hiyo ndiyo gharama ya Demokrasia. Ila amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.
Source: TBC 1 News Bulletin
zito unatuabisha please, ikiwa sisi wananchi wa kawaida tunawaunga mkono wewe mbona upo kinyume unajua hatupendi hayo mambo yako , tulikuamini sana ila sasa unapoenda sio, ivi unajua kuwa sisi tuna uchungu na nchi hii na tumekupa tu dhamana ya kutuwakilishi, ona akina Warioba, Jaji Mkuu maneno yao yantutia moyo .
Dear Zito , still you have an ample to change tunakupenda na tuna kuamini kindly usituangushe wala usituhudhunishe, when you fight you need to be risk taker, all the best,
MZEE GOMEZI
Kuna wakati nilikuwa nashirikiana na vijana fulani wa Kigoma katika kutatua tatizo lao, sasa mambo yalikuwa kama haya tunakubaliana hivi wao wanakwenda kinyume na makubaliano. Mtu mmoja akanishauri ya kwamba watu wa Kigoma wana kawaida ya kuwa kigeugeu hivyo niachane na shauri lao, sijui kuna ukweli juu ya hili? Maana tabia wakati mwingine zinaweza kutegemeana na asili yetu (mother land).Mimi nadhani ijapokuwa kutofautiana mawazo chamani ni kawaida, sio busara hata kidogo kuutangazia umma kutofautiana huko kwani hayo ni maamuzi ya ndani. Kwa kawaida watu mkishapiga kura wengi wakashinda mnakubaliana wote na unakuwa uamuzi wa pamoja. Huwezi tena wewe ukatoka nje ukasema mimi sikukubali. Hii ndiyo inayoitwa "colective responsibility." Kama jambo ni zito kiasi kwamba huna budi kutofautiana nalo hadharani hata baada ya kura kupigwa basi unajiuzulu kwanza. Lakini huwezi kupingamana na wenzako katika jambo liliopigiwa kura na kuamuliwa na wengi ukiwa wewe mwenyewe bado ni mmoja wao. Kitendo cha chadema kupiga kura katika uamuzi huo chaonesha kuwa kuna demokrasia ndani ya chama, na sio kuburuzwa na Mbowe kama watu wa propaganda za ccm wanavyopenda tuamini. Matamshi ya Zito yanaonesha kuwa ama ni mtoto kidemokrasia na utawala wa pamoja au ni kibaraka hatari wa ccm.
Huyu bwana mdogo mwangalieni kwa makini, kwani hata kama sio kibaraka kamili sasa, basi yuko mahali anapoweza kununuliwa kirahisi kutokana na uchanga wake. He is not stable, na siyo mtu wa kutegemewa katika maswala magumu. Don'nt trust him. Niliwaambia mapema kuwa watu wa aina hii watatumiwa sana na ccm miaka mitanao hii kukidhoofisha chadema machoni pa jamii. Lakini hawatafaulu.
naunga mkono kabisa, juu ya chama hiki kutofautiana kimtazamo, kam Mwalimu alisena kama unaona hukubaliani na maamuzi ya chama uwe dhahiri kuepuka unafiki na hii ndio kukua kwa demokrasia, cha msingi ni kuangalia maamuzi mnayochukua kutofautiana na wengine chamani hakileti madhara kiutendaji.
Numeipenda hii ingawa ningependa zaidi kam wote wangekuwa bungeni na kutoka, HII NDO DEMOCRACY!! express your feelings freely.
Nilicho fuarhi sana leo ni kauli za Jaji Mkuu na Jaji Warioba kuhusu mabadiliko ya katiba, CDM's votes were successuly registered, gud job people, sasa wameanza kupresha kubadili katiba, keep it burning Gud start.
democrasia hii ya CDM kama mzee King Kingo kinaweza kutumiwa kama mtaji wa kusambaratisha chama!! Lakini naamini Nguvu ya Mungu ni kubwa na it will keep these people united!!
wanaJamii Msichonge tu, wekeni chama hiki mbele ya Maombi ili alichoanzisha Mungu kiendelee kwa ukombozi wa watanzania
Asanteeeeee!!
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), walikaa chini na wakafanya demokrasia ya uamuzi kwa kupiga kura, hayo yote sisi hatukuyajua na yalikuwa ni siri ya Chama, kama hayakuwa siri, Katibu ama mwenyekiti wa Chama angetueleza (Kupitia vyombo vya Habari),
lakini kitendo cha Zitto kwenda kwenye vyombo vya habari na kuiongea hiyo siri ya vikao vyao ni USALITI, MIMI hapa simpingi Zitto kwa uamuzi wake aliochukua wa kutokubaliana na hilo la kutoingia bungeni kabisa, hiyo ni Demokrasia na ndio maana Chadema walipiga kura, ninachomlaumu na kumwona Zitto kuwa msaliti iweje aende kwenye vyombo vya HAbari na Kuropoka, Chama kitamwamini vipi tena katika siri zingine za kichama,
Zitto inampasa kuelewa kuwa Chama kina viongozi na kuna wasemaji, Mwenendo wa Zitrto ndani ya Chadema ni wakutia mashaka sana, kwa nini anapenda kwenda kwenye vyombo vya habari bila baraka za viongozi wake, Angalia issue kama ya mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni, nadhani kwake ilikuwa ni busara kusubiri maamuzi ya chama kupitia vikao vyao ili wapendekeze jina, lakini alikurupuka na kutangaza atagombea hiyo nafasi,
Ushauri kwa Zitto
ki ukweli kabisa siasa zako haziendani na Chadema kabisa, uko fast sana, una siasa za kipekeyako, za kibinafsi na sio za kichama, kama ukiwa kwenye Chama cha muhimu ni kufuata chama kinataka na kinasema nini, aina za Chama zinazokufaa ni kama TLP na NCCR, kwamba kila mtu anasema lwake