yaani unatumia nguvu nyingi na kubwabwaja utafikiri huyo Zitto ndio amekuwa akiongoza hii nchi kwa miaka 50 na ushehi ama ndiye chanzo cha taifa kudumaa kimaendeleo...endelea kukumbatia ujinga wako.
Hivyo mkuu naomba nikuulize kitu, wewe unavyo imba kuhusu maendeleo unafikiri maendeleo ni nini hasa?
Matatizo yenu nyie watoto mlio lemazwa na Facebook, twitter, Instagram, Whatsapp na YouTube mna matatizo makubwa sana!
Baadhi ya matatizo yenu;
-kwanza napenda kukuambia ili uelewe kuwa nyie wengi wenu ni wazembe na wavivu sana (samahani),
-mbili hamtaki kujituma wenyewe kufuatilia vitu na kujishughilisha na historia ya nchi yenu na ulimwengu mnao ishi kwa ujumla.
Hivyo nyie mnafikiri kwamba kila kitu kinakuja chenyewe?
Aisee kijana jitahidi kujua historia ya maisha yako kwanza na ile ya wazazi wako na ikiwezekana ile ya babu na bibi zako wanako toka na jinsi gani waliishi mpaka leo wewe kama kiumbe kuweza ku-appear na ku-exist. Na sio kulopoka tu hapa vitu usivyo vijua, maadam umevisikia kutoka kwenye vijana wenzako kwenye ma-groups yenu. Umeenda shule wewe?
Miaka 50 iliyo pita Mambo yalikuwa mengine. Hiyo mitandao yenu haikuwepo.
Habari za nje sisi tulikuwa tunazipata kupitia radios (enzi hizo sisi waswahili wa Dar tulikuwa tunaziita Bomba)
hasa BBC London, magazines za nje Newsweek na Times na pia vitabu na magazines ambazo watanzania na wageni walio toka nje walituletea. Mara nyingi habari zilizopitwa na wakati. Hatukuwa hata na ile TV sembuse mtambo wa Television.
Kuna kipindi Magazine ya Times ilifungiwa kwa kuandika habari za uongo kuhusu Mwalim Nyerere kwamba amejilimbikizia mahela kibao kwenye account yake Uswiss, kitu ambacho hakikuwa cha kweli.
Mimi nimemzungumzia Zitto kwa sababu kuna watu wame soma naye chuo kikuu ambao nawafahamu na wanamjua jinsi alivyo. Kwa taarifa yako sio mtu wa kumwamini sana. Ni mtu ambaye anataka yeye awe mbele na aonekane kila kitu yeye ndiye anajua zaidi na anacho kisema ni cha maana zaidi kuliko mawazo ya wengine.
Pamoja na haya yote tulimpa credit ya kuwa one day angeweza kuja kutuongoza.
Sasa umejiuliza kitu gani kilimtoa yeye CHADEMA?
Unakumbuka Kufukuzwa kwake CHADEMA kuli kifanya chama na pia UKAWA kupoteza wafuasi wengi, kwani existence yake na activities zake kwenye kile chama kiliwapa watanzania wengi matumaini ya kuwa wapinzani wanaweza wakawashinda CCM na wakaongoza nchi. Lakini yeye kwa pupa zake za kutaka madaraka haraka haraka alitupilia mbali mategemeo hayo yote ya wananchi kwa kuamini kuwa yeye peke yake ndiye anaye weza kukifanya chama kikashinda uchaguzi na kuongoza nchi. Alisahau kuwa team Work ndiyo iliyo kuwa inawapa nguvu kubwa. Ni mistake kubwa sana aliyo ifanya! Nafikri utakubaliana na mimi kuhusu hili.
Kwa kufukuzwa kwake CHADEMA wananchi na wataka mapinduzi wengi ambao walikuwa wafuasi wake walio weka matumaini makubwa kwa CHADEMA walisononeka sana na hatimaye kuona kuwa kumbe viongozi wote ni sawa tu. Viongozi wa CHADEMA na CCM hawana tofauti yeyote.
Kama sio hitlafu ya viongozi wa CHADEMA, hayo niliyo yasema ya Zitto Kabwe na Dr Slaa na CCM kumweka Magufuli kuwa mgombea wao, UKAWA wangeshinda uchaguzi. Definitely! Na hivi sasa tungekuwa na serikali nyingine. Na kukiona CCM ni story. Mbona wa Zenji walifanikiwa kuitoa CCM? Hata sisi wa bara tungeking'oa hicho chama.
Matatizo yaliyotekea ni kwamba watu ambao tuliwapa credibility kama akina Zitto na Dr Slaa ndiyo walio tuangusha na kutufanya sisi tusiweze kukiondoa Chama Cha Mapinduzi, sijui mapinduzi gani Mwalim Nyerere na Karume waliyafanya mpaka chama chao wana kiita hivyo?
Hivi sasa ukiniuliza kama mimi ni member wa chama chochote Bongo, jibu langu ni NO! Lakini nampenda Magufuli na nina mwamini yeye na sio mwingine yeyote katika nchi hii, japo kuwa ana hitilafu fulani fulani, pamoja na hayo nikiziweka hitilafu zake kwenye mzani na kulinganisha na matendo yake anayo wafanyia watanzania naona bado ana credibility mkubwa sana yakuwa kiongozi wetu hata awamu yake ya pili. Sina shaka naye.
Nafikiri utakubalina na mimi mkuu CCM bara imeshinda kwa ajili ya Magufuli tu. Na kama siyo yeye sijui CCM wamekuwa wapi.
Above all these discrepancies my fellow tanzanian, I would like from the bottom of my heart to say only a couple of words to you, please try to be you! JUST YOU AS AN INDIVIDUAL! Jiamini!