Zitto afunika Igunga

naona CCM na CUF haina haja ya kuendela na kampeni wanapoteza muda na rasilimali za vyama vyao bure....
 
My GAWD!!!! Igunga haijawahi kuona umati kama huo katika maisha yake yote! Muulize mtu yoyote pale mwenye umri mkubwa atakueleza hivyo. Kilichobaki kwa CCM ni kufanya kawaida yao ya ujambazi waliozoea na kunyang'anya kwa nguvu. Namna nyingine hakuna. Najua CCM watasema wote hao hawakujiandikisha.

umeona ee, CCM wakiona huo umati wao wanaimarisha kamati ya uchakachuaji, lakini siku za ukombozi zinakuja, kitaeleweka tu. Ukiona mikutano ya CCM ina umati mkubwa fanya uchunguzi ni msanii gani alikuwa anapaform, lakini chadema ni sera za ukombozi tu, no time for cheap politics.
 
Jana TBC walirusha mapokezi yake na mkutana wa hadhara, ilikua nyomi mbaya! lazima pachimbike Igunga!
 
Hakika Igunga wameona maajabu katika kampeni hizi sasa uamuzi ni wao maana Pumba na Mchele vyote viko Igunga .
 
Najaribu kuwaza CCM watatokea wapi huko Igunga. Nilimsikia Mbunge wao mmoja mwanamke akiwahutubia wanavijiji kama kumi katika eneo moja ati CDM ikishinda kutakuwapo vita kama vile Burundi. Mie nadhani CDM wakienda eneo hilo waende na bango la Rage na bunduki yake kiunoni ili wanavijiji hao wajue ni akina nani hasa wako tayari kwa vita.

huyo mwanamke alinikera, nilitamani kumzaba vibao kwenye TV. Eti bora kuwa maskini lakini amani, wakati wao wenyewe ndio wanaanzisha vurugu kuwatisha wananchi. Ila saizi pumba zinaonekana wazi, watu wanaelimika taratibu
 
umeona ee, CCM wakiona huo umati wao wanaimarisha kamati ya uchakachuaji, lakini siku za ukombozi zinakuja, kitaeleweka tu. Ukiona mikutano ya CCM ina umati mkubwa fanya uchunguzi ni msanii gani alikuwa anapaform, lakini chadema ni sera za ukombozi tu, no time for cheap politics.
ccm huwa inawasaidia sana watz maskini waliowanyonya na kupigika ili waweze kuhudhuria matamasha ya bure ya muziki ambayo hawawezi ku-afford, kwa hiyo wananchi wanajua pale ishu ni muziki tu lakini wakienda kwenye mikutano ya cdm huwa wanasikia sera makini na kuombwa wawapigie kura na bila hiyana wananchi wanatekeleza!
 
Mkuu mbona siamini amini hivi ni kweli au? Aisee natamani nije huko igunga, mbona raha jamani hadi 'masaburi' yangu yanawasha kwa jinsi yalivyohamasika. Mbona mwafaidiiiiiiii!!!!!!!!!!
du!!! kumbe chadema kuna baadhi ya watu c ridhiki!!!!!!!
 
Naona Zitto anang'ara sana this time. Chadema HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Nimeiangalia hiyo clip ya video na nina nadhani CCM wainue mikono juu tu, ili Igunga iwe salama. Na hapo sijaona watoto wa shule, sijawaona waliopewa kapelo na T-shirt za chama. Kama hawa wapo, basi ni wachache mno wa kuhesabu.
na pia hakukuwa na KIKUNDI CHOCHOTE CHA BURUDANI
 
mwita kumbe kingereza chako ni cha kuunga? Hajasema chemical ally bali ni comical from comics wewe wawapi kumbe unatumia google translator? Mwita ccm oye
wewe unachanganya habari, yule waziri alikuwa haitwi chemical Ally.
 
igunda-zitto1.jpg
Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe akizungumza na wananchi kwenye uwanja uliopo nje ya ofisi za chama hicho Wilaya ya Igunga baada ya kumpokea kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi mdogo wa kiti cha Ubunge wa jimbo hilo jana.​
 
Kampeni sawa lakini kumbukeni kuna kibarua cha kulinda kura zenu, sasa kama makamanda wenu wanaishia lupango si ndio maadalizi ya uchaguzi kuchakachuliwa.

09_11_ujnw37.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom