Zitto amefeli Leadership Qualities

Zitto amefeli Leadership Qualities

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,798
Reaction score
24,431
Tuingalie kutumia kurunzi ya leadership qualities and skills. Baada ya kwenda mahakamani na kuweka pingamizi, Zito alikuwa amejepiatia muda wa zaidi ya mwaka mmoja kujionesha kama kiongozi mzuri kwa kufanya mambo mawili tu:

(a) Kuunganisha tena wanachama wa chama chake ambao walikuwa wamekorofishana kutoka na ule "Mkakati;" halafu,

(b) Baada ya kukamilisha hilo la (a) hapo juu angekwenda mahakani kufuta kesi na kusema sisi sote na wamoja na tuna lengo moja, malumbano hayafai kwa hiyo hakuna kesi baina yetu.

Ila inaonekana Zitto alikuwa ama ana-buy time ili aendelee kuwa mbunge, au alikuwa na confidence kubwa sana kuwa atashinda kesi ambayo sote tunafahamu kuwa ameshindwa.

Ku-buy time ili aendelee kuwa mbunge siyo sifa nzuri ya uongozi kwani unakuwa ni kiongozi anayeangalia maslahi yake tu.

Vile vile kuwa na overconfidence kuwa utashinda halafu ukashindwa pia siyo sifa nzuri ya uongozi kwa utakuwa ni kiongozi atakayepeleka watu wake pabaya.

Vilevile nadhani CHADEMA wamekurupuka sana kumtolea uamuzi kwani iwapo kweli katiba ya CHADEMA inasema kuwa ukipeleka kesi mahakamani ukashindwa basi unavuliwa uanachama, ni afadhali wao wangekaa kimya tu ili wamuache Zitto mwenyewe ndiye apime msingi ya katiba ya chama chake, tendo lake la kwenda mahakani na matokeo ya uamuzi wa mahakama.

Huna haja ya kusukuma mzoga uzidi kuzama majini kama unajua kuwa tayari hauna uhai.
 
Tangu mwanzo wa mgogoro tulishauri kuwa kwa kiongozi kijana kama ZZK ilikuwa ni muhimu kuwa na washauri wenye mtazamo chanya badala ya wasaka tonge. Ninaamini bado ana nafasi ya kufanya mabadiliko na akabakia kuwa a young political icon kwa siasa zetu.
 
wachaga walishaamua kumng'oa zito baada ya yeye nakundi lake kutaka katiba ya chama ifanyiwe marekebisho pia safu ya juu ya viongoz ibadirishwe...!,mbaya zaid wanasiasa wakibongo wana tabia ya kukomoana bila kujali madhara ya pande zote...!uwepo wa zito chadema ulikuwa na umuhim wake,hivyo kukurupuka kumng'oa huenda pia kukaleta madhara makubwa sana kwa chama kuliko watu wanavyo dhania,km kumegeka kwa wafuas,siri za chama kuwa pasipo huska km na yeye ataamua kukomoa,jino kwa jino,akuanzae mmalize... n.k
 
Madhara yangekuwa yameshatokea wakat alipokuwa mbunge wa mahakama!!! CDM inasonga tu
 
Umakini wowote wa taasisi ni kusimamia miongozo yake hasa KATIBA. CDM haijamfukuza Zitto bali amejifukuza yeye kikatiba. Anaijua vizuri Katiba YA Chama na ameshiriki kwenye marekebisho yake. Ajipange kuomba upya uanachama au aanzishe chama chake .
 
Chadema imejifunga goli dakika za majeruhi, CCM itapeta tu uchaguzi October
 
Umakini wowote wa taasisi ni kusimamia miongozo yake hasa KATIBA. CDM haijamfukuza Zitto bali amejifukuza yeye kikatiba. Anaijua vizuri Katiba YA Chama na ameshiriki kwenye marekebisho yake. Ajipange kuomba upya uanachama au aanzishe chama chake .

Kwa stahili hili hii ya ubabe,Chadema bado sana kuchukua nchi.Bado chama hakijakomaa kidemokrasia.
 
Wakulu wa Chadema walishamchukia Zitto,wala msisingizie mahakama.Kilichotea ni kama mchezo wa kitoto,kuwa wewe si una nguvu mimi nina nguvu zaidi yako.
 
wachaga walishaamua kumng'oa zito baada ya yeye nakundi lake kutaka katiba ya chama ifanyiwe marekebisho pia safu ya juu ya viongoz ibadirishwe...!,mbaya zaid wanasiasa wakibongo wana tabia ya kukomoana bila kujali madhara ya pande zote...!uwepo wa zito chadema ulikuwa na umuhim wake,hivyo kukurupuka kumng'oa huenda pia kukaleta madhara makubwa sana kwa chama kuliko watu wanavyo dhania,km kumegeka kwa wafuas,siri za chama kuwa pasipo huska km na yeye ataamua kukomoa,jino kwa jino,akuanzae mmalize... n.k

Alitaka kupindua wafalme wa chama,kweli demokrasia kazi!!!.
 
WOTE MNAOMKOSOA ZITTO HAPA UMRI WENU NAONA NI MDOGO NA MNAONGEA BILA YA KUFANYA RESEARCH, NA MLIIDANDIA HII MELI MWAKA 2010, WAKATI PALE MWANGA WA NURU ULIPOTUFIKIA CHADEMA, MNASAHAU NI ZITTO, NA WENZAKE WAKONGWE NDANI YA CHAMA NDIO WALOKISAIDIA CHAMA KUONEKANA NI CHAMA CHENYE WATU MAKINI, NA WENYE MAWAZO YA KIMAGEUZI, LEO HII MBOWE KATEKWA AKILI NA WAKUJA AMBAO HATA HAWANA MIAKA 10 NDANI YA CHADEMA,.

MTOA POST HUJAFANYA RESEARCH YA KUTOSHA, NAHISI HIKI KITU KINACHOITWA "DURANTE BENE PLACITO NOSTRO" KINAUTESA UONGOZI WA JUU. SITAKI KUAMINI KUWA CHAMA KITAKUFA, NA SITAKI KUAMINI UTAKUA MWISHO WA ZITTO, HII VITA YA KUMZIMA ZITTO NI MIPANGO YA MAFISADI, WA CCM WAKISHIRIKIANA NA WAJINGA WACHACHE TENA WAKUJA NDANI YA CHAMA, AMBAO WAMEPEWA MADARAKA NOW WAMEKUA WANAKIBURI KIASI WANAWEZA KUMVUA YOYOTE UANACHAMA, KAMA KINA KIBATALA, MALLYA, LISSU, MABERE MARANDO, GODBLESS LEMA, NA WENGINEO WANGEKUWA WASAFI NA WAADILIFU kwanini walihama vyama vyao na kuja kujiunga na chadema, na kama ni mikakati yao ni kuiua chadema, NASEMA WASHINDWE, TENA WASHINDWE KABISA NA WALEGEE, MWISHO napenda kumpa pole ZZRK, kumptia moyo kuwa haya ndio maisha ya siasa, kwani umetufanyia mengi, mazuri japo BINADAMU MWEPESI KUSAHAU NDIO NATURE YAKE, ila pia hatujakamilikazzk kama binadamu anamapungu yake.

HAKI YA KWELI IPO KWA MUNGU DUNIA NI DHULUMATI.

PUMZIKA KWA AMANI RASTA MAN CHACHA WANGWE, JANA TAREHE 10 ZITTO KAFUTWA UANACHAMA NA WANACHAMA WALIOJIUNGA CHADEMA 2004. WAKATI ZITTO ANA ZAIDI YA MIKA 20 CDM.
 
kusita kutoa maamuzi magumu ndicho kinachoigharimu CCM,.Chadema wao wakiifanya kwa vitendo bado kuna watu wanadai si demokrasia..Hakuna cha funika kombe....
 
Chadema ni chama au saccos ya mbowe maana kila anayehoji uhalali wa mbowe basi ni msaliti endeleeni nanyi mtapata mavuno yenu kwenye sanduku la kura.
 
Lema amehamia Chadema mwaka 2009 Lakini ana nguvu kupita wakina Slaa na Mdee kisa ni kipenzi cha Mtei na Mbowe
 
Nashangaa wanaoshangaa maamuzi ya Chadema.... Zitto huyu wa siku hizi ni too complicated ...... unaona wazi amejaa roho ya kushindana na viongozi wake waliomlea kisiasa ........alitaka akapigiwe magoti? Huyu hawezi kufanikiwa chama chochote labda huko ACT ambako atakuwa Mungu mtu na kuwaburuza akina Kitila Mkumbo.
 
Ubabe wa kusimamia katiba ndio watanzania wanautaka.Wamechoshwa na UDHAIFU wa kiuongozi.
Hawataki mambo ya kulindana kwa kuitana mwenzetu pindi mtu anapokengeuka.
Hii ni tofauti sana na ccm.ChADEMA wababe wanaofuata katiba ilhali CCM wadhaifu wasiojali katiba,wanajiendea tu.
Kwa stahili hili hii ya ubabe,Chadema bado sana kuchukua nchi.Bado chama hakijakomaa kidemokrasia.
 
Back
Top Bottom