Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 81
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto (pichani), amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumruhusu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akague matumizi ya fedha za chama wakati wa Uchaguzi Mkuu, mwaka 2005.
Kwa mujibu wa Zitto, uamuzi huo utathibitisha kauli za viongozi hao kuwa chama chao hakihusiki na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Zitto alitoa ushauri huo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Lamadi, wilayani Magu, mkoani Shinyanga mwishoni mwa wiki. Alisisitiza kuwa haitoshi kwa viongozi wa chama hicho kutamka tu kuwa chama chao hakihusiki bali wamruhusu CAG ili athibitishe kitaaluma.
Maelezo hayo ya Zitto pia yanaweza kutafsiriwa kama majibu kwa Mweka Hazina wa CCM, Amos Makala ambaye wiki iliyopita alisema chama chake hakihusiki na wala hakikushirikiana na kampuni yoyote kuiba fedha za EPA.
Makala alitoa kauli hiyo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Katika kukanusha kwake, Makala alisema hata Msajili wa Vyama vya Siasa amethibitisha kuwa CCM hakihusiki na wizi wa fedha Benki Kuu, na kwamba wanasiasa wanaohimiza upotoshaji huo wanastahili kupuuzwa.
Lakini akihutubia wananchi, Zitto alisema; Iwapo CAG ataruhusiwa kukagua hesabu za CCM na kuweka hadharani matokeo ya ukaguzi huo, Watanzania wataweza kuridhika kwa sababu wengi wanaamini CCM ilichota fedha EPA, Benki Kuu na kuzitumia katika kampeni.
Nilimsikia Mweka Hazina wa CCM Amos Makala akisema CCM haikuchota fedha za EPA. Kama kweli hawakutumia fedha za EPA katika kampeni zao basi wamruhusu CAG akague hesabu zao na za vyama vingine na majibu ya ukaguzi huo yawekwe hadharani, alisema.
Mtanzania iliwasiliana na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, John Chiligati, kuhusu changamoto hiyo kutoka kwa Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Katika majibu yake Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema; Huyo Zitto hana jipya lolote alilosema na hizo ni porojo za kisiasa zisizokuwa na maana au tija yoyote kwa wananchi.
Alisema hesabu za CCM zilikwishakaguliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa ambaye hufanya kazi hiyo kwa mujibu wa sheria.
Kila mwaka hesabu zetu zimekuwa zikikaguliwa na si za chama chetu tu na hata vyama vingine vya siasa. Sisi hatuna cha kuficha, kama wapo wengine wanataka kukagua waje tu, ila anachosema Zitto ni porojo zisizo na maana, alisema Waziri Chiligati. by Na Maregesi Paul, Magu -Mwananchi
My Take:Ofisi ya msajili wa vyama lazima watakuwa wanafanya mahesabu na si kwa CCM tu bali hata kwa vyama vingine.
Je ofisi ya msajili wa vyama imesimamia wapi juu ya hilo, au wenyewe hukagua fedha walizotoa wao tu, kama ndiyo wazo la Mh Zitto ni zuri sana, wananchi wajue fedha za kampeni ile zilitoka wapi, wazibue mirija yote.
MJ