Zitto airarua serikali; abeza Rais kulalamikia matatizo badala ya kuyatatua

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, ameitaka serikali ichukue maamuzi ya haraka ya kulinusuru taifa na tatizo la umeme nchini, kwani uzoefu unaonyesha ndiyo imekuwa ikichelewesha na wakati mwingine kukwamisha uwekezaji wa miradi mikubwa ambayo ingeweza kulipatia taifa umeme wa uhakika.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (CHADEMA), aliyasema hayo wakati akisoma ripoti ya mapendekezo ya kamati yake kuhusu tatizo la umeme, ambayo kwa kiasi kikubwa imeonyesha kuwa uzembe na urasimu ndani ya serikali umechangia kwa kiasi kikubwa taifa kukosa umeme wa uhakika na kujikuta likiingia gizani mara kwa mara.

Akisoma maazimio hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alilitaka Baraza la Mawaziri chini ya Rais Jakaya Kikwete kufanya maamuzi ya haraka ili kukamilisha miradi ya umeme wa makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma, aliyosema ina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha na wa uhakika.

Alisema wakiwa katika ziara ya siku tano ya kukagua mradi wa Liganga na Mchuchuma, walibaini kuwa ipo haja ya haraka kwa serikali kutimiza wajibu wake kufanikisha utekelezwaji wa haraka wa miradi hiyo na kwamba wanaunga mkono hatua zilizofanywa na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kwa kukamilisha hatua za kumpata mbia kutoka nchini China.

Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutaifanya nchi inufaike kwa kupata umeme wa Megawati 1500 KV ndani ya kipindi cha miaka mitano na kuendelea, ambao unaweza kuzalishwa kwa takriban miaka 150 kabla ya makaa ya mawe kwisha.

"Hatuwezi kuwa na taifa la walalamikaji kila mara…. rais, wabunge na wananchi wote sasa tumekuwa walalamikaji lakini muhimu ni kwa baraza la mawaziri kufanya uamuzi wa haraka ili kuinusuru nchi na tatizo la umeme. "Hata kampuni tanzu itakayoundwa ili kuendesha miradi hii ifuate taratibu zote za uchimbaji ikiwamo kusainiwa kwa mkataba wa uendelezaji wa mgodi kwa madhumuni ya kulinda masilahi ya taifa na watu wa Ludewa," alisema Zitto.

Alisema NDC wameingia ubia na Kampuni ya Atomic Resources ya Australia na kuunda Kampuni tanzu ya TANCOAL Energy wilayani Mbinga kwa lengo la kuzalisha umeme wa megawati 450, ambapo shirika hilo litakuwa na hisa ya asilimia 30 na uwekezaji wake utakuwa ni dola za Marekani milioni 350.

"Mkataba wa ubia kati ya NDC na Kampuni ya Sichuan Honga kutoka nchini China ili kuendeleza mradi wa Mchuchuma na Liganga ni vema ukasainiwa haraka na serikali," alisisitiza Zitto.

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), alisema Wizara ya Nishati na Madini inatakiwa kuharakisha utoaji wa leseni ya uchimbaji wa makaa ya mawe kama ilivyokuwa imeombwa na Kampuni ya TANCOAL ambayo inamilikiwa kwa ubia na NDC ili uchimbaji huo uanze na umeme uzalishwe.

Kwamba, umefika wakati kwa TANESCO kuanza kuwekeza katika msongo wa kusafirisha umeme kuelekea kwenye miradi hii ili iwe ya maana, ikiwa ni pamoja na suala la msongo wa umeme kuwa chini ya TANESCO.

Akifafanua kuhusu mradi wa umeme wa makaa ya mawe wa Kiwira, alisema kamati yake inaunga mkono hatua ya mashirika ya umma kuwekeza katika sekta ya uzalishaji wa umeme na Shirika la Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF), kujitokeza kuendesha mgodi huo.

"Kamati yetu mwaka 2009 ilikwenda nchini Malaysia na kukuta mashirika ya mifuko ya hifadhi za jamii yamewekeza na kuzalisha umeme megawati 27,000 huku wakiwa na akiba ya megawati 12,000 ya umeme katika nchi yao, je, Tanzania tunasubiri nini?" alihoji Zitto.

Alisema kamati hiyo itakuwa na mkutano na wadau wa kujadili miradi ya umeme ambapo mkutano huo utawakutanisha NDC, STAMICO, TANESCO,NSSF na CHC pamoja na makatibu wakuu wa wizara na wenyeviti wa kamati za Bunge za Viwanda, Biashara, Nishati na Madini ili kujadiliana kwa pamoja na kupata njia mbadala zaidi.

Akijibu maswali, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe, alisema kamati yao imefuatilia na kubaini kuwa mchakato wa kurejesha umiliki wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira na kubaini kuwa mchakato huo bado haujakalimika kama ilivyokuwa imeelezwa
 
“Hatuwezi kuwa na taifa la walalamikaji kila mara…. rais, wabunge na wananchi wote sasa tumekuwa walalamikaji lakini muhimu ni kwa baraza la mawaziri kufanya uamuzi wa haraka ili kuinusuru nchi na tatizo la umeme. “Hata kampuni tanzu itakayoundwa ili kuendesha miradi hii ifuate taratibu zote za uchimbaji ikiwamo kusainiwa kwa mkataba wa uendelezaji wa mgodi kwa madhumuni ya kulinda masilahi ya taifa na watu wa Ludewa,” alisema Zitto.
Hiki ni kijembe live kwa baba-mkwe wetu jk!...
Wape somo Zitto!, watafanya usharobaro wee, lakini mwisho wa siku wataona aibu na kutekeleza japo nusu ya ushauri wako!
 
Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutaifanya nchi inufaike kwa kupata umeme wa Megawati 1500 KV ndani ya kipindi cha miaka mitano na kuendelea, ambao unaweza kuzalishwa kwa takriban miaka 150 kabla ya makaa ya mawe kwisha.

Hapo kwenye red, utakuwa unamaanisha Megawatt 1500, au ungeandika 1500[MW]. Nikirudi kwenye maada, serikali ndo wamefanya umeme sehemu ya kufisadi taifa, sehemu ya kujipatia umaarufu kwa wanasiasa na ni sehemu ya kutafutia hela za kampeni. siku tukipata umeme wa uhakika tutaona wanasiasa wa kweli na waongo.
 
Zittto anatafuta umaarufu kwa kutumia shida ya umeme. Sasa anashindana na Makamba. Wao serikali lolote jema. Ikosaini mkataba baraka watasema wafisadi Hao. Wakichelewa wazembe hao.

Huh urais 2015 sijui utaipeka wapi Tz!!!
 
Zittto anatafuta umaarufu kwa kutumia shida ya umeme. Sasa anashindana na Makamba. Wao serikali lolote jema. Ikosaini mkataba baraka watasema wafisadi Hao. Wakichelewa wazembe hao.

Huh urais 2015 sijui utaipeka wapi Tz!!!
Kha! wewe vp, Zitto anatimiza majukumu yake, acha chuki za kipumbavu. Mbona zitto maarufu kuliko........
 
Tatizo letu si kuwepo kwa resorces, tatizo letu ni serikali iliyotopea kwenye rushwa. Hii miradi mingi haiendi kule inakotakiwa kwa wakati muafaka kwa sababu watu wanachezesha mduara ili hatimaye ifikie a "Richmond like" contract halafu ndo mambo yaende. Sasa hivi wenye majukumu yao ya kiutendaji, waziri wa Madini na Nishati pamoja na Tanesco wenyewe, wamezamishwa vichwa vyao kwenye mchanga! Kamati za Bunge ndo ziko bize utafikiri bunge ndo kimegeuka chombo cha utendaji.

Watendaji wenyewe watakapoibuka, litakuwa li-IPTL lingine. Naamini hata Zitto analijua hili tatizo. Serikalini hakuna pragmatic approach kama Zitto anavyotaka iwe. Ndo maana wengi tunalinyooshea vidole li-CCM lenye serikali. Hawa watu siku zote wanaambiwa. Lakini hali ilikofikia ni kuwa hawaambiliki. "Superstructure" yote ya government iko compromised kwa hiyo maamuzi ambayo yanaonekana logical na ya wazi kabisa unashangaa inachukua miongo kuyatekeleza na yanapotekelezwa ni uozo mtupu.

Utashangaa hadi tunaingia kwenye ma-IPTL, Ma-Richmonds, Ma-Dowans, n.k. Haya ma kina Mchuchuma, Liganga, Kiwira si yalikuwepo? Kwa nini tokea hapo tukaingia kwenye miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta, ambayo ni gharama kubwa kwani mafuta tunaagiza, wakati hayo ma-reserves ya Coal tunayo na tunajua kuwa tunayo toka Uhuru? Kiwira imekuwa ikizalisha makaa kwa kitambo sasa (toka miaka ya 80's); hivi haikuwahi kuwajia akilini viongozi wetu kuwa Kiwira ilikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme? Tatizo ni kuwa watu walikuwa bado wanatengeneza Michongo!

Matatizo haya hayawezi kuisha bila CCM kuondoka madarakani, haiwezekani. Zitto, approach yako ya kwanza iwe ni kuhakikisha hawa CCM wanaondoka madarakani. Ukianza kuwapelekea mapendekezo, haisaidiii hata kidogo. Mapendekezo lukuki yamejazana kwenye makabrasha na mashubaka ya offisi za Tanesco na Wizara ya madini. Hayafanyiwi kazi na yakifanyiwa kazi tunaona uozo wa Richmond aka Dowans!

Kwa hiyo Mheshimiwa Zitto, Mie nakushauri urudi kwenye ile approach yako ya mwanzo kabisa. Yaani u-focus katika kuing'oa CCM madarakani. Hizi pragmatic approach unazozipendekeza zitafanya kazi tu pale mitandao ya ulaji rushwa ndani ya serikali (web of corruption) itakapong'olewa. Vinginevyo mtakuwa mnapoteza muda na Energy bure!
 
hili limekaa vema, tatizo ni kuwa nssf na ndc wakifua umeme, rostam atakula wapi? mgao wa umeme ukiisha rostam atakula wapi vile? pesa za kampeni itakula kwao akina makamba, hili halitatokea hata kama ni kwenda kwa babu wa loliondo wataenda
 
Zittto anatafuta umaarufu kwa kutumia shida ya umeme. Sasa anashindana na Makamba. Wao serikali lolote jema. Ikosaini mkataba baraka watasema wafisadi Hao. Wakichelewa wazembe hao.

Huh urais 2015 sijui utaipeka wapi Tz!!!

Ulitaka asemeje ili asionekane anatafuta urais? Watu waache kufanya kazi zao kisa wasije onekana watafuta urais-huo ni uzube mwingine!
 
Back
Top Bottom