Zitto aivaa CCM, Chiligati apuuza

- Kumbe sheria ipo sasa tatizo lipo wapi?

Kaka,
Msajili wa vyama hakagui hesabu za vyama. Yeye hupokea hesabu ambazo zimekaguliwa na wakaguzi wa vyama kwa rekodi. Hatua inayopaswa kufuatwa ni kwa CAG kukagua hesabu hizo kwa vyama vya siasa ni taasisi za umma kwa mujibu wa sheria na. 5 ya mwaka 1992.
Vyama pia hupata fedha za ruzuku ambazo ni fedha za umma na kwa mujibu wa sheria za fedha za umma, CAG ndio mwenye mamlaka ya kikatiba kukagua matumizi ya fedha zote za umma.

Hakuna chama cha siasa ambacho CAG anakagua. Tumejaribu kupeleka muswada Bungeni ili kuweka wazi kwenye sheria ya vyama vya siasa ili mkaguzi akague, CCM wamegoma na muswada ukachomolewa dakika za mwisho.

CCM walitumia fedha za EPA katika kampeni za uchaguzi mwaka 2005. Walitumia pia fedha za Benki Kuu mwaka 2000 na mwaka 1995 walisaidiwa na Mugabe kwa maombi ya Mwalimu Nyerere. Njia pekee ya CCM kujichomoa katika hilo ni kukubali mkaguzi akague hesabu zao. CHADEMA tupo tayari.

Next step, Accounting Officer wa CCM aunganishwe na kesi ya EPA ili kujibu tuhuma za kufaidika na Proceeds of Corruption kwa mujibu wa sheria ya PCCB ya mwaka 2007.

Salamu kutoka Mwanza
 
Zitto Kabwe said:
Walitumia pia fedha za Benki Kuu mwaka 2000 na mwaka 1995 walisaidiwa na Mugabe kwa maombi ya Mwalimu Nyerere.

Zitto Kabwe,

..hapo utagombana na Mwanakijiji,Bibi Ntilie,Jasusi,Rev.Kishoka, na vigogo wengine wa JF.

..hizo ni tuhuma kali sana umeelekeza kwa Baba wa Taifa.
 
...Tumejaribu kupeleka muswada Bungeni ili kuweka wazi kwenye sheria ya vyama vya siasa ili mkaguzi akague, CCM wamegoma na muswada ukachomolewa dakika za mwisho.

Mheshimiwa Zitto,

Nadhani ni wewe tu ndio huwa unasema umeleta miswaada. Wengine - na hata leo Sitta mwenyewe kasema - wanasubiri miswaada ya Serikali.

Hebu naomba unisaidie kidogo hapo kuhusu mpangilio wa kupitisha miswada.

Mlileta muswada ukawa voted down bungeni au ?

How and who controls the tabling of bills, CCM ?

Kwa utaratibu gani wa Standing Orders ?
 
Mheshimiwa Zitto,

Nadhani ni wewe tu ndio huwa unasema umeleta miswaada. Wengine - na hata leo Sitta mwenyewe kasema - wanasubiri miswaada ya Serikali.

Hebu naomba unisaidie kidogo hapo kuhusu mpangilio wa kupitisha miswada.

Mlileta muswada ukawa voted down bungeni au ?

How and who controls the tabling of bills, CCM ?

Kwa utaratibu gani wa Standing Orders ?

Hapana. Hatukuleta muswada ukashindwa Bungeni. Serikali ilileta muswada wa mabadiliko ya sheria ya ya vyama vya siasa. Ilipofika kwenye ngazi ya kamati tukajipanga na kupeleka ammendments na zikapita kwenye ngazi ya kamati na muswada ukawa tayari kwa kuwasilishwa Bungeni.
Unceremoniously muswada ukaondolewa kwenye order paper siku ya kuwasilishwa baada ya kikao cha kamati ya uongozi wa wabunge wa CCM.

Kuna njia nyingi kwa wabunge kuifanya serikali iwajibike. Ikiwemo maswali ya msingi na nyongeza, maelezo binafsi, hoja binafsi, taarifa ya Mbunge, muswada binafsi nk.

Wabunge wengi hutumia njia ya maswali tu. Toka mwaka 1999 Bunge limekuwa na hoja binafsi moja tu, ya Buzwagi. Toka mwaka 1995 Bunge limekuwa na Muswada binafsi mmoja ambao haujawasilishwa - sheria ya Maadilii. Mara ya mwisho Mbunge kuwasilisha muswada binafsi Bungeni ni Jenerali Ulimwengu mwaka 1995.
Kanuni zinaruhusu yote niliyotaja hapo juu. Spika ana udhibiti mkubwa kuhusu miswada ya wabunge lakini wabunge wa CCM ndio wenye uamuzi wa mwisho kwani wao ndio wengi ndio maana utume wangu kwa Taifa ni kumaliza ukiritimba wa chama kimoja bungeni - ending single party dominance
 
Kinachofanya nimpende Zitto na kuwa shabiki wake namba moja ni jinsi anavyokuwa rahisi kuja hapa kujibu hoja zinazoelekezwa kwake na chama chake.
Hivi sisiemu wanasubiri nini nao kuja mtandaoni kujibu tuhuma zao?
Kuhani si kisheria ukisomewa kosa na ukaamua kukaa kimya mahakamani, mahakama ina haki ya kukuona una hatia? au ni uelewa wangu mdogo wa sheria?
Nauliza je nikikaa kimya mahakamani nisijibu lolote, inaonyesha ni kama nimekubali kosa?
 
Toka mwaka 1999 Bunge limekuwa na hoja binafsi moja tu, ya Buzwagi. Toka mwaka 1995 Bunge limekuwa na Muswada binafsi mmoja ambao haujawasilishwa - sheria ya Maadilii. Mara ya mwisho Mbunge kuwasilisha muswada binafsi Bungeni ni Jenerali Ulimwengu mwaka 1995.
...Unceremoniously muswada ukaondolewa kwenye order paper siku ya kuwasilishwa baada ya kikao cha kamati ya uongozi wa wabunge wa CCM.

.... wabunge wa CCM ndio wenye uamuzi wa mwisho kwani wao ndio wengi ndio maana utume wangu kwa Taifa ni kumaliza ukiritimba wa chama kimoja bungeni - ending single party dominance

Sawa.

Hizo statistics za miswaada binafsi ni absolutely appalling.

Sasa hicho kigezo cha uwingi wa CCM ndo nina tatizo, especially kuhusiana na hivi vikao nje ya Bunge.

Ni hivi, Zitto, hiki "kikao cha kamati ya uongozi wa wabunge wa CCM" siku zote kitakuwa na wabunge wa CCM tu! Si ndio ? Hata CHADEMA ingekuwa madarakani. Sasa sidhani kama sheria inakipa chama tawala uamuzi wa miswaada gani ije bungeni ipi isije kwa kulazimisha kuipitisha kwenye hii bottleneck ya "kikao cha Kamati ya uongozi wa CCM." Utaratibu gani huo kisheria (statutory ama Standing Orders) ?

Ningependa kujua miswada binafsi inakwamishwa wapi kwa nguvu gani ?

Muswada wako wa sheria ya Maadili ulisema Marmo aliuwekea mizengwe mpaka ukafa kifo cha mende. Well, japo yeye ni Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu, taratibu za Bunge, lakini Marmo anapata wapi nguvu za kuamua miswaada gani iende, ipi isiende ? Executive branch haijapewa nguvu ya kuliamulia Bunge mpangilio wa kuleta miswaada! Kwa katiba ya Tanzania - najua utashtuka kusikia hii idea - lakini kwa structure ya Katiba ya Tanzania, Bunge la Tanzania ndio linatakiwa liwe executive!! Linasimamia Serikali! Linatakiwa liwe juu ya Serikali. Kwa nini mkubali mizengewe ya Serikali ?

Nitachopenda kuona mimi ni miswaada inafika Bungeni halafu inakuwa voted down na CCM halafu wananchi wanaona. Lakini mkikubali iwe inaishia ishia huko kwenye vikao na kamati za vificho vificho vya CCM wananchi hawataweza jua. Utakuja hapa utatulelezea watu 50, mia, wa Jamii Forum lakini the preponderant of the masses hawana clue kuhusu michezo ya chini chini ya CCM.

Halafu, kingine, usipokazana sana ku assert hizi rights za kisheria, kama zipo, za kufikishiwa miswaada yako bungeni unaweza kuanza kuoneka kama unatumia kisingizio tu. Kwamba, ""aaaah, nilileta muswaada wakaukataa... wao ni majority." Halafu ikawaje ? "aaaah, tunasubiri tuwe majority!" Kama ni hivyo basi the minor party hakina haja ya kuwepo Bungeni!
 
Kama kuna njia ya kuiweka miswada hii open, na voting records open, ningeshauri tuwekewe ili tujue mbunge gani anapiga kura kwa maslahi ya taifa na mbunge gani ni mnazi wa CCM tu.

Maana kuna wengine wanajua sana kuongea lakini ikifika kwenye voting records wanakuwa wanafyata baada ya kuimbishwa nyimbo za CCM.

Je, kuna njia ya kupata hizi voting records ili hata kesho keshokutwa zitumiwe kwenye kampeni?
 
Kama kuna njia ya kuiweka miswada hii open, na voting records open, ningeshauri tuwekewe ili tujue mbunge gani anapiga kura kwa maslahi ya taifa na mbunge gani ni mnazi wa CCM tu.

Maana kuna wengine wanajua sana kuongea lakini ikifika kwenye voting records wanakuwa wanafyata baada ya kuimbishwa nyimbo za CCM.

Je, kuna njia ya kupata hizi voting records ili hata kesho keshokutwa zitumiwe kwenye kampeni?

Bro, the electorate is not that sophisticated.....ndio tatizo la kukaa Marekani muda mrefu!!
 
Back
Top Bottom