Zitto amburuza Kilewo polisi

Zitto amburuza Kilewo polisi

Status
Not open for further replies.
Zitto hana ushahidi wa kumtia hatiani Henry Kilewo, hiyo ni kutapa tapa maana hicho anachokilalamikia hakionekani.
Kwani wewe ndiyo unatafsiri sheria au wewe ndiye mpelelezi polisi na mahakama ndiyo watatoa ufafanuzi juu ya haya mambo wewe kula ndizi na kahawa tu huko machame.
 
Hii sasa itamuondoa bwana Zitto kabisa kwenye siasa za Tanzania,

Namuonea huruma sana kwani ataumbuka zaidi, ni heri atafute mshauri katika suala hili lakini kukimbilia polisi ni kukaribisha mauti ya kisiasa.

Wewe sasa yaweza kuwa kweli mnafiki,huyu traitor,na ushahidi uliweka (kama wa kweli) unamuhisi anataka kukuua!!!!!
Leo unamuonea huruma?????!!!Kabisa?????!!!!!

Nilitegemea ungekuwa na furaha ya msaliti kuteketea!!!!
 
WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.

Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.

Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.

“Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema Kileo.

Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.

-Tanzania daima.

Kwi kwi kwi teh teh teh

Kimenuka. Yericko Nyerere na Ben Saanane jiandaeni.
 
Last edited by a moderator:
Hii sasa itamuondoa bwana Zitto kabisa kwenye siasa za Tanzania,

Namuonea huruma sana kwani ataumbuka zaidi, ni heri atafute mshauri katika suala hili lakini kukimbilia polisi ni kukaribisha mauti ya kisiasa.
Sio rahisi kama upeo wako unavyofikilia,siasa is more than jf comments,siasa ni vitendo
ACTIONS SPEAKS LOUDER THAN WORDS.....
 
Hii sasa itamuondoa bwana Zitto kabisa kwenye siasa za Tanzania,

Namuonea huruma sana kwani ataumbuka zaidi, ni heri atafute mshauri katika suala hili lakini kukimbilia polisi ni kukaribisha mauti ya kisiasa.

Jitayarishe uende ukasema ule uzi uliounzisha JF wa tuhuma kwa Zitto chanzo chake ni wapi. Au uliutunga mwenyewe?
 
Last edited by a moderator:
Mimi hapa ndio napozidi kumuona Zitto ndumi la kuwili,kwa sababu kwenye press conference hakukanusha wala kufafanua waraka huu wa yeye kuhongwa pesa na pia kushirikiana na TISS na hata hajazungumzia uhusiano wake na Jack Zoka na Ighondu na mnyumbuliko wa pesa hizo kutoka NMB kwenda Ujerumani kwa Andrea na pia kuwatumia wakina Kitila,Mwampamba,Mchange,Ben Saanane,Juliana Shonza etc.

Baadala yake kakimbilia Polisi na kufungua defamation case ili suala hili liishe kimya kimya na kuepusha kwa Zitto kufafanua bali Kileo na obviously Polisi inajulikana kwenye siasa inavyotumika!!

Ben Saanane upo kwenye waraka ule kuwa ulitumiwa pesa na Zitto,please tueleze ulipewa kwa minajili gani??!!#### BEN SAANANE KAMA NA WEWE NI MMOJA WA WAPOKEA HUO MLUNGULA MAANA YAKE NA WEWE NI MIONGONI MWA WALE WALE WANAFIKI WASIOFAA NDANI YA CHAMA NI BUSARA UKAJIENGUA MAPEMA WAKABAKI WACHACHE WALIO SAFI AU FAFANULIA WANA CDM DHIDI YA SUALA HiLI
 
Kwani wewe ndiyo unatafsiri sheria au wewe ndiye mpelelezi polisi na mahakama ndiyo watatoa ufafanuzi juu ya haya mambo wewe kula ndizi na kahawa tu huko machame.

Hawa jamaa wanajichora sana,hawajui wanaongeza hisia za ukabila chadema,they better stay quit
 
Hii sasa itamuondoa bwana Zitto kabisa kwenye siasa za Tanzania,

Namuonea huruma sana kwani ataumbuka zaidi, ni heri atafute mshauri katika suala hili lakini kukimbilia polisi ni kukaribisha mauti ya kisiasa.
Tulizana wewe subiri kwenda segerea Zitto hawewezi kutaka huruma kutoka kwako, teh teh teh kumekucha.
 
....CHADEMA ni mpango wa Mungu
 
Kwani wewe ndiyo unatafsiri sheria au wewe ndiye mpelelezi polisi na mahakama ndiyo watatoa ufafanuzi juu ya haya mambo wewe kula ndizi na kahawa tu huko machame.

Hujakosea, maana bado tunasherekea uamuzi wa haki wa kamati kuu wa kuwafukuza wasaliti na wahaini, uamuzi ambao ccm hawathubutu kuufanya japo lichama lao limekaribia kuzikwa na ufisadi, wizi, ujangili, ugaidi na ubakaji wa watoto yatima
 
Jela zipo kwa ajili ya watu kama kileo,mjela jela siku zote panapomfaa ni jela tuh
 
people HATE each other because they don't know each other, they don't know each other because they do not communicate, and they do not communicate because they are separate.
YOU GUYS HATE ZZK BECAUSE YOU DON'T KNOW HIM.
 
usimchokoze kamanda Ben,ana ushahidi mtamu zaidi ya sms ya mpesa.Zitto anasubiriwa kwny mahakama ya wananchi

Ndio maana nimemwomba japo kidogo afafanue,mgao ule alienda kumlipia Zitto gharama ya kurekodi ule wimbo wa leka dutigite au vocha??!!

Kuna watu mi naonaga kero saana kuambiwa ni wasomi na wanaaminiwa,wakati ukiwatazama hata kwa kauli tu bila matendo unawaona upstairs ni hovyo na bora darasa la 7 kuliko PhD na masters zenye upogo Bali zinabebwa na publicity plus watawala!!
 
Kwani wewe ndiyo unatafsiri sheria au wewe ndiye mpelelezi polisi na mahakama ndiyo watatoa ufafanuzi juu ya haya mambo wewe kula ndizi na kahawa tu huko machame.

....ha ha ha ha yaani jamaa mpaka kakimbilia polisisisiemu
 
Tulizana wewe subiri kwenda segerea Zitto hawewezi kutaka huruma kutoka kwako, teh teh teh kumekucha.

Huyo mtu siku hizi hana tena thamani,mimi nikimuona humu ndan huwa nacheka sana,

Amedharaulika JF,amedharaulika mtaani anakofanya utapeli,na amedharaulika hadi pale UFIPA

Ni wa kuhurumiwa tuh
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom